Tumjibu Askofu Gwajima Kisayansi na si Kisiasa, tuache kumshambulia na kumtishia. No research no right to speak

Halafu mavuvuzela wa Gwajima Chameleon wengi karibu wote ukiwauliza kwa nini wanataka uthibitisho wa chanjo miaka 10 mbele na kwanini isiwe 20, 30,au 50 au miaka 5 jibu watakuambia
dawa ndio muda wa uthibitisho.
Nani kapanga hiyo miaka waulize wakupe jibu.

Kwa ugunduzi wetu au wa hao hao wanaotupa dawa na chanjo kila siku !!?

Je chanjo ba dawa tutumiazo toka tuwe nchi huru tulishadai uhakika wa miaka 10 mbele.

Wajinga sana. Wanasahau computer zenye nguvu kabisa zimegunduliwa ndani ya miaka ya 50 tu iliyopita.

1970 windows computer hata mouse yenyewe au cd au dvd vitu hivi havikuwepo duniani, labda kwa Billgates huko.

Flash ilipotea bongo watu wengine walikuwa wanazivaa shingoni kwenye chain. !!! Ilikuwa uvbuzi wa kutisha 60mb !!!!

Lakini upuuzi wowote wa Gwaji Chameleon wanapiga vuvuzela sijui ndg zetu mmelogwa na huyu Chameleon.

Sambamba na uvumbuzi na ugunduzi ni kuokoa muda.

Muulizeni alipokuwa anaanza kile kanisa pale hunters pub ubungo alikuwa anaenda na Tablet au smartphone.
Ile clip ya kwichikwichi hatujaisahau pia.
 
Waziri wa afya ana watumishi wengi wenye sifa na ufahamu mkubwa, siyo tu wa chanjo ya UVIKO-19, zaidi ya 1m ya chanjo iliyoletwa awamu ya kwanza. Kama hao, ambao ndio wanapaswa kutoa mfano kuoonesha ubora na usalama ya chanjo, wanasita, kwa nini Gwajiboy abebeshwe lawama. Yeye, Gwajiboy anachukua tahadhari ili kondoo wake wasiangamie
 
THE HUNGRY MAN IS ANGRY.... 😂😂😂😂😂 NJAA MBAYA SANA.
Ndio maana kuna watu walipopata uongozi tu walitengeneza mkakati wa kuiba tu kwa miradi ya kinguvu hakika njaa mbaya sana hasa ukikulia sehemu yenye dhiki unakuwa na roho mbaya sana.
 

Umeshaambiwa kuchanja ni hiyari.

Ugonjwa wenyewe ni mgeni changamoto ya wizara zote za afya duniani ni kutoa elimu kuhusu huo ugonjwa na umuhimu wa chanjo kuondoa sintofahamu watu wajilinde.

Sasa wewe na huyo Gwajima wenu kutwa kupinga kwa hoja za kuokota okota mitandaoni.

Kwanza sioni kwanini unatetea Bishop Gwajima kukwepa fursa aliyopewa kuthibitisha madai yake; si ndio atawaumbua zaidi serikali.

Hiyo ni nafasi nzuri kwake sio tu kuonyesha ingredients za kwenye chanjo but also proving mawaziri walichanja maji mbele ya camera. You can do that aombe aletewe vaccine antibody test damu ya waziri itajibu kama kuna protein za kupambana na COVID kama amna mpaka leo basi yale yalikuwa maji.

Ifike mahala mjue upotoshaji una madhara, umeshaambiwa kuchanja sio lazima sasa kwanini uzidi kuogopesha watu; wakati mitungi ya oxygen ikikosekana hospitali watu wanailalamikia wizara na serikali sio kanisa la mtu.
 
Wow,I like this!
 
Tengeneza yako na wewe
 
Mkuu badala ya kumshambulia Gwaji boy tu tupeni na matokeo ya wale waliochanjwa, fuatilieni ndio utajua kwanini wengi hawaamini hiyo chanjo
Wewe personally unawafahamu wangapi waliochanjwa na wakapata madhara ?
 
