Elections 2010 Tumsamehe mama yetu Sophia Simba

Elections 2010 Tumsamehe mama yetu Sophia Simba

minda

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2009
Posts
1,068
Reaction score
67
Katika makala ya Mungu aliyemchagua Kikwete anaruhusu 'madudu' haya?, kwenye gazeti la raiamwema la hivi karibuni, deusdedit jovin anatueleza kuhusu mafundisho ya Machiavelli; kwamba, katika hali tete, ni ruksa kwa mwanasiasa au kiongozi mwingine yeyote kutumia mbinu chafu kufukuzia lengo safi.


Akatoa baadhi ya mifano inayojumuisha mbinu chafu kwa ajili ya kufukuzia malengo safi kuwa ni pamoja na:


  • kutoa rushwa ili kupandishwa cheo;
  • kuiba pesa za jirani ili kununua gari,
  • mume kumlawiti mkewe ili kutuliza maumivu ya misuli,
  • mwanamume kuzini na mke wa jirani ili kuzaa mtoto,
  • kumfundisha mtoto wizi ili awe na maisha mazuri baadaye na
  • kutoa mimba ili kupata muda wa kufanya maandalizi ya mitihani.



Kwa kutoa mifano halisi ya mafundisho ya huyo mwana-fa kwa mazingira ya tanzania, dj akanza kwa kuandika hivi:


Awali ya yote hapa kuna Sofia Simba (Waziri wa utawala bora na pia Mwenyekiti wa UWT) ambaye alianzisha uhusiano wa kimapenzi na Mzee Kitwana Kondo (boyfriend) ili kuzaa naye mtoto wakati akijua kwamba Mzee Kitwana Kondo ni mume wa mtu, na kwamba kitendo hiki ni kinyume cha sheria ya ndoa inayokataza uzinzi. Lengo ni safi lakini mbinu ni chafu.




Source: gonga hapa


Hata kama huyo mama ni maarufu kwa kutoa kauli zenye kukanganya kimaadili, wakuu mnaonaje akisamehewa bure tu?, kwani naye ni binadamu ambaye ni inclined to sin kama walivyo wengine; isitoshe ni sawa na mama/dada yetu kiumri hivyo maisha yake binafsi aachiwe mwenyewe.
 
..mbona katika kundi la wanasiasa ambao mwandishi anaodai ni wasafi kuna waliozaa nje ya ndoa kama alivyofanya Sofia Simba?

..makala ya mwandishi ni ya hovyo-hovyo kwasababu hakufanya utafiti wa kutosha kuthibitisha madai yake.


.mwandishi makini anayefanya utafiti wa kutosha hawezi kumuweka Samuel Sitta ktk kundi la wanasiasa wasafi wa kupigiwa mfano hata siku moja. Sitta amefanya madudu mengi nchi hii tangu alipokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu CDA, kituo cha uwekezaji TIC, na majuzi kujenga ofisi ya mbunge kutumia mamilioni ya fedha wakati wananchi wake hawana zahanati.
 
Back
Top Bottom