Tumsaidie Binti huyu,majeraha yake yanaumiza,yanaliza

Ndagullachrles

Senior Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
153
Reaction score
161
Crala Wilfred Kimath (21)yupo chini ya uangalizi wa madaktari wa mifupa kwenye Hospital ya Rufaa ya kiKanda ya KCMC baada ya kujeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili katika tukio linaloacha maswali mengi kutokana na mazingira ya tukio lenyewe.

Binti huyu ambaye ni yatima baada ya wazazi wake wote kufariki dunia kwa nyakati tofauti mwaka 2019 na mwaka 2020, amepatwa na mkasa huo akiwa mikononi mwa mama yake mlezi, Hyasinta Uisso katika mji mdogo wa Himo, Desemba 5 mwaka jana.

Alianza mama yake Eugenia Julius Massawe kufariki Dunia Agosti Mwaka 2019 na mwezi machi mwaka 2020, Baba yake Wilfred Kimath alifariki dunia na hivyo kuwa mikononi mwa mama huyo ambaye inadaiwa aliomba kwa ndugu zake kumlea kama mwanae.

Kwa mujibu wa ndugu wa Crala na watu wa karibu wanasema kabla ya kufikwa na mkasa huo amekuwa hana amani kutokana na matendo ambayo alikuwa anafanyikwa na mlezi wake ambaye awali alionekana kama mtu sahihi.

Matumaini ya Crala kuwa na maisha mazuri na kuwasaidia wadogo zake wawili baada ya kuhitimu masomo yake ya Utalii kwenye Chuo cha Mafunzo ya Utalii Kilichopo Marangu ,yanaanza kutoweka kutokana na mkasa huo ambao umemfika akiendelea na masomo yake.

"Hapo Hospital anasema mama mdogo nikipona nitamalizia ile nyumba nikae na wadogo zangu, hapo mlipotusadia kwa kweli panatosha",ni maneno ya Crala yaliyonukuliwa na Mama yake mdogo ambaye pamoja na ndugu zake wengine wanapambana kuokoa maisha yake.

Crala ameumizwa vibaya sana na amepoteza uwezo wa kukaa kwani miguu yake haina nguvu, mkono wake wa kushoto umekatwa na kitu chenye ncha kali kiasi cha kufanya uning'inie na madaktari wanapambana kuona hali yake inarudi kawaida lakini kikwazo kikubwa ni gharama za matibabu na familia hiyo inapaza sauti kuomba wasamalia wema wasaidie gharama za matibabu.

Wakati Crala akipigania uhai wake, ndugu zake wameingiwa na hofu juu ya usalama wake kutokana na madai ya kupewa vitisho mara kwa mara kutoka kwa watu wanaodaiwa kuwa upande wa mama mlezi na kutaka vyombo vya uchunguzi na uongozi wa Hospital ya KCMC kuchukua hatua haraka ikiwamo kuwazuia kuingia wodini alikolazwa binti huyo.

"Juzi alikuja baba(mme wa Hyasinta Uisso )akampa simu Crala aongee na Mama huku akimwambia mama anaomba umsamehe wakati mtoto yupo kwenye hali mbaya, sasa huoni wanamuongezea maumivu", analalamika mama yake mdogo.

Kauli hiyo inaungwa mkono na Baba yake mdogo ambaye anadai jambo hilo ni hatari kwa usalama wa mtoto wao na pia itawapa changamoto madaktari wakati wa kumhudumia kutokana na kile kinachodaiwa hofu aliyonayo binti huyo .

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, kamishina Msaidizi Mwandamizi wa jeshi la Polisi(SACP), Simon Maigwa ameomba kulizungumzia tukio hilo kesho jumatatu alipozungumza nami na juhudi za kuupata uongozi wa Hopistal ya KCMC juu ya usalama wa mgonjwa huyo zinaendelea.

tukutane kesho Inshallah
 
Kwa nini kajeruhiwa? Hajapita na baba mlezi kweli? Manake wanawake wa siku hizi wamepagwa, akigundua unatembea na mumewe hafungashi virago kuondoka.....unawekewa mtoto kautaka tu....
 
Hao mama zake wadogo wapumbavu! Unaruhusu vipi mtoto wa ndugu yako akalelewe na mtu baki na wewe upo? Hayo manyanyaso kutoka kwa huyo mama mlezi walikuwa hawayaoni?
 
Crala Wilfred Kimath (21)yupo chini ya uangalizi wa madaktari wa mifupa kwenye Hospital ya Rufaa ya kiKanda ya KCMC baada ya kujeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili katika tukio linaloacha maswali mengi kutokana na mazingira ya tukio lenyewe.

Binti huyu ambaye ni yatima baada ya wazazi wake wote kufariki dunia kwa nyakati tofauti mwaka 2019 na mwaka 2020, amepatwa na mkasa huo akiwa mikononi mwa mama yake mlezi, Hyasinta Uisso katika mji mdogo wa Himo, Desemba 5 mwaka jana.

Alianza mama yake Eugenia Julius Massawe kufariki Dunia Agosti Mwaka 2019 na mwezi machi mwaka 2020, Baba yake Wilfred Kimath alifariki dunia na hivyo kuwa mikononi mwa mama huyo ambaye inadaiwa aliomba kwa ndugu zake kumlea kama mwanae.

Kwa mujibu wa ndugu wa Crala na watu wa karibu wanasema kabla ya kufikwa na mkasa huo amekuwa hana amani kutokana na matendo ambayo alikuwa anafanyikwa na mlezi wake ambaye awali alionekana kama mtu sahihi.

Matumaini ya Crala kuwa na maisha mazuri na kuwasaidia wadogo zake wawili baada ya kuhitimu masomo yake ya Utalii kwenye Chuo cha Mafunzo ya Utalii Kilichopo Marangu ,yanaanza kutoweka kutokana na mkasa huo ambao umemfika akiendelea na masomo yake.

"Hapo Hospital anasema mama mdogo nikipona nitamalizia ile nyumba nikae na wadogo zangu, hapo mlipotusadia kwa kweli panatosha",ni maneno ya Crala yaliyonukuliwa na Mama yake mdogo ambaye pamoja na ndugu zake wengine wanapambana kuokoa maisha yake.

Crala ameumizwa vibaya sana na amepoteza uwezo wa kukaa kwani miguu yake haina nguvu, mkono wake wa kushoto umekatwa na kitu chenye ncha kali kiasi cha kufanya uning'inie na madaktari wanapambana kuona hali yake inarudi kawaida lakini kikwazo kikubwa ni gharama za matibabu na familia hiyo inapaza sauti kuomba wasamalia wema wasaidie gharama za matibabu.

Wakati Crala akipigania uhai wake, ndugu zake wameingiwa na hofu juu ya usalama wake kutokana na madai ya kupewa vitisho mara kwa mara kutoka kwa watu wanaodaiwa kuwa upande wa mama mlezi na kutaka vyombo vya uchunguzi na uongozi wa Hospital ya KCMC kuchukua hatua haraka ikiwamo kuwazuia kuingia wodini alikolazwa binti huyo.

"Juzi alikuja baba(mme wa Hyasinta Uisso )akampa simu Crala aongee na Mama huku akimwambia mama anaomba umsamehe wakati mtoto yupo kwenye hali mbaya, sasa huoni wanamuongezea maumivu", analalamika mama yake mdogo.

Kauli hiyo inaungwa mkono na Baba yake mdogo ambaye anadai jambo hilo ni hatari kwa usalama wa mtoto wao na pia itawapa changamoto madaktari wakati wa kumhudumia kutokana na kile kinachodaiwa hofu aliyonayo binti huyo .

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, kamishina Msaidizi Mwandamizi wa jeshi la Polisi(SACP), Simon Maigwa ameomba kulizungumzia tukio hilo kesho jumatatu alipozungumza nami na juhudi za kuupata uongozi wa Hopistal ya KCMC juu ya usalama wa mgonjwa huyo zinaendelea.

tukutane kesho Inshallah
Ngoja kesho tumsikilize Kamanda Maigwa ili tujuzwe chanzo ni nini?
 
Sasa ni kwanini huyu mama mlezi aliyefanya huo ukatili bado yupo uraiani?
 
Yaani unamsababishia mtu ulemavu na majeraha mwilini, halafu unataka usamehewe! Pumbavu, sheria ifuate mkondo wake.
 
Back
Top Bottom