Jamaa alioa mke kwa ndoa kanisani yapata miaka mitano iliyopita huko kijijini na kuhamia Dar kikazi, wakabahatika mtoto mmoja. mwanamke alianza kubadirika baada ya kufika mjini ugomvi ndani hauishi maelewano hamna kila mwanaume akijaribu kumrekebisha mkewe lakini ikashindikana tena kufikia hatua mwanamke kugombana hata na shemeji zake, wifi pindi wanaposuluhisha.
Wakati mwingine mkewe huyo huchangia na mdogo wake wakike ambaye walikuwa wakiishi wote kumpiga pindi panapokosekana maelewano. Basi mwanaume akaona suluhisho ni kujali mtoto pindi atokapo kibaruani akijua amekula tu suluhisho ni kukimbilia Bar kupoteza machungu.
Siku anatoka kazini, jamaa akakuta mwanamke kabeba kila kitu ndani na mtoto katimka hajui pakumtafutia akagundua baada ya siku tatu yakuwa aliuza vitu akaenda kuishi mkoa mwingine na jamaa mwingine ambaye mpaka hii leo wanaishi wote na kesha mfungulia miradi mbalimbali na gari kamnunulia na wameisha zaa watoto mapacha, lakini mtoto wa jamaa naye wanamlea.
Jamaa akaamua kuondoa upweke akamtolea mahali msichana mwingine na wameshazaa mtoto mmoja lakini alimficha huyo msichana yakuwa hakufunga ndoa ya kanisani ila alizaa tu na kuishi naye yule mke wake, msichana anataka ndoa kwani mahali keshatolewa na wanaishi wote na mtoto pia wamezaa.
Je afanyaje? anaruhusiwa kufunga kanisani? au mpaka Serikalini? anasema mwaka watano toka akimbiwe nayule mke wake,na yule mkewe ndo anaishi na mumewe huyo aliyemkimbilia. NIMELETA KWENU WANAJAMII TUMSAIDIE MSAADA WA KISHERIA AFANYAJE?? Kwani mke aliyenaye anahitaji ndoa.