Tumulike ufisadi: Magufuli tarehe 29/11/2015 alisema pesa za sherehe za uhuru za December 2015 zikapanue barabara ya Morocco

Fikira za watanzania za ajabu..hizo billion nne zilipanua kutoka two lane wakaweka 3 lane..hzi zilizokuja zimeongeza upana na urefu na mitaro nk
Sijui kwa nini hawa wahuni wanataka kudanganya. Yaani wanatunga uongo. Watuambie ile Hospital ya Uhuru Dodoma hela zilitoka wapi??? Yaani hawa mafisadi acha waenjoy kidogo kikija chuma kingine ni wa kuwekwa pembeni tu ili nchi ibaki na wazalendo wenye nia ya dhati kwa maendeleo ya Tanzania ya sasa na vizazi.
 
Wao wanahisi hizo hela Magufuli kala! Hata kama hazikwenda hapo Morrocco ila lazima kuna jambo la maana alifanyia
Hata ufisadi kwa Ccm ni jambo la maana. Kama mnaweza kuiba kura nchi nzima!! B 4 ni kitu gani kwenu??
 
Kweli kabisa.
 
Wananchi wanataka maelezo na uwazi katika kutekeleza miradi ya maendeleo na siyo longo longo!

Sasa serikali inashindwa vipi kutoa ufafanuzi?
Hili ndilo tatizo kubwa la awamu ya tano. Kukosekana uwazi na uhuru wa kutoa taarifa fasaha za shughuli za umma kumeacha uvumi (speculations) wa kila aina kuhusu matumizi ya pesa na ufisadi.

Vyanzo vya pesa na matumizi yake hasa kwenye miradi mikubwa ya ujenzi na ununuzi wa mitambo ni siri kuu (top secret) ya serikali. Wananchi wanatakiwa kuishi kwa imani tu! Asili ya binadamu haiko hivyo. Leo hata maaskofu wanahojiwa kwa tuhuma za ufisadi.
 
Fikira za watanzania za ajabu..hizo billion nne zilipanua kutoka two lane wakaweka 3 lane..hzi zilizokuja zimeongeza upana na urefu na mitaro nk
Hii biashara ya nk hii 🤔🤔 watu wanataka reality in open qoutations na sio maneno! Uwaz na uwajibikaj ni muhimu sana kuliko majibu ya maneno matupu.
 
Ila yy aliruhusiwa kutukana wenzake iblis atabaki kuwa iblisi tu
 
U geuliza kwanza tunatumia kiasi gani kwa sherehe za uhuru mwaka huu?midege inaruka huko angani na shughuli yenyewe ni ya si zaidi ya masaa 4....
 
Ili kurekebisha hilo tuanze na uwazi kabla ya ujenzi wa bagamoyo haujaanza maana mnasema mama ni msikivu! Aweke mzigo live uchambuliwe kabla hawajaupitisha😅
 
Njaa mbaya sana,mnalipwa ngapi ndio mjitafutie laana?Magufuli hachafuki na anaendelea kupata umaarufu.
Magufuli ndiye Rais fisadi bora wa muda wote kwani haijawahi kutokea tokea uhuru Rais akapiga ufisadi wa TZS 1.5 trilioni ndani ya awamu moja ya uongozi.

Ufisadi aliopiga Magufuli ni mkubwa kuliko ufisadi wote wa awamu zote nne za nyuma yake ukijumlisha kwa pamoja.

Sifa na utukufu zimwendee CAG Profesa assad ambae alifanya kazi nzuri sana ya kuibua ufisadi ule.
 
Hiyo barabara kilichofanyika sana ni sewage system mpya ambayo mwanzoni haikuwepo
 
baadae Serikali ya Japan ikaleta fedha lakini nadhani kwakuwa zilikuwa zimeshapangwa na kupigiwa mahesabu kutumika barabara ya Morocco ikabidi zizame tena hapohapo..
Kwa hiyo TZS 71.85 billion imejenga barabara yenye urefu wa 4.3KM?

Unaelewa gharama ya kutengeneza barabara kilomita moja kwa kiwango cha lami kwa makadirio ni TZS ngapi?
 
Chuki mbaya sana tena kwa unaa mtu akaongeza na takwimu za uongo ilimradi tu mwamba aonekana mbaya....mtaumwa uharo huu mwaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…