i

Naungana na wanao mpongeza Michuzi. Wana JF wenzangu naomba tufike mahali tuukubali ukweli na kuutawala utofauti wetu (managing divesity).

Blog ya Michuzi ndio blog kiongozi kwa habari motomoto kuwahabarisha na kuwaunganisha Watanzania wa nyumbani na ulimwenguni kote kwenye taarifa za shida na raha, lazima tukubali Michuzi anafanya kazi nzuri na anakubalika sana, tukubali, tukatae!.

Lakini pia lazima tumkubali Michuzi for who he is katika maamuzi yake na mrengo wa blog yake. Kama ameona mrengo huo ndio unalipa, mwacheni andelee hivyo hivyo hivyo kwani katika kutimiza malengo, ni jamii ndio inafaiidika hata kama katika kinu chake pumba ni nyingi kuliko mchele, tuuchukue tuu huo mchele ndio tuumeze na pumba zake tumuachie haswa kwa kuzingatia wapo pia walaji wengi wa pumba hizo.

Zamani mpunga ukipepetwa punga ziliachwa na kutupwa, siku hizi pumba nazo hutumika, ndio malighafi ya chakula cha viumbe wengine ambao huzitegemea ili nao waishi.

Hivyo hongera Michuzi Blog asante kwa kutupatia mpunga ambao hutusagia, hutupepetea na hatimaye kutulisha mchele wakati mwingine ni mchele safi na wakati mwingine ni mchele na pumba zake. Asante kwa yote!.