Tumtengeneze Mwigulu kuwa Rais bora ajae

Kuna mfumo wa kupata wagombea urais hapa nchini. Wakishajulikana ndio kila mtu ampambe mgombea wake. Wa kwangu awe mtu mwenye uwezo wa kututoa katika hii hali ya umaskini, kwa kubadilisha mfumo wa elimu yetu uwe kama wa India au China. Ili ndani ya miaka kadhaa tuwe tunafanya mambo yetu kivyetuvyetu. Mfano tuwe na uwezo wa kutengeneza baiskeli, sahani, vikombe, sindano, nguo nk kwa kutumia rasilimali za hapa nchini!
 
Binafsi simkubali kutokana na tabia za hovyo za sifa na bullying ya watumishi ila kwamba amefanya nini hapo ana Cha kuonesha.

Ni katika nafasi yake kama Waziri wa fedha ambapo uchumi umefanya vizuri sana na ndio kipindi ambacho Serikali imemwaga mabilioni mengi kuliko wakati mwingine wowote.
 
asikwambie mtu, kazi ya mwanasiasa ni kutatua kero za wananchi hata kama kinafiki tu. Kero iliyotatutuliwa haijali kama imetatuliwa kinafiki au kidhati. Mwanasiasa anaangalia sasa, leo na kesho kwa wakati mmoja. Hata Trump anafanya hivyo, Macron anafanya hivyo, Museven anafanya hivyo nk.
 
Wewe mwenye akili timamu umefika wapi? Huyu jamaa ana PhD wewe umesoma hadi wapi? Alishakuwa mfanyakazi wa Benki Kuu, mbunge, waziri wa mambo ya ndani, Katiba, fedha na sasa waziri mkuu katika awamu za Kikwete, Magufuli na sasa Samia. Kama angekuwa mbovu kama Lugola, January, Jaffo, au Nape Mnauye. siangeshapigwa chini?
 
Yeye ni msomi wa PhD, hana maneno mengi kama yale ya akina kasheku Musukuma ambao wanasema sena ili kufidia elimu ndogo yao.
 
Mimi bado nasoma
Pia unaweza kupata PhD na bado usiwe na akili timamu. Mwigulu ni mfano mzuri tu. Hata wanafunzi wa form 4 wapo wengi wanamzidi kwenye uwezo wa kufikiri
 
Yeye ni msomi wa PhD, hana maneno mengi kama yale ya akina kasheku Musukuma ambao wanasema sena ili kufidia elimu ndogo yao.
Ndio majibu ya Kupenda sifa za camera ,dharau na bullying au?

Ndio sifa za nyie wasomi?
 
Makonda aka Bashite kashasema wazi piga uwa garagaza Urais 2030 una muhusu na hakuna wa kumzuia, hayupo.

Ndugu zangu ni hivi bila Katiba mpya tutakuja kutawaliwa na ma taahira.. pole Tanganyika yangu.
 
Kama angekuwa hana kitu JPM angeshamtimua kama alivyofanya kwa Kange Lugola. Haya makusanyo serikali ya JPM na Samia inayotamba nayo yameletwa na Mwigulu.
Unatamba na makussnyo Kisha unajadili MATUNDU ya vyoo shileni. Seriously unajua unachojadili hapa
 
Ukishakuwa waziri mkuu possibility ya kuwa rais ni ndogo, aliweza mwalimu Nyerere. Kama Salim Ahmed Salim alikosa, itachukua miaka mingi huko mbele kuja kupata rais aliyekuwa PM.
 
Makusanyo ni makubwa, wasingetuingiza kwenye nchi zenye uchumi wa kati. Tusingeweza kujenga barabara, reli, meli, mashule, mahospitali, mabwawa ya umeme, na kuhamia Dodoma kama hatuna pesa kabisa. Mbona nchi nyingine hakuna vitu hivi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…