Ggadafi
Member
- Jun 22, 2022
- 9
- 11
Habari zenu wadau! Bila Shaka mko vizuri, poleni na majukumu
ebana, nashangaa sana na sifurahi nimwonapo kijana msomi, tena aliyezaliwa kijijini akihangaika mijini na maisha ya kuungaunga na elimu yake kichwani.. unaanzajaje kuondoka kijijini sehemu ambako kuna fursa chungu nzima, et unaenda ambako hujuwi unachoenda kufanya?
Mwingine anasema hawezi kukaa kijijini kwa kisingizio kwamba hakuna miundombinu ya kutosha mara oh sijui nini.. (hiyo ni sawa na baba kuikimbia familia yake et kwa sababu nyumbani mwake hakuna chakula cha kutosha) unafikiri ni nani atakuja kuondoa mapungufu yako kama sio wewe?
Ndio maana kuna baadhi ya maeneo kuna umasikini mkubwa sana lakini wasomi waliozaliwa hapo ni wengi tu lakini nyumba zenyewe zipo zile za nyasi. Jamaa unasubiri TANESCO wakipeleka umeme hapo sasa ndo uanze kufikiria ukafungue mradi ! mkalete maendeleo vijijini kwenu..
🤔🤔 Nimesahau nilichotaka kusema ila sawa, huenda ningetukanwa