mabuba
Senior Member
- Dec 5, 2006
- 133
- 90
Niwetu, tumewatoa, Maungoni,
Ni wetu, tumewaleta, Ulimwenguni,
Ni wetu, tumewalea, duniani,
Ni wetu tumewabinafsisha.
Ni huria, tumewaacha, Sokoni
Ni huria, tuwachuuzia, hadharani,
Ni huria, twauzia, dukani,
Ni wetu tumewabinafsisha.
Soko, tumeliachia, kutulelea wanetu,
Soko, tumelisusia, wetu
Soko, tumelikazia, amali zetu,
Ni wetu tumewabinafsisha.
Tabia zao, zimenyumbulishwa, hewani,
Mienendo yao, imezungukiwa laanani,
Utu wao, umemengenyuliwa vitani,
Ni wetu tumewabinafsisha.
Mavazi wajinunulia, sasa wavaliana,
Waume wake watamaniana, Mavazi kuchukulina,
Haya usoni hawana, Wabaki kutamaniana,
Utandawazi tumewaachia, watoto unatulelea.
Walimu tumewachia, watoto kutulelea,
Walimu wamejichokea, wana wetu kutushikia
Walimu nao wamesusia, watoto kutukamatilia,
Utandawazi tumewaachia, watoto unatulelea.
Wabadilisha chaneli, pasikuwa makatazo,
Sasa, wameleta digitali, pande zote nivikuwazo,
Movi zao tumekariri, wametufanya hamnazo,
Utandawazi tumewaachia, watoto unatulelea.
Haki za binadamu, zimeshika yake hatamu,
Jamii haina hamu, kwenda polisi kwazamu,
Watoto sasa ni bomu, risubiliwalo kuzimu,