Tumuombee Rais au tumhurumie?

Si walisema upinzani ndio uliokuwa unawakwamisha imekuaje tena!!
 
Ndugu,umeandika mengi sana,na ya msingi,lakini jambo la msingi zaidi ni kutengeneza mfumo. Kuwa na jeshi la mtu mmoja hakusaidii utendaji makini na wa haraka wa kutatua changamoto zilizopo toka juu mpaka mashinani huko chini.
Uteuzi kufanywa kwa vigezo vya ukada au "mtoto wa nyumbani" badala ya sifa stahili kunafanya wateuliwa kutenda kisiasa zaidi wakiamini kuwa teuzi zao ni za kisiasa zaidi.
Kama tuna kiongozi mkuu anayeteua msaidizi wake bila kujiridhisha "vetting", je tuna sababu ya kuendelea kuamini kuwa matatizo ni ya hawa watendaji tu na si mfumo!!??
 
Hata uombe vipi lakini nchi bila ya kuwa na sensa ya watu ni bure.
 
Huyo si wakuombewa wala kuhurumiwa bali ni wakulaani kwa nguvu zote maana Katiba imempa fursa ya kuteua watendaji anaowaamini toka kati ya Watanzania milioni 60 lakini yeye anateua wasiyo na uwezo wala ujuzi kwa kuwa tu ni homeboys au maswaiba. Wateule wake wanajua udhaifu wake na kwamba ni yeye tu ndo anaweza kutengua teuzi zake kwa hiyo kazi zao ni kungoja na kufikisha maagizo yake kwa wa chini yao ambao nao wanayapuuza