Tumuhamishe Wizara Dkt. Ndugulile kwa sababu hakuna innovation yoyote anayoifanya

Tumuhamishe Wizara Dkt. Ndugulile kwa sababu hakuna innovation yoyote anayoifanya

Joined
Oct 13, 2018
Posts
35
Reaction score
260
Na Thadei Ole Mushi

Serikali inaandaa sheria maalumu ya mtu kuwa na laini moja ya simu kutoka kampuni moja ikiwa ni njia ya kulinda faraga za watu inayolenga kudhibiti wahalifu mtandaoni.

Bado naona Kuna tatizo kwa Wizara yetu ya Technolojia ambayo ni Wizara Mpya kabisa.

Tatizo kubwa hawa wajamaa wamejikita kwenye kudhibiti badala ya kuwekeza kwenye uvumbuzi. Dunia kiteknolojia inakimbia Sana sisi bado tunahangaika na wanaomiliki line mbili za Simu.

Twende sawa hapa

Tuna tatizo mahali na tatizo hili linanzia kichwani kwa Mh Ndugulile. Kwa sasa laini zote za Simu zimesajiliwa kwa Kutumia alama za vidole (Biometric) kwa maana hiyo Mimi Ole Mushi hata nikiwa na Line mia Moja za Simu as long as nimezisajili kwa Kutumia fingerprint na kitambulisho changu nikifanya uhalifu popote ni rahisi kunikamata.

Au tuseme lile zoezi lilikuwa ni danganya toto? Kwamba pamoja na kusajili kwa alama za vidole bado hatujui ni kina nani wanaomiliki hizo line?.

Hivi wizi wa Mitandao anaujua Ndugulile?

Hawa wanaotuma sms kuwa nitumie hela kiasi Fulani au wanakupigia simu sio wezi wa Mitandao hawa ni vibaka wadogo Sana .

Wizi wa Mitandao kwa mfano hapa Tanzania tunafanya Transaction nyingi Sana online fikiria kuhusu kununua Luku, Kutuma Pesa kwenye Mitandao ya Simu nk. Ukisikia wizi wa Mtandao ni Mtu anazuia mifumo hiyo isifanye Kazi mfano Mtu anaweza kuhack mfumo wa Kutuma Fedha Tigo. Anazuia hakuna Fedha kwenda Wala kutoa. Halafu wanawapigia Tigo kuwa tupe bilioni kadhaa tuachie mfumo wako ufanye Kazi.

Ni kama walivyokuwa wasomali wanateka Meli wanakuambia tutumie Fedha tuachie Meli yako na huna Cha kuwafanya.

Sijui Mifumo yetu ya Transaction ipo secured kiasi Gani au tunazo server au tunategemea server za nje ya nchi lakini watu Duniani wanapigwa Sana kwenye uharamia huu.

Ninaposema ipo secured kiasi Gani ni kama unamtuma Mtu apeleke hela anaondoka Nazo Kinondoni anapeleka Tegeta hapo njiani Kuna maharamia wengi Sana je tunazilindaje zifikie? Ni vivyo hivyo online tunapofanya Transaction Kuna watu wanaweza ku generate code na wakazizuia au kuchukua na hutawajua.

Mh Ndugulile yeye anawaza line za Simu tu wakati Dunia ilishahama huko. Na akumbuke watu kumiliki lain zaidi ya Moja sio kwa kupenda ni kujaribu kutafuta unafuu wa maisha.

Naona Umuhimu wa Ndugulile kurudi kwenye masuala ya Afya akatusaidie kunyoosha mifupa iliyovunjika kuliko huku Aliko.

Hakuna innovation yoyote anayoifanya hapa.

Ole Mushi
0712702602

FB_IMG_1623221666236.jpg
 
Well said, huyu mzee arudishwe afya maana alifit sana huku hapawezi, huku apewe January Makamba
 
Tatizo ni Siasa zina haribu mambo.

Wazo la kuwaondoa vijana wanaosajili mitaani na kuweka maduka au vibanda maalum kisheria kwa ajili ya kusajili line ndo ilikua suluhisho ya utapel.

Kwa sababu vijana ndo wanawajilisha watu line mbilimbili bila wao kujua na kuziuza kwa watu wasio na Nida ikiwemo ao matapel. Lakin wanasiasa wakapiga kelele za apa na pale wakabitilisha lile zoezi.

Lakin swala la kusajili line moja kwa kila mtandao ni kuturudisha nyuma.
 
Hii Picha alikuwa anataka tuone Para lake au Suti yake au hasa hasa hiyo Saa yake ambayo inaonekana ni ya Thamani kutoka katika ' Brand ' Kubwa huko Ulaya / Mamtoni?
 
Hii nchi ina viongozi vilaza sana, badala ashughurikie masuala ya kuruhusu malipo ya mtandaoni kama PayPal nk. Ili kufungulia vijana wa kitanzania fursa za kufanya kazi online yeye yuko busy kupambana na line za simu.
 
Huyu nae amewekwa sehemu siyo yake....Mama amtoe haraka kuna vijana wengi kwa post ile yeye hataiweza
 
Na Thadei Ole Mushi.

Serikali inaandaa sheria maalumu ya mtu kuwa na laini moja ya simu kutoka kampuni moja ikiwa ni njia ya kulinda faraga za watu inayolenga kudhibiti wahalifu mtandaoni...
Jana nilikuwa natafuta solution ya simu Lumia 640 (airplane mode solution) nikakuta Do you need a help for your cellphone replied yes ,question what OS is the version of your phone, replied. Answer you have to pay nonrefundable $5 nikachomoa
 
Well said, huyu mzee arudishwe afya maana alifit sn huku hapawezi, huku apewe January Makamba
Cyber crime si alileta muswada na kupitisha, labda walete tena kwa ajili ya Tallying center ya kubadilisha na kuibia kura
 
Hapo alipowekwa ni kumuonea. Dr. Ndugulile ana-fit zaidi wizara ya afya kuliko yule naibu.
 
Huwez kuweka waziri, naibu waziri na katibu wa wizara ambao sio wataalam wa ICt wakaanzishe wizara ya ICT, hapa hakuna miujiza ni madudu tu ndo yatakayotokea huko.
 
Hauko sahihi kwani wizara yake ya C&IT ni mtambuka ikigusa sana masuala ya afya ingawa wachangiaji wengi humu wanazingatia zaidi uhalifu mtandaoni hasa katika miamala ya kifedha. Tuzingatie kuwa wizara ya C&IT kwa wakati huu wa mapinduzi ya nne ya viwanda ndiyo muhimili wa sekta zingine ikiwa ni pamoja na afya,elimu,biashara,viwanda,kilimo,ufugaji,ujenzi ,uchukuzi n.K.
 
Back
Top Bottom