Uchaguzi 2020 Tumpe kura huyu...

Johnson Alex Otieno

Senior Member
Joined
Mar 14, 2013
Posts
172
Reaction score
57
Hodi wana jukwaa.

Katika kipindi hiki cha harakati za wagombea na vyama vyao kuendelea kunadi kampeni zao ili kupata uhalali wa kuunda serikali zikiendelea bado najikuta nina maswali mengi ya kujiuliza.

Moja ya maswali yangu ni je serikali tutakayoipa mamlaka ya kuongoza nchi na wananchi itatulinda sisi wananchi na Mali zetu?

Msingi wa swali langu ni matukio tuliyoyasikia kupitia vyombo vyetu vya habari katika kipindi cha miaka mitano, katika kipindi hiki tumeshuhudia mengi haya ni baadhi tu

1. Kutekwa kwa watu muhimu na maarufu nchini, katika kipindi cha miaka mitano tumeshuhudia watu wakitekwa na kufichwa na watu wasiojulikana, mfano wasanii, wafanya biashara na waandishi wa habari.
Je serikali tutakayoiweka madarakani itatulinda dhidi ya uhalifu huu wa ubinadamu na Mali zao?

2. Mauaji ya hovyo hovyo, kwa miaka mitano tumeona ndg zetu na watanzania wenzetu wakiumizwa na watu wasiojulikana, serikali ya awamu ya tano ilishindwa kuwabaini hawa wasiojulikana, je tutoe fursa kwa walioshindwa kuwabaini watu wasiojulikana ili hali moja ya wajibu wa serikali ni kutulinda?
Naomba mnieleze nimpe nani kura yangu kwa maana napata wasiwasi wa kesho ya watanzania na Mali zao.

3. Je hizi kesi za uhujumu uchumi nani atazitatua kwa sheria na haki? Kwa miaka mitano nimesikia watanzania wakishitakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi, kwa mtazamo wangu nataka serikali tutakayoipa mamlaka iheshinu misingi ya kisheria na isiingilie uhuru wa nguzo zingine za nchi, serikali inayoamini yenyewe ndio nguo iliyojichimbia zaidi haina uhalali wa kuendelea kuongoza watanzania.

4. Maagizo kutoka juu, nataka tumchague mtu atakayekomesha hili neno, ndg zetu wanasota magerezani na vituo vya Polisi kwa kauli hii, aidha haki zao zinakanyangwa kwa maigizo kutoka juu, naomba kujua ni nani kati ya wagombea tulionao atakayekomesha maigizo kutoka juu?

5. Ni mgombea gani atakaye ruhusu uhuru wa waandishi wa habari na vyombo vyao,? Mathalani bunge letu tukufu kwa sasa wananchi hatuna fursa ya kujua kinachoendelea kwa kadri ya maagizo ya wachache, niambie ni nani nimpe kura ili arejeshe bunge mbashara na uhuru wa waandishi wa habari na vyombo vyao?

6. Niambieni nani ataongeza mshahara na kuamsha Ari kwa wafanyakazi wa umma, kwa miaka mitano woga na kujipendekeza vimetamalaki, nani ataweza kuhamasisha wafanyakazi hawa wafanye kazi kwa majibu wa taaluma zao?

7. Ni nani atatoa fursa za ajira kwa vijana bila kujali itikadi za vyama, kwa miaka mitano vijana wanalia na wasio na majina makubwa ndo hawana kabisa matumaini ya kesho zao.
Nambieni nani atarejesha tumaini kwa vijana wanyonge?

8. Naomba mnielekeze na nielewe Hivi kweli yupo mtu atakayeleta mabadiliko ya tozo kwa wafugaji na wakulima? Hivi yupo mtu atakayeregeza kodi kwa wafanyabiashara? Mtu huyo naomba kumjua ili nikampe kura yangu October 28.

Niambie ni nani atajibu na kuondoa mambo haya,?

Nataka kiongozi atakayewajua na kuwashughulikia watu wasiojulikana, awalete kwa wananchi na mahakama zetu ziwatendeee kwa kadri ya sheria zetu.

Nataka kiongozi atakayetambua kwamba mamlaka zote zinatoka kwa wananchi na akili hilo kwa maneno na matendo yake.

Bado na ngoja msaada kwa wajuzi wa siasa wanieleze kura yangu nimpe nani.
 
Lissu anatosha

Umenikumbusha Yule bwana tuliambiwa alikuwa Ana anahujumu uchumi kwa kuhamisha mil. 7 kila DK, aliachiwa kwa plea bargain,

Cha kushangaza Dpp alipokea mabulungutu kwa cash. Wakati tuna utaratibu wa e- gov. Payment.

Hii serekali ya kisanii sana
 
Tujitahidi kuondoa serikali yenye janjajanja nyingi
 
Jibu ni Jiwe!
Tumpe jiwe miaka mingine mitano!
Nitaeleza sababu kwanini tumpe jiwe kura zetu kwa kipindi hiki cha 2020-2015.
1. Kutekwa kutakwisha(Sasa hivi ataua kabisa hadharani kupunguza gharama za kumsafirisha mateka kumpeleka Dodoma, safe houses)
2. Wafanyakazi waache kazi maana wanadai mishahara haitoshi(hii itapunguza tatizo la ajira, unemployed watafill vacancies zilizotemwa na wafanyakazi).
3. Mamlka ya mapato Kisutu(Kisutu revenue authority) itaongeza pato la taifa kwa kukusanya faini za kutosha kutoka kwa "wahujumu uchumi"
4. Tutaongeza kiwanja cha ndege chato, international airport.
5. Hatutaiba trillio 1.5 tena, tutachukua trillion 10 kabisa, maana CAG ni wetu sasa hivi.
6. Tutaifuta katiba, neno la jiwe (maelekezo) yataongoza nchi.
7. Vyombo vyote vya habari vitachukua habari kutoka TBC, tutaachana na BBC, voa na DW, hii itapunguza gharama
 
Umeeleza vizuri sana mhujumu uchumi
 
Dah mkuu umejibu kiwepesi sana ingawa nayo ni majibu.
 
Jamaa amepwaya ili mbaya, ila faulo zake ndizo anaamini zitambeba;
1. Vyombo vya habari hasa luninga na redio kutoa habari zake tu
2. Vyombo vya dola kuhakikisha vinafanya figisu ya nguvu kwa wapinzani ktk kipindi hiki
3. NEC kuwa silaha ya mapingamizi na kufanya "delaying tactics" ili kuwatoa kwenye reli wapinzani
4. Rasilimali za taifa zitokanazo na kodi na maduhuli ya wananchi kutumika kukipendelea chama tawala
5. Kutumia njia za wazi ama vificho kuwatisha watu ambao watajitokeza kwa wazi kuunga mkono upinzani
5. Njama za kutaka kuwadhuru wagombea wa upinzani kupitia sumu za kijasusi wawapo majukumu
6. TCRA kutumika kama silaha kwa kutumia kanuni zake zilizo kandamizi
7. Green Guards kwa kificho cha jeshi la akiba kutumika kama sehemu ya kimkakati kufanya uhalifu ktk mikutano ya wapinzani.
8. Mengine GT mnaweza kuyaonngeza ili njia za waovu zikapate kubainika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…