Tumkumbuke Nicholaus Zengekala

Tumkumbuke Nicholaus Zengekala

Ladslaus Modest

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2008
Posts
635
Reaction score
27
Wapendwa wana JF
Leo ningependa tumkumbuke Hayati Nicholaus Zengekala ambaye alikuwa mwanamuziki asiyeona (kipofu).
Ninakumbuka Nyimbo zake kama SOLEMBA, na JACK MTOTO WA NAIROBI
Huyu ndugu kwa wanaomkumbuka aliuwawa katika mazingira ya kutatanisha; katikati ya miaka ya 80 ambapo mie hadi leo sijui kisa cha kilichopelekea kuuwawa kwake.

Ninawaomba wana JF wenye habari kuhusu huyu ndugu marehemu watupashe.
Asanteni.
 
aleemba ,solemba solemba ..aah aaaaaaaaaaaaahh.,,,

nilikupenda kimapenzi solemba ee..

ila tamaa uliweka mbele solembaa......

ulisema nikusubiri ...kumbe ulikuwa ukichungulia dirishani..

tangu asubuhi mpaka jioni ..sababu ya kukungoja wewe..nimeshtuka solemba ..nimeshtuka solemba....

sikutaki tena ..sina haja nawee nimeshapata mwingine anayenipenda kwa roho moja..

tafuta bwana mwingine utakayemwangaisha kama mimi....

JUWATA JAZZ HAO..BABA YAO..

MWANAKIJIJI TUWEKEE HICHI KIBAO PLEASE...

JAMAA ALIKUWA KIPOFU ALIKUFA KWA KUGONGWA NA GARI ..LATE OR MID 80 S
 
Mimi ni mmoja kati ya wale waliokuwa wanavutiwa sana na sauti muruwa na tamu ya Marehemu Nico Zengekala. Nilipenda sana uimbaji wake, ama hakika alikuwa na kipaji katika fani ya muziki hasa uimbaji.

Hata hivyo kumbukumbu zangu hazioneshi kuwa Marehemu Nico aligongwa na gari au kupigwa risasi. Nakumbuka kuwa aliumwa na baadae wakampeleka Pemba, nadhani ikashindikana, na hatimaye alifariki dunia.
Haya ndiyo ninayoyakumbuka, lakini mwenye kujua vinginevyo anaweza kunisahihisha
 
Hata Waswahili walisema "Kizuri hakidumu".
Huyu Ndugu alikuwa anaimba vizuri sana, enzi hizo nilikuwa sitoki pembeni ya redio yangu (dudu proof) ya mbao.

RIP Nico.
 
Mimi ni mmoja kati ya wale waliokuwa wanavutiwa sana na sauti muruwa na tamu ya Marehemu Nico Zengekala. Nilipenda sana uimbaji wake, ama hakika alikuwa na kipaji katika fani ya muziki hasa uimbaji.

Hata hivyo kumbukumbu zangu hazioneshi kuwa Marehemu Nico aligongwa na gari au kupigwa risasi. Nakumbuka kuwa aliumwa na baadae wakampeleka Pemba, nadhani ikashindikana, na hatimaye alifariki dunia.
Haya ndiyo ninayoyakumbuka, lakini mwenye kujua vinginevyo anaweza kunisahihisha
....Niliwahi kusikia kuwa Mzee Gurumo alimbana Kiasilia dogo ili asing'ae sana maana alikuwa tishio!!!
 
Ndugu zanguni, leteni habari kuhusu huyu mpendwa, alitutoka akiwa mbichi kabisa, angekuwepo hadi leo muziki wa kitanzania ungekuwa unaunguruma zaidi na zaidi.
 
Huyu mwamba amefariki mimi sijazaliwa kabisa lakini nyimbo zake ninazozijua nazikubali sana.
Sasa hivi nipo nasikiliza hasira hasara.
 
Back
Top Bottom