Je wangapi hivi tunavyoongea wamo MAHOSPITALINI?
Je wangapi hivi tunavyoongea Matumbo yao Matupu, na hawajui kitakachoingia Matumboni mwao?
Je wangapi hivi tunavyoongea wamo kwenye Majonzi makubwa sana, na wengine wanafikiria kufanya Maamuzi magumu?
Je wangapi hivi tunavyoongea wamo kwenye Vituo vya Polisi?
Je wangapi hivi tunavyoongea wamo Mahabusu wanasubiri Hukumu zao, tena kwa Makosa ya kusingiziwa?
Je wangapi hivi tunavyoongea wamo Magerezani wanatumikia Vifungo si vyao, yaani vya Kusingiziwa?
Je wangapi hivi tunavyoongea hawakubahatika kuwaona Wazazi wao (japo Mzazi mmoja)?
Je wangapi hivi tunavyoongea wapo kwenye hali ngumu kiasi kwamba hawana uhakika wa Nyumba ya kuishi?
Je wangapi hivi tunavyoongea wametimuliwa kwenye Nyumba walizokuwa wamepanga, kwa kukosa KODI ya Nyumba?
Je wangapi hivi tunavyoongea wamekatiwa Umeme kwa kukosa PESA za kulipia UMEME?
Je wangapi hivi tunavyoongea wamesimamishwa Masomo kwa ajili ya kukosa KARO (ADA) ya kulipia SHULENI?
Je wangapi hivi tunavyoongea AJALI za Vyombo vya Usafiri zimewapata?
Je wangapi hivi tunavyoongea pamoja ya kuwa wana PESA zao, lakini wamelazwa Mahospitalini na wanashindwa hata kupitisha chochote Midomoni mwao, na badala yake Chakula kinapitishwa kwa MIPIRA?
Je wangapi hivi tunavyoongea pamoja ya kuwa wana PESA zao, lakini wamelazwa Mahospitalini na wanashindwa hata kujinyanyua, na matokeo yake HAJA zote wanamaliza hapo hapo KITANDANI?