Tumia utulivu kuchagua kwa sababu kesho nawe utachaguliwa na ulichokichagua

Tumia utulivu kuchagua kwa sababu kesho nawe utachaguliwa na ulichokichagua

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
344
Reaction score
926
TUMIA UTULIVU KUCHAGUA KWA SABABU KESHO NAWE UTACHAGULIWA NA ULICHOKICHAGUA ✍️

Hamna namna utakwepa kuchaguliwa na ulichokichagua, swali ni je kipi ulikichagua ?

1.Kozi uliyochagua kuisoma chuo bila shaka na yenyewe ilishakuchagua.

2.Aina ya mahusiano uliyochagua na yenyewe yalishakuchagua au yatakuchagua tu.

3.Uvivu uliochagua na wenyewe kesho utakuchagua .

4.Ukiachagua kutumia tu bila kuwekeza basi uzeeni utachaguliwa pia na mtindo ulioishi.

JE UFANYAJE ILI KUEPUKA MADHARA MAKUBWA PINDI UNAPACHAGULIWA NA CHAGUO LAKO BAYA?

1.Usitafute mtu wa kumlaumu.
2.Jua upo unalipia machaguo yako
3.Hakikiaha unakuwa mtulivu sana ili usirudie tena makosa .
4.Tumia matokeo hayo kama darasa la kujitathimini mfumo wako wa maisha.

Mwanasayansi Saul kalivubha
Fikia Ndoto zako.
 
Kwaufupi uchawa unalipa sana kuliko kozi yoyote
Ajira hawatoi
 
Waswahili wanasema, ukichonga kinyago chonga ukipendachoo manake waweza enda uza kisiuzike, mwishowe waweza jiwekea ndani mwako
 
Back
Top Bottom