Tumuache Maxence Melo na JamiiForums yake afanye kazi yake

Tumuache Maxence Melo na JamiiForums yake afanye kazi yake

Kidagaa kimemwozea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
3,680
Reaction score
6,554
Hujambo mdau na msomaji wangu, Leo imenipendeza kulijadili hili swala, wewe mwenyewe utakuwa ni shahidi kwa namana, watu mbalimbali hasa vijana wanapo chakata akili zao na kuja na jambo la kimaendeleo namna wanavyo kumbana na changamoto mbalimbali zinazotokana na fikra hasi miongoni mwa pengine viongozi wetu au watu wengine kuyahusisha maendeleo hayo na siasa zao.

JamiiForums ni jambo la kujivunia sio tu kwa ndugu Maxence na Mike bali ni maendleo ya watanzania kwa ujumla. Aidha mtandao huu ndio unao ongoza duniani kwa kuwa na machapisho mengi au maudhui yaliyo chapishwa kwa lugha ya kiswahili, au kwa maelezo rahisi naweza kusema hakuna sehemu palipo andikwa kwa kiswahili duniani kitehama kama mtandao Wa Jamii forum, hivyo mtandao huu ni nguzo muhimu katika ukuzaji wa kiswahili kimaandishi , BAKITA mnalifahamu hili?

Aidha huu ndio mtandao wa kienyeji (wakwetu) unao ruhusu watumiaji wake kujadili mambo yanayotuhusu, ukiachana na mtandao mingine ya kijamii ya nje kama Facebook na mingineyo, Kutokana mtandao huu kutoa kipengele cha watumiaji wake kuweza kujadili mambo yanayotuhusu ni jambo zuri ambalo linaweza kuchangia maendeleo ya nchi yetu.

HALI ILIVYO MBAYA
Mtu anapofanya jambo zuri Jamii haina budi kumpongeza, lakini hali imekuwa ni tofauti kwa wamiliki wa mtandao huu! Badala ya kupata pongezi na kuthaminiwa mchango wao katika TEHAMA wamekuwa kama ni maadui, kuburuzwa mahakamani kila wakati na kuishia kupata tuzo za kimataifa peke yake na kuandikwa vibaya katika magazeti. Je nikweli Watanzania hatuoni mchango wa Jamii forum badala yake tunataona madhaifu yake tuu?

Maxence amekuwa akipokea tuzo mbalimbali za kimataifa na kupokea mialiko ya kimataifa kuliko hata hali ilivyo hapa nyumbani. Wahenga waliwahi kusema nabii hakubaliki nyumbani, lakini sidhani kama usemi huu ungali unanafasi, ifike pahala tuwathamini wakina maxence walioko katika Jamii zetu

Tuwathamini watu wanaoipaisha nchi yetu kimataifa, tutambue mchango wao tuache kuwasumbua, na kuwakatisha tamaa ili ifike siku kila mtanzania ajivunie maendeleo ya nchi yetu Kiteknolojia.

Tukutane wasaa mwingine
info.masshele@gmail.com
 
Ni kweli kabisa yaani JF ingeshafungwa zamani kabisa na wengine kukamatwa hovyo
 
Maxence amekuwa akipokea tuzo mbalimbali za kimataifa na kupokea mialiko ya kimataifa kuliko hata hali ilivyo hapa nyumbani. Wahenga waliwahi kusema nabii hakubaliki nyumbani, ifike pahala tuwathamini wakina maxence walioko katika Jamii zetu

Tuwathamini watu wanaoipaisha nchi yetu kimataifa, tutambue mchango wao tuache kuwasumbua, na kuwakatisha tamaa ili ifike siku kila mtanzania ajivunie maendeleo ya nchi yetu Kiteknolojia.

Tukutane wasaa mwingine
info.masshele@gmail.com
Naunga mkono hoja
P
 
Back
Top Bottom