Tumia mafuta ya habat soda (black seed oil) kutibu magonjwa mengi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
MATUMIZI ya mafuta ya habat soda ni mengi sana katika mwili wa binadamu lakini leo utajifunza na kufaidika na haya machache ambayo ninayaandika hapa chini:

KWA AFYA
Kunywa kijiko kimoja cha mafuta haya asubuhi na usiku, tena asubuhi unaweza kunywa kabla ya kifungua kinywa. Unaweza kunywa kijiko kimoja cha mafuta peke yake au ukachanganya na kijiko kimoja cha asali safi.

HAMU YA KULA
Kabla ya kuanza kula, jipatie kijiko kimoja cha mafuta hayo kisha kunywa maji ya kawaida au yaliyochanganywa na siki kidogo.


VIPELE, CHUNUSI NA NGOZI
Changanya na pasha moto kwa dakika mbili kikombe kimoja cha habat soda iliyosagwa, ½ (nusu) kikombe cha maganda ya komamanga yaliyosagwa, na ½ (nusu) kikombe cha siki ambayo inatokana na juisi ya tufaha (apple). Paka sehemu inayotakiwa kabla ya kwenda kulala kila usiku mpaka vipele (chunusi) vitakapoondoka. Mchanganyiko huu unaweza kukaa mpaka wiki tatu, ni lazima uuweke katika hali ya baridi.

PUMU
Weka kijiko cha habat soda iliyochemshwa katika maji yaliyochemshwa kisha unywe ikiwa ya moto.

KUTIBU MGONGO
(sehemu ya chini)

Changanya asali pamoja na ¼ (robo) kijiko cha habat soda kunywa kabla hujala kitu chochote wakati wa asubuhi.

KIBOFU/FIGO

Kama unasumbuliwa na kibofu cha mkojo au figo, tumia asali kila asubuhi kabla ya kufungua kinywa. Changanya vikombe viwili vya habat soda iliyosagwa na ½ (nusu) kikombe cha asali safi.

Kunywa kijiko kimoja cha mchanganyiko huu pamoja na kikombe kimoja cha maji ya moto kila asubuhi kabla ya kufungua kinywa. Mchanganyiko wa asali na habat soda unaweza kukaa kwa siku 15 tu na hifadhi kwenye baridi.

KIKOHOZI
Tumia matone matatu au manne ya mafuta ya habat soda kwenye kahawa au chai.
Kunywa kijiko kimoja cha habat soda na asali mchana na usiku. Pia kwa wenye matatizo ya kutokwa na haja ndogo (mkojo): Kunywa kijiko kimoja cha habat soda pamoja na asali, kisha kunywa maji ya uvuguvugu.

NGOZI KAVU
Kwa wale wenye ngozi kavu changanya asali pamoja na robo kijiko cha mafuta ya habat soda, kunywa wakati wa asubuhi kabla ya kufungua kinywa.

MINYOO:
Kunywa habat soda pamoja na siki kuondoa minyoo ya aina yoyote ile, inaweza kuwa ya limao au ya tufaha apple.

KICHWA
Kama unasumbuliwa na kichwa, chukua unga wa habat soda, karafuu iliyosagwa nusu, kijiko cha habat sauda kisha uchanganye.
chukua kijiko kimoja cha chai kisha kunywa na mafuta yake unaweza kupaka kichwani.

USINGIZI
Kama una tatizo la kukosa usingizi, chukua kijiko kimoja cha habat soda changanya na maziwa glasi moja pamoja na asali kijiko kimoja kikubwa kisha kunywa.

SIKIO
Chukua tone moja la mafuta ya habat soda nyunyizia ndani ya sikio husaidia kulisafisha na kuliponya kabisa.

MALENGELENGE
Chukua mafuta ya habat soda jipake mpaka yaishe.

MARADHI YA WANAWAKE
Tumia mafuta ya habat soda, kunywa kwenye kila kinywaji cha moto, unaweza kuweka kijiko kimoja kwenye maziwa, kwenye maji ya moto, kwenye supu n.k.
Mbali na matatizo hayo pia inasaidia kusafisha kizazi na ni rahisi kwa mwanamke asiyezaa kushika mimba kwa haraka.

KUSIKIA VIZURI
Mtu mwenye ugonjwa wa kutosikia achemshe habat soda na karafuu, anywe bila kuongeza kitu chochote mara tatu kwa siku atapona.

VIDONDA
Kama una kidonda changanya matone kumi ya mafuta ya habat soda katika kikombe cha asali na kijiko kimoja cha maganda ya komamanga yaliyokaushwa na kusagwa. Kula mchanganyiko huu kabla ya kula chakula baadaye kunywa glasi ya maziwa yasiyotiwa kitu chochote.
 

Attachments

  • 264px-Nigella_sativa_oil.jpg
    21.9 KB · Views: 1,649
  • Habat sauda.jpg
    9.9 KB · Views: 1,504
  • Nigella_Sativa_Kalonji_Oil.jpg
    34.9 KB · Views: 1,488
kumbe haya mafuta yana faida nyingi hivi! mimi nimepona moyo ulikuwa unauma sana na kuhisi kupooza, maana upande wote wa moyo ulikuwa unauma. nilitumia mafuta 'black seed oil' kijiko kidogo x3 kila siku, ndani ya siku 3 nilikuwa nshapona.
 
Kwa mwanza tutapata wapi jamani na vip beizake na kwawanywaji haina matatizo?
 
Kwa mwanza tutapata wapi jamani na vip beizake na kwawanywaji haina matatizo?

nenda kariakoo kama upo dar. nakama mikoani nenda kwenye maduka yanayouza madawa ya kiarabu.au dawa za kisuna. utapata. kiboksi kimoja kwa dar ni tshs 5000
 
Kwa mwanza tutapata wapi jamani na vip beizake na kwawanywaji haina matatizo?

mwanza nenda soko kuu.lango kuu lakuingilia nenda moja kwa moja utakuta jamaa wa kipemba wanauza madawa ya kiarabu utaipata pale mwambie nataka habat souda ya mafuta ni shs elfu 10 kwa boksi
 
Daah, Shukrani sana Lady.A kwa ushuhuda huu. Nimeyanunua jana namtumia Mama yangu Mzazi ana matatizo kama yako naamani yatamsaidia kama yalivyokusaidia wewe.
kumbe haya mafuta yana faida nyingi hivi! mimi nimepona moyo ulikuwa unauma sana na kuhisi kupooza, maana upande wote wa moyo ulikuwa unauma. nilitumia mafuta 'black seed oil' kijiko kidogo x3 kila siku, ndani ya siku 3 nilikuwa nshapona.
 
Last edited by a moderator:
Acha nikanunue nimpe mtoto wangu maana anasumbuliwa na kuwasha/kuuma sikio na amesafishwa Muhimbili na kupakwa dawa kwa wiki 6 lakini tatizo liko pale pale. Asante MziziMkavu kwa tiba hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…