Tumjue kidogo furaha mpya ya Manchester United Alexis Sanchez

Tumjue kidogo furaha mpya ya Manchester United Alexis Sanchez

mwanahabari93

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
263
Reaction score
170
Alex sanchez ni miongoni mwa majina ya wacheza yanayo tajwa sana katika dirisha hili dogo la Usajili na inaeelekea Mchezaji huyu mashuhuli wa kimataifa wa Chile atamwaga wino na mashetani wekundu. Mashabiki wasoka wa Manchester united duniani kote wametega masikio yao wakisubiri usajili wa Alexis ukamilike na kuamini kuwa atakuwa msaada mkubwa sana kuleta mafanikio Pale Old Trafford akishilikiana vizuri na wachezaji wengine mashuhuli kama pogba na Lukaku .

Habari ya Usajili wa Manchester United itakuwa habari kubwa kwa mashabiki wa Manchesrer united na itakuwa ni habari mbaya kwa vilabu pinzani kutokana na uimara wa mchezaji huyu pia nikutokana kuwa mchezaji ninayemuona kuwa katika kiwango cha dunia ukimtofautisha na wachezaji wengi pale Manchester untd wenye viwango vya kawaida

Huyu Alexis Sanchez ni nani?
Alexis Sanchez alizaliwa miaka 29 iliyopita Katika Mji wa Tocopilla katika Mkoa wa Antofogasta kaskazini Mwa Chile.Alianza amaisha yake ya soka akiwa kijana mdogo mwenye Umli wa miaka 17 katika timu ya C.D Cobreloa ya nchini Chile lakini baada ya Kumaliza msimu na timu hiyo alieelekea katika timu ya Udinese mwaka 2006 na alifanikiwa kuchukua ubingwa akiwa na timu hiyo lakini aliishia kutolewa kwa mkopo katika vilabu vya Colo-colo na River plate lakini mwa ka 2008 alifanikiwa kurudi kwenye timu yake ya Udinese aliecheza kwa mafanikio na baadae akapata bahati ya kuitajika kwenda kuitumikia miamba ya nchini Uhspania ilikuwa ni ndoto kwake kucheza sambaba na wa chezaji wa kubwa usajili wake ulifanikiwa £25millionna kuwa mchezaji ghali kutokea nchini chile na alicheza kwa mafanikio makubwa na kikosi cha Baarcelona sambamba na Lionel Messi na David Villa kwa kuchukua vikombe vya kutosha. Baada ya hapo mwaka 2014 akasaini mkataba na mzee wenger pale Arsenal kwa uhamisho wa £31.7million na kuwasaidia Arsenal kupambana kuiweka timu katika ubora wake na aliweza kuwa mchezaji muhimu sana pale kwa wabeba bunduki wa London.

Alex Sanchez ni mchezaji mwenye spidi ya hali ya juu anapokuwa Uwanjani na anayetumia nguvu anejua goli , anachenga za mauzi Alexis pia anweza kuwatoka mabeki kwa chenga zake za mauzi..Sio Man U peke yao wanaojua ubora wake bali hata vilabu vingine vinaelewa shughuli ya huyu Mchile ..itachukua mda mrefu Kwa Arsenal kupata mchezaji mwe kariba ya Alexis lakini pia swali jingne linalotawala midomoni mwa mashabiki ni Morinho ataweza kumuweka Sanchez katika kiwango chake bora kama alichokuwa nacho Aresnal? Bila shaka kwa nionavyomimi naamini Sanchez ni Mpambanaji na anweza kucheza na mfumo wowote. Tusubiri tuone kama kweli ataleta Furaha kwa mashabiki wa Machester untd au ataleta lawama hayo yanawez akutokea ndani ya muda mfupi kutoka sasa.

Karibu Sana”El nino Maravilla”(The wonder Kid)
 
Back
Top Bottom