Uchaguzi 2020 Tumkatae Magufuli, tumkubali Lissu

Swelana

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2016
Posts
418
Reaction score
1,259
Ni dhahiri kwamba uongozi wa Magufuli umetuumiza sana watanzania wote wa rika zote na kada zote. Kwanza kuna watu wametekwa na kuuawa na serikali haijawahi eleza chochote na ushahidi wa hawa watu kuuawa wananchi tunao, Ben sanane ametekwa na kupotezwa mpaka Leo wazazi wake hawakuweza kupata hata mfupa ili wazike na kupumzisha nafsi zao, roho zao zipo juu juu, utekaji huu na uuaji wa namna hii hatujawahi kuushuhudia katika awamu zote zilizopita na wala huwezi msikia Magufuli akiongelea hilo la utekaji na uuaji, sasa tumchague tena Magufuli wa nini?

Azory Gwanda amefuatwa na waliojitambulisha ni Polisi na wamempoteza, tena anafuatwa mbele ya mkewe na mpaka sasa si familia yake ipate hata kidole angalau wazike na roho zao zitulie, huyu ni mwandishi wa habari amepotezwa na kuuawa lakini huwezi kuona hata Magufuli kuliongelea hivyo, sasa tumchague wa nini?

Kuna watu wengi sana wameuawa na kupotezwa, wengine wamepewa kesi za kubambikiwa na wanaozea gerezani, Mdude Chadema amebambikwa kesi ya dawa za kulevya ili anyamazishwe, Tito na mwenzake wamebambikwa kesi ya uhujumu uchumi na wanaozea gerezani, sasa tumchague Magufuli tena Kwa lipi?

Wafanyakazi miaka 5 hawajaongezwa mishahara, mbaya zaidi wananyanyaswa makazini, achaguliwe Magufuli Kwa lipi? Wafanyabiashara wamefilisiwa na wengine wamenyanyaswa na kuporwa Mali zao Kwa lazima na utawala wa Chuma wa Magufuli, sasa achaguliwe Kwa lipi?

Wahitimu wa kada mbalimbali nao pia wamekumbwa na uhaba wa ajira na wanaendelea kutaabika mtaani bila matumaini ya ajira, sasa achaguliwe tena Kwa lipi? Wananchi wa kawaida wanaishi katika umasikini uliopindukia baadhi ya familia zinapata mlo mmoja kwa siku na zingine zimekosa kabisa, achaguliwe Magufuli tena Kwa lipi?

Wananchi wa vyama vya upinzani wametukanwa na kutishiwa kuuliwa na vikundi vya CCMMara Kwa Mara UVCCM imekuwa ikihubiri machafuko na hakuna hata aliyewakaripia si polisi wala Magufuli, sasa tumchague wa nini tena. Maovu ni mengi sana yaliyofanywa na Magufuli katika utawala wake, tumchague tena wa nini?

Ni wakati sahihi wa kumuweka pembeni Magufuli na maovu yake yote yaliyo dhahiri na tuambatane na Lissu ambaye amepigwa risasi na utawala wa Magufuli, yawezekana hata Mipango ya kupigwa risasi Lissu ilipangwa na Magufuli na genge lake,tumkatae Magufuli na uovu wake.

Niliyosema yote ni kweli na hiki ni kipindi cha kampeni hivyo mtuache tuzungumze kikicho cha kweli. Ni mengi sana maovu ametutendea Magufuli kuliko mazuri,tunkataeni na tulinde kura zetu Kwa damu na jasho ili Magufuli asiibe kura zetu.

Swelana.
 
Kataa ccm
Kataa uhuni wa ccm
Kataa uonevu wa ccm
Kataa unyanyasaji wa ccm
Kataa ubinafsi wa ccm
Kataa ufisadi wa ccm
Kataa utapeli wa ccm
Kataa ukabila wa ccm
Kataa mizaha ya ccm
Ikatae ccm kwa nguvu , akili na uwezo wako wote

Mpe kura mgombea yeyote wa CHADEMA kwenye eneo la kupigia kura.
 
Mkatae wewe na mkeo kwa kuwa mlikula pesa za walala hoi kwa muda mlefu, huku mkijifanya ninyi mna akiri sana kuliko wale masikini watozwa kodi.

Lazima muumie baada ya kutolewa kwenye ulaji.
 
Halafu nyie msozijua siasa sijui kwa nini mnaruhusiwa kupost haya mashudu yenu, hivi unayajua madhara ya mtu aliekosa uzalendo na kutumika na maadui dhidi ya taifa lake kwa maslahi yake?


Je kama amekosa uzalendo kwa taifa lake ni ipi thamani yake?
amani na thamani ya taifa ni bora kuliko mtu yeyote anaekosa uzalendo dhidi ya taifa lake.

Haya mambo bado ni mageni sana afrika kwa wenzetu ukitumika na maadui dhidi ya taifa lako kifuatacho ni kuuawa, bora hata hapa kwetu watu wanaonywa kwanza japo wanajitia ujuaji hadi yanawapata yakuwafika.
 
Magufuli hana uzalendo wowote, msitufanye sisi watoto bwana.
 
Magufuli hana uzalendo wowote, msitufanye sisi watoto bwana.
ungelizijua siasa zaidi ya unavozishabikia hapa sidhani kama ungefungua hilo bakauli lako dhidi ya magufuli, mabeberu wenyewe washachanganyikiwa dhidi yake hata huyo shoga wenu lisu anaujua ukweli, anajua kabisa hadi chanzo cha yeye kupgwa risasi ni kukosa uzalendo dhidi ya taifa, na naamini hua analijutia sana kosa lake japo nyie mazuzu hamuwezi elewa.
 
alafu nyie msozijua siasa sijui kwa nini mnaruhusiwa kupost haya mashudu yenu, hivi unayajua madhara ya mtu aliekosa uzalendo na kutumika na maadui dhidi ya taifa lake kwa maslahi yake?
je kama amekosa uzalendo kwa taifa lake ni ipi thamani yake?
amani na thamani ya taifa ni bora kuliko mtu yeyote anaekosa uzalendo dhidi ya taifa lake.

haya mambo bado ni mageni sana afrika kwa wenzetu ukitumika na maadui dhidi ya taifa lako kifuatacho ni kuuawa, bora hata hapa kwetu watu wanaonywa kwanza japo wanajitia ujuaji hadi yanawapata yakuwafika.
 
Nchi ya wenye raisi wa moyo ni ya ajabu sana kubadilika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…