Ndio maana kuna watu walipopata uongozi tu walitengeneza mkakati wa kuiba tu kwa miradi ya kinguvu hakika njaa mbaya sana hasa ukikulia sehemu yenye dhiki unakuwa na roho mbaya sana.
THE HUNGRY MAN IS ANGRY.... 😂😂😂😂😂 NJAA MBAYA SANA
 
Sijui kwanini kila nikimwona Askofu Gwajima anahubiri au anazungumza mahala popote pale hudhani ni Mgonjwa wa Akili amezidiwa na anahitaji Tiba ya haraka ili asije akafanya tukio baya kwa wenye Akili timamu.

Hata P kaunga mkono, basi hoja hizi afikishiwe na bi nanihii.
naunga mkono hoja.
p
 

Simtetei Gwajiboy ila nailaumu Serikali, hasa Mawaziri wa afya kudai anapotosha. Hana kesi ya kujibu kwa sababu ni swala la afya na uhai wa kila mtu. Kama chanjo ni bora na salama pasingekuwa na mijadala kote duniani. Kwa kauli yako, kote duniani, wanaohoji wakamatwe kuthibitisha?

Kama ni kuogopesha watu, Serikali ndio iko mstari wa mbele. Mawaziri wa Afya na wataalamu wao wanapaswa kuelimisha jamii kuhusu ubora na usalama wa chanjo ili wampuuze Gwajiboy. Kinyume chake nami nitaendelea kuhoji ubora na usalama wa chanjo, kwa SAUTI KUBWA

Ili kuthibitisha ubora na usalama wa chanjo hao Mawaziri wafanyiwe wafanyiwe hiyo "vaccine antibody test" kuthibitisha wana kinga ili jamii iamini na Gwajiboy aumbuke. Vinginevyo Gwajiboy ataendelea kuwapiga nyundo
 
Kama chanjo ni bora na salama, wahusika waelimishe jamii na hakika Gwajiboy atapuuzwa.

Je, wanaohoji ubora na usalama wa chanjo, dunia nzima wanatakiwa kuthibitisha? Ni wajibu wa mtengenezaji kuthibitisha. Hiyo ndiyo kanuni kuu katika tiba.
 

Waziri keshasema yeye binafsi yupo tayari kwenda nae popote kuthibitisha madai yake. Ataje mtu aliechanjwa maji atapelekwa atapimwa antibodies mbele yake.

Ina maana hata akitajwa yeye (waziri) yupo tayari kupimwa antibody, mbele ya mchungaji kuonyesha uongo wake.

Ndugu kuhusu usalama wa chanjo kuna nchi zishachanja 80% ya adults over the age 18 sasa hivi wapo kwenye majaribio ya chanjo kwa under 17.

Human trial ya under 17 years nimekuwekea video jana imeanza five months ago, sasa hivi bado wana monitor reactions za volunteers waliochanja, go ahead ya kuanza kuwachanja hilo kundi lote bado.

Kila kitu kinakwenda kutokana na medical requirements, hakuna short cuts.

Ngoja nikupe testimony yangu ya COVID mimi nilipata sasa kuna wengine reaction yao ni tofauti na hata hayo maelezo ya wataalamu wanaotupa ndio maana wanasema ni ugonjwa mpya ata wao wataalamu bado wanajifunza with new information.

Sasa what happened to me, to cut the story short mie nilipata mid March mwaka jana na elimu tuliyokuwa tukipewa attack ni siku 7-14 hiyo kwa wale wataopata homa. Basi homa kali likanitandika kama kwa siku 10 hivi ya 11 nikapona nikawa fresh kabisa.

Upumbavu wangu siku ya 12 nikanywa vodka (anyway nilikuwa najiona, poa kabisa) kilichotokea kesho yake ilirudi homa kali ya mara ya kwanza afadhali. Na hii ya safari ya pili nilikaa nayo kuanzia late March- mpaka mid May 2020, kwenye hizo siku leo unaamka asubuhi mzima jioni homa. Kesho siku nzima mzima, keshokutwa upo hoi na homa yaani ni up and down for six to seven weeks.

