Ladslaus Modest
JF-Expert Member
- Jun 27, 2008
- 635
- 27
....Niliwahi kusikia kuwa Mzee Gurumo alimbana Kiasilia dogo ili asing'ae sana maana alikuwa tishio!!!Mimi ni mmoja kati ya wale waliokuwa wanavutiwa sana na sauti muruwa na tamu ya Marehemu Nico Zengekala. Nilipenda sana uimbaji wake, ama hakika alikuwa na kipaji katika fani ya muziki hasa uimbaji.
Hata hivyo kumbukumbu zangu hazioneshi kuwa Marehemu Nico aligongwa na gari au kupigwa risasi. Nakumbuka kuwa aliumwa na baadae wakampeleka Pemba, nadhani ikashindikana, na hatimaye alifariki dunia.
Haya ndiyo ninayoyakumbuka, lakini mwenye kujua vinginevyo anaweza kunisahihisha