DustBin
JF-Expert Member
- Jun 3, 2021
- 609
- 604
Mitandao ya kijamii imeleta faida kubwa sana katika maisha yetu ya sasa. Miongoni mwa faida zake lukuki ni kuwakutanisha watu kutoka sehemu mbalimbali za dunia na kuwa ndugu wa ukoo mmoja. Mimi ni miongoni mwa wanufaika wa mitandano hii ya kijamii, hasa mtandao wa Whatsapp.
Mwaka 2012 niliungwa kwenye group moja la Whatsapp, rafiki yangu ambaye nilisoma nae chuo kikuu aliniunga. Lile group lilikua na members 15 tu kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania. Wengi wakiwa wahitimu wa vyuo vikuu waliojiajiri kwenye shuguli mbalimbali, wachache walikua watumishi wa serikali na mashirika binafsi na wengine waliobakia ni wafanyabiashara wa daraja la kati. Baadhi yetu tulikua hapa Dar-es-Salaam, wengine Arusha na Mwanza, kuna mwingine wa Morogoro, kuna mmoja wa Mtwara na wawili kutoka Zanzibar. Ingawa kundi lilikua na mrengo wa dini, maana members tulikutana kwenye makundi mengine ya dini. Kundi hili liliundwa kwa dhumuni la kuinuana kiuchumi.
Tulipata wazo la kusaidiana, na kwa kuwa tulikua na wataalamu wa fani mbalimbali basi hilo alikua tatizo kila mtu alitumia taaluma yake kuchangia mawazo ili tuweze kufikia malengo. Lengo letu lilikua kusaidiana kila mmoja wetu baada ya miaka kadhaa awe amepata msingi wa biashara utakaomsaidia kuendesha maisha yake. Tulipeana kazi la kila mmoja kubuni wazo la kibiahsara na kutoa makadirio ya gharama. Kila mmoja alifanya hivyo na kuhudhurisha makadirio yake na kuonesha matarajio ya biashara yake. Kutokana na hali duni tuliyonayo tulikubaliana kila mmoja wetu atasaidiwa mtaji wa milioni sita (Tsh. 6,000,000/-) ambazo ataziingiza kwenye biashara yake na ataanza kurejesha kiasi cha shilingi laki tano (Tsh. 500,000/-) kila baada ya miezi minne. Kwa hiyo ndani ya mwaka atarejesha milioni moja na laki tano tu (Tsh. 1,500,000/=). Ndani ya miaka minne atakua amerejesha kiasi chote.
Tuliweka utaratibu kila baada ya hiyo miezi minne kila mtu anatoa hicho kiasi cha laki tano ili apatiwe mtu mwingine, na milioni moja inawekwa kama salio kwa ajili ya dharura na gharama muhimu za uendeshaji. Kwa siku za mwanzo lilikua ni jambo zito sana, lakini kwa kuwa tuliaminiana na kwa sababu wote tulikua tumefungwa na jambo la dini hivyo tulijilazimisha kuwa wavumilivu. Tunamshukuru Mungu mwaka wa kwanza tulifanikiwa kuwapa watu watatu milioni sita kila mmoja na ndani ya mwaka huo huo tuliweza kuwatembelea kwenye biashara zao na kuona maendeleo. Na kupitia safari hiyo ndio mimi nilifanikiwa kuwajua members wengine kwani wengi tulikua hatujawahi kuonana, bali tuliaminiana kwa ule ukaribu wetu lakini jambo la dini lilituunganisha zaidi.
Mwaka 2013 tulifanikiwa kuwapatia members wengine watatu, na zoezi liliendelea hivyo mpaka mwaka 2017 ambapo members wote tulikua tumeshapata ule mgao wa mtaji. Na tunamshukuru Mungu hadi hivi sasa kila mmoja wetu ana biashara yake na wengine biashara zao zimekua kubwa. Na members wengine wale wenye biashara zao tangu zamani walitumia hizo fedha kwa ajili ya kulipia watoto karo na matumizi mengine ya nyumbani. Wao lengo lao lilikua ni kuwawezesha wengine ambao hawakua na cha kuanzia katika biashara.
Japo tumefikia malengo lakini tumepitia changamoto nyingi sana ambazo kama tungekua na nyoyo laini tungeishia njiani. Kuna wakati baadhi ya members huchelewesha kutoa fedha hivyo anajitolea mmoja kuziba lile pengo na yule member akipata fedha anamrejeshea. Lakini kusubiri zamu yako ifike nalo linahitaji moyo wa subira sana. Maana kama umeanza kuchangia tangu mwaka 2012 alafu zamu yako inafika 2016 ni mtihani. Kweli maendeleo hayaji ndani ya muda mfupi, kikubwa ni malengo uvumilivu, na moyo wa kutokata tamaa.
Lakini pia inahitaji moyo wa kujitoa (commitment) ya kila member na kila mmoja aone lile jambo ni la kwake. Hivyo ile hisia ya kuona ni jambo lako inaleta uwajibikaji wa kutekeleza majukumu uliyopewa.
Mtandao wa Whatsapp umetukutanisha ukatufanya tukawa ndugu, na zaidi umetusaidia kuinuana kiuchumi. Baadhi yetu wamefungua viwanda vidogo vya kufyetulisha matofali, wengine duka la hardare, mwingine ana shamba la kumwagilia, mwingine ana mashine ya kukoboa na kusaga nafaka na wengine ni mawakala wana mobile banking services. Ninashauri na wengine tutumie mitandao katika mambo yenye tija, mnaweza mkabuni mpango wenu sio lazima uwe unafanana na mpango wetu kwani kuna namna nyingi tu za kuweza kusaidiana. Kwa mfano sisi tuliwahi kuwaza tukusanye fehda kama milioni kumi hivi kisha tukanunue shamba huko rufiji tulihudumie tulime mazao mbalimbali. Lakini tukasema ngoja tuanze na hili kwanza na kama tutajaaliwa huko mbele basi tunaweza kutekeleza mpango mwingine. Hivyo hii mitandao iwe msaada kwetu na isiwe ni mzigo kwetu ikatuletea hasara.

Upvote
3