Albinoomweusi
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 3,433
- 8,585
Anaandika @exaud_msaka_habari
Kiukweli inawezekana Mkude ana mambo yake, ila baadhi ya sisi wanahabari na sisi tuna mambo yetu makubwa sana
Leo kuna watu wamenitumia Vitu DM kuwa sjui mkude kafuta picha alizovaa jezi za Simba zote nikasema sawa, Nikaona watu wameanza kupost tena watu naowaheshimu kabisa nikasema hebu ngoja nikaone
Naingia kwenye Page yake nakuta kafuta mpaka picha za mtoto wake na picha zake nyingine zote hadi aliyompost Kahata na hakuwa amevaa jezi kafuta
Cha ajabu ameacha Picha yake ya Profile kavaa zake jezi ya simba na hatujaiona, Ameacha utambulisho wake BIO kuwa yupo Simba na Taifa Stars na hatujaona hiyo
NIMEJIULIZA YAFUATAYO
1. Siku hizi mchezaji kufuta picha yake instagram ni Habari?
2. Kwanini story yetu haijamalizia kuwa ameacha picha ya Profile na BIO yake vile vile (lengo letu nini)
Alafu kesho tunakaa kwenye Redio tunasema wachezaji wazawa hawajitumi, hawana adabu na maneno kibao, wakati tunamzushia na kumchongea hatuoni uzawa wake? Wakati mwingine mtu unaona aibu kusema ni Mwanahabari yani