SENGANITU
Member
- Sep 19, 2012
- 50
- 15
Mtoto wa kiume mwenye miaka 12 (jina limehifadhiwa) mwenye ulemavu wa kutokusikia na kuongea yaani Hearing Impairment na Speech Impairment ameshindwa kuendelea na shule kwa kukosa shule yenye kukidhi mahitaji yake maalum kielimu. Mahali anakopatikana ni Morogoro,Turiani (mtibwa). Mahitaji yake mahsusi kielimu ni pamoja na kupata shule ya bweni yenye kufundisha kwa kutumia lugha ya alama. Kwa ufupi huyu mtoto anaishi na mama yake ambaye aliachwa na mumewe baada ya kugundua kuwa mtoto wao ni mlemavu, na wanaishi maisha ya kimaskini kupita kawaida. Sijatoa jina la mtoto, na namba ya simu yangu ili kuepusha udanganyifu. Yeyote aliye tayari kutoa msaada kwa mtoto huyu nitamwelekeza mahali anapopatikana hasa(kata,kijiji,mtaa pamoja na viongozi wa serikali wa maeneo hayo).Toa msaada wako kwa kadri utakavyosukumwa na nafsi yako!!!