Tumpe maua yake RPC wa Mwanza DCP Wilbrod Mutafungwa

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Sisi wananchi wa Mkoa wa Mwanza tunakupongeza sana kwa uchapaji wako wa kazi katika Mkoa wetu. Tangu ulipohamishiwa katika Mkoa wetu matukio mengi ya kihalifu yamepungua sana.

Katika funga kazi ya kukupa maua yako ni pale ulipofanikiwa kuwaokoa watoto wawili waliotekwa na wahalifu kwa kuwakuta wakiwa salama na afya njema. Kitendo cha kupambana na hao wahalifu na hatimaye kuwaua ni kitendo cha kishujaa sana. HONGERA sana RPC na vijana wako wote walioongoza zoezi hilo. Ninamwomba Mhe. Rais aone kama itapendeza upandishwe cheo kwa kazi nzuri unayoifanya katika Mkoa wetu wa Mwanza. Kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Mwanza NINAKUPA MAUA YAKO kwa kazi nzuri unazozifanya katika Mkoa wetu wa Mwanza.
 
Mmmhh! Wewe ni huyo RPC na hapa unajaribu kujipigia debe ili upate uteuzi wa Cheo Cha juu zaidi??
Endapo Kama kweli Jeshi la Polisi linachukia utekaji, kwa nini lisiaanze kuwasaka Wahusika waliofanya utekaji wa Watu mbalimbali Kama vile Azory Gwanda, Ben Saanane, n.k?
Kwa nini hawa Watu wanaodaiwa kuwateka hao watoto hawakukamatwa wakiwa hai ili waweze kulisaidia Jeshi hilo katika kufichua mtandao wa uhalifu?
 
MUNGU mwema CHADEMA hawajasingiziwa.....ingekua karibu na uchaguzi, na walivyo wavivu sasa, wangewadondoshea CHADEMA na issue ingeishia hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…