Tumulike ufisadi: Magufuli tarehe 29/11/2015 alisema pesa za sherehe za uhuru za December 2015 zikapanue barabara ya Morocco

Mkuu ungekuwa mkazi wa Maeneo husika wala usingehangaika kuandika utumbo huu.. Hizo pesa za Magufuli zilitumika ndani ya hiyo barabara kandarasi mmoja hivi mhindi mpuuzi kabisa kama alivyo mpuuzi mwingine anayejenga barabara ya mwendokasi ya mbagala/Keko n.k ile barabara ilikuwa na changamoto kipindi kile mashimo mashimo na wembamba wake foleni hatari na uhakika pesa zilitumika zikarekebisha ubovu ule na japo kulikuwa na mpango wa wajapani wa kujenga hiyo barabara ila ilikuwa hamna namna kuiweka at least ipitike vizuri so usilamu kipindi hiki wakati muda ushapita...

Tukienda hivi tuwalaumu basi na kajima waliokuwa wakijenga barabara ile ya morogoro road hadi pale jangwani ambao ndio walikuja kuweka njia nne maana ilikuja tena kujengwa na strabag kama tunakuwa wajinga tusioendana na muda husika wa matukio.... Mwishowe mtakuja sema hadi wale wa kwenye vitabu vya Dini waliokuwa wakipigana kwa Mapanga mtasema wajinga na kwanini hawakutumia Bunduki! ndio akili za Watanzania wengi ni wapumbavu kama wewe... Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni.
 
Hujajibu maswali ya msingi.Je,ni sawa TZS 71.85 billion kutumika katika kujenga barabara yenye urefu wa 4.3KM?

Unaelewa gharama ya kutengeneza barabara kilomita moja kwa kiwango cha lami kwa makadirio ni TZS ngapi?
 
Kwenye Hili Hapana Ukweli Usemwe, Hii Barabara imejengwa kwa Awamu mbili Sasa Awamu ya Kwanza kwa Fedha za Uhuru zilitumika kufanya upanuzi na kuongeza Njia hadi kufikia 5 na Awamu ya Pili kwa Fedha za Wajapan ndio ilitumika kutengeneza Njia 4, utanuzi na kuacha Space kwa Njia ya Mwendokasi kwa hapo Baadae. Tunaweza kumkosoa kwa yale yaliyo ya Kweli na Wazi, tusipotoshe.
 
Tukisema CCM ni majambazi muwe mnaelewa. Mikataba ya ujenzi yote kipindi cha magu ilikua inapambwa kwa mwembwe na sherehe nyingi. Hii ya mwenge-moroco naona mkataba ulisainiwa kimya kimya kwa kuwa tulishapigwa changa kuwa barabara inajengwa kwa pesa ya sherehe za uhuru.

Hatimaye sasa imefahamika kuwa si fedha za sherehe bali ni msaada wa mabeberu. Sasa wazee wa dona kantri sasa hivi wanajificha kwenye shamba la karanga.
 
Tukisema CCM ni majambazi muwe mnaelewa. Mikataba ya ujenzi yote kipindi cha magu ilikua inapambwa kwa mwembwe na sherehe nyingi. Hii ya mwenge-moroco naona mkataba ulisainiwa kimya kimya kwa kuwa tulishapigwa changa kuwa barabara inajengwa kwa pesa ya sherehe za uhuru.

Hatimaye sasa imefahamika kuwa si fedha za sherehe bali ni msaada wa mabeberu. Sasa wazee wa dona kantri sasa hivi wanajificha kwenye shamba la karanga
 
Fikira za watanzania za ajabu..hizo billion nne zilipanua kutoka two lane wakaweka 3 lane..hzi zilizokuja zimeongeza upana na urefu na mitaro nk
Wait a minute... unasema??
 
Tatizo ni Watanzania. Kitu hawajui ni kuwa mfumo (wa ccm) uliotufikisha kwenye hizi changamoto tulizonazo leo hauwezi kuwa mfumo sahihi wa kutuvusha!!
 
Labda kama hujui.
Cc tunatumia cash bajet.
Unakusanya kwanza halafu unatumia. Unapoambiwa serikali imetenga 39 trillion kama bajeti sio kwamba hizo pesa zipo pale BOT.alichokuwa anakifanya magufuli ni kuhalalisha ufisadi tu kwakuwa hizo pesa zikipangiwa huku lazima kwanza niende wizara husika na zikifika znaingizwa kwenye accounts za huko ndo zije huku sasa mzunguuko wote huu ni rahisi sana kuiba.
Note: kila wizara ina mafungu yake
 
Uza ubongo huo kaka. Bilioni nne zinaweza kujenga barabara ya urefu gani? Uongo una mwisho wake.
kira za watanzania za ajabu..hizo billion nne zilipanua kutoka two lane wakaweka 3 lane..hzi zilizokuja zimeongeza upana na urefu na mitaro nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…