Na baada ya kupona in May nilikuwa sitoi makamasi kabisa yaani hata nikijaribu unatoka mvuke tu na aushuki unabaki juu baada ya dakika kadhaa huo mvuke unaganda inabidi uchokonoe pua kukakwangua ndio utoke na ukiushika ukoko wenyewe ni mgumu kama jiwe.

Hiyo hali nimeenda nayo mpaka mwaka huu April 2021 nilipopata jab ya kwanza, baada ya sindano usiku huo huo ndio makamasi yalianza kuchuruzika for the first baada ya karibu mwaka (bila ya kusahau ata mkojo wangu ulikuwa ni wa njano tu, ule wa rangi ya dehydration indication ata ninywe maji vipi).

Sasa nina uhakika kwa wale COVID iliyotupiga kwa homa ya week 6-7 kila mtu ana story yake; kuna dada namjua na yeye aliugua muda sawa na mimi; yeye mpaka December mwaka jana alikuwa kuna siku moja au mbili kwenye mwezi homa linamwendea mpaka alipochanjwa yeye ni nurse December ndio hiyo hali ilipoisha, kama mimi side effects zangu zilivyopotea.

So what am I trying to say COVID 19 bado wanasayansi wanajifunza madhara yake, however vaccine helps asikwambie mtu.

Tatizo la huyu Gwajima sio kupinga with merit na uongo juu anawatungia wahusika to justify his position, now that is just stupid.
 
Kitu kinaniuma kabisa ni mwanangu wa form one wakike eti kachanjwa sindano ya kinga ya kansa ya kizazi...siku hiyo katoka shule ananiambia mama tumechoma sindano asee niliumia na bado naumia..mpaka nataman nikafungue kes mahakamani...hata cjui hatma ya mwanangu akiwa mkubwa walah..
 

Pole kwa kupitia athari za kuambukizwa na kuugua UVIKO-19.

Maelezo yako ya kupona, baadhi ya athari za ambukizo, baada ya kupata chanjo yanazua maswali mengine ya kisayansi.
[emoji830]︎ kwamba ukiambukizwa ugonjwa wa kirusi ukapona unakuwa na kinga ya huo ugonjwa, je, iweje kuwe na ulazima wa chanjo?
[emoji830]︎ hizo athari za ambukizo baada ya kupona (homa, mafua makavu, nk) yaonekana ni baadhi ya madhara ya ugonjwa, je, wataalamu wa afya walikushauri nini kabla ya kupata chanjo?

Kwamba So what am I trying to say COVID 19 bado wanasayansi wanajifunza madhara yake, however vaccine helps asikwambie mtu inazua maswali anayouliza Gwajiboy. Isije kuwa chanjo kwako imekupa nafuu ya athari za kuambukizwa kuliko ambaye hajaugua kabisa?

Kwamba Tatizo la huyu Gwajima sio kupinga with merit na uongo juu anawatungia wahusika to justify his position, now that is just stupid ni maoni yako binafsi lakini kwangu maswali yake yamenisaidia kufanya maaumuzi sahihi kuhusu kuchanjwa au la.

Msimamo wangu uko palepale kuwa waliochanjwa, hasa viongozi walioonesha mfano wa kuchanjwa, akiwemo Rais SSH, wafanyiwe vipimo kuthibitisha kuwa miili yao imetengeneza kinga. Kinyume chake nami nitaendelea kuamini walichanjwa "placebo"

VIONGOZI watupe majibu ya kisayansi kuhusu ubora na usalama wa chanjo ili watu kama Gwajiboy wapuuzwe
 
Hizo stages haziwezi kuwa fupi kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia? Kama unaamini hizo stages kuwa inabidi zifuatwe, kwanini ushindwe kuamini hao walioziweka wanavyotwambia kuwa chanjo ni salama?
 
Pia anawazushia viongozi kuwa wamehongwa na mabeberu na pia walifeki kuwa wamechanja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…