Tumsaidieje huyu mtoto aweze kupata elimu kama wenzake? Inatia huruma!!!

Tumsaidieje huyu mtoto aweze kupata elimu kama wenzake? Inatia huruma!!!

SENGANITU

Member
Joined
Sep 19, 2012
Posts
50
Reaction score
15
Mtoto wa kiume mwenye miaka 12 (jina limehifadhiwa) mwenye ulemavu wa kutokusikia na kuongea yaani Hearing Impairment na Speech Impairment ameshindwa kuendelea na shule kwa kukosa shule yenye kukidhi mahitaji yake maalum kielimu. Mahali anakopatikana ni Morogoro,Turiani (mtibwa). Mahitaji yake mahsusi kielimu ni pamoja na kupata shule ya bweni yenye kufundisha kwa kutumia lugha ya alama. Kwa ufupi huyu mtoto anaishi na mama yake ambaye aliachwa na mumewe baada ya kugundua kuwa mtoto wao ni mlemavu, na wanaishi maisha ya kimaskini kupita kawaida. Sijatoa jina la mtoto, na namba ya simu yangu ili kuepusha udanganyifu. Yeyote aliye tayari kutoa msaada kwa mtoto huyu nitamwelekeza mahali anapopatikana hasa(kata,kijiji,mtaa pamoja na viongozi wa serikali wa maeneo hayo).Toa msaada wako kwa kadri utakavyosukumwa na nafsi yako!!!
 
Pole sana kwa mtoto na mama yake. Mimi nina msaada wa kimawzo kama ifuatavyo;

1.Weka taarifa za kutosha hapa kuhusiana na huyo,ikiwemo jina lake nk(basic info)
2.Ambatanisha vithibitisho kuonyesha kweli huyo mtoto ni mlemavu,kama vile nakala kutoka hospitalini,picha zake nk.
3.Toeni taaeifa polisi ili baba wa mtoto atafutwe na awajibishe kisheria.
Mkuu weka mambowazi kwasababu sio kila mtu anauwezowa kufika Moro kwenda kumtazama mtoto.Asante.
 
kuna shule moja Tabora ya walemavu, nafikiri itamfaa...ipo Tabora Mjini inaitwa Furaha ni Boarding
 
uhuru mchanganyiko au pale buguruni malapa kuna shule ya viziwi...hizi zote zina hostel
 
hawa watu wa namna hii katika jamii zetu ni wengi sana. Ni jambo la kushukuru wewe umemuona huyo huko Mtibwa, lakini wako wengi wenye mahitajo tofauti-tofauti!

Nakuomba mtoa mada upige hatua moja mbele katika kumsaidia, au mwana jf yeyote si lazima mtoa mada anayefahamu iliko shule ambayo inaweza kumpokea mtoto huyu alete hapa mahitaji ya shule hiyo ili kuweza kumpokea huyo mtoto ili sasa kwa umoja wetu tuje na mikakati ya kuona kwamba anapata haki hiyo ya elimu kwa manufaa ya jamii yetu ya Tanzania.
 
Asanteni wana JF kwa kuonyesha nia ya kumsaidia huyu mtoto. Nawaombeni popote mlipo tafuteni hiyo shule ya kufaa kwake ili baadae tufanye mchanganuo wa mahitaji yake ya shule. Leo nimeanza mimi kuonyesha shida ya huyu mtoto, kesho yawezekana na wewe ukaleta mwingine nasi tukajitoa kwa kadri tuwezavyo.
 
mkuu fanyia kazi ushauri wa Msafiri Kasian ili tuanze kuchangia. mambo mawili yakigongana kati ya mchango wa shule na mchango wa Harusi, kwangu mchango wa shule ndio hushinda.
 
Last edited by a moderator:
ni ya anglican ruaha diocese,boarding,ada ni kama 120k per year plus mahtaji mengne ya msing kwa boarding
 
*Tayari hoja ya Msafiri Kasian naifanyia kazi,ila wazo lake la tatu haliwezekani kwani sisi interest yetu ni mtoto asome na si kumrudisha jamaa kwa mke wake. hata hivyo kwa taarifa za jana ni kwamba huyu baba ameshatangulia mbele ya haki takribani miezi 6 hivi imepita akiwa hukohuko alikokimbilia. Ushauri wenu ni mzuri,kila linalowezekana nalitekeleza.
 
Back
Top Bottom