SoC04 Tumtue mama wa kitanzania madeni kwa ustawi bora wa taifa

SoC04 Tumtue mama wa kitanzania madeni kwa ustawi bora wa taifa

Tanzania Tuitakayo competition threads

Naaal

New Member
Joined
Apr 23, 2024
Posts
2
Reaction score
0
Hivi karibuni,tumeshuhudia wingi wa ofisi ndongo ndogo za mikopo katika nchi Yetu,mikopo iliyopewa majina tofauti tofauti,lakini ikiwa inasadifu ugumu wa mikopo iyo katika urejeshwaji wake. Hapa ninazungumzia taasisi za mikopo ambayo haijasajiliwa na BOT(Bank of Tanzania).

Mkopo ni mzuri lakini inapogeuka deni basi hugeuka kuwa adha.Wanawake wenye kipato kidogo na wajasiriamali wadogo huchukua mikopo hii kwa ajili ya kuanzisha biashara ama kuziendeleza biashara zao ndogo ndogo Ili waweze kusapoti familia zao,kulipa ada n.k.

Mikopo hii hugeuka kuwa adhabu kwa muhusika pale anaposhindwa kurejesha.

waadhirika wakubwa wakiwa ni wanawake kama tunavyoshuhudia kwenye jamii zetu.

pale mama anaposhindwa kuirejesha basi hudhalilishwa, lakini pia usishangae kuingia kwenye familia ukakuta watoto wanalala chini, kumbe godoro limechukuliwa na kausha damu. Mbali na hayo kuna athari nyingi mno anazopata mama ikiwemo; Msongo wa mawazo, ndoa kuvunjika, malezi duni ya watoto na watoto kutelekezwa,umasikini kwenye familia na hata wengine kujiua.Haya yanatokana na namna yao ya kudai,kwani wanadai kwa kudhalilisha,kwa mfano kubandika bango nje ya nyumba,ama kuchukua vitu vya mkopaji.

Haya yanatokea kwa sababu mara nyingi hizi taasisi uchwara zinakuwa na riba kubwa sana, lakini pia uelewa mdogo kuhusu mikopo na elimu ya fedha kwa jamii,swala lingine ni taasisi kutofuatilia kuhusu uwezo wa mteja kabla hajapewa mkopo,urahisi wa upatikanaji wa hii mikopo,ipo kila mahali hivyo ni rahisi hata mtu kushawishika.
Mikopo umiza Mingi inatolewa pale mteja anapokuwa na barua ya mwenyekiti na kuweka zamana vitu vya ndani.


kwa lugha rahisi tunaweza kusema taasisi hizi zinafanya kazi bila kuzingatia sheria na utaratibu wa utoaji mikopo zinajiendesha kiholela holela.

NAMNA YA KUTATUA CHANGAMOTO HII.

-Serikali kupitia BOT(bank of Tanzania)iache kutoa leseni kiholela holela ama zifungie hizi taasisi .Na zile zitakazokidhi vigezo ndizo zipewe kibali.Hizi ofisi ni nyingi mno,bila kupaza sauti tutaendelelea kushuhudia watoto ambao ndio tegemeo la kesho wakitelekezwa na kukosa malezi bora.

-Taasisi zote za mikopo zisajiliwe na zifuatiliwe na kuwe na sheria ya kumlinda mkopaji kipaumbele akiwa ni mwanamke.

- Mikopo inayotolewa halmashauri ilenge kumuinua mjasiriamali mdogo ikimlenga mwanamke,na iwekwe mikakati mizuri yenye lengo la kuwafikia akina mama wengi zaidi kutokea sasa mpaka miaka 25 ijayo,ikusudiwe kutolewa kwenye vikundi vya akina mama wasiozidi watano(5).Ikiwalenga akina mama wajasiriamali,waliojikita kwenye dunia ya technologia pamoja na wajasiriamali wadogo wasiokopesheka benk.

- Taasisi za serikali na zisizo za kiserikali pamoja na vyombo vya habari ziwekeze kwenye utoaji wa elimu ya fedha pamoja na ujasiriamali.
Kuwe na mabango yanayoelezea faida na hasara za mikopo.

- Elimu ya fedha na ujasiriamali iwekwe kwenye mtaala wa elimu.
Kuanzia ngazi ya sekondari.

- Elimu ya ujasiriamali wa mtandao(digital entrepreneurship)ifundishwe kwenye majukwaa mbalimbali tena iwe bure,ikiwalenga akina mama,Ili kuwawezesha kupanua wigo wa biashara zao lakini pia na kuendana na mabadiliko ya technologia.

Mama ni mlezi,Mama ni mlinzi wa familia,Mama anajukumu kubwa la kuandaa taifa la kesho.Hivyo basi kama
SERIKALI IMEFANIKIWA KUMTUA MAMA NDOO KICHWANI.
IMTUE MADENI KWA USTAWI BORA WA JAMII.
Hii ndiyo Tanzania tuitakayo.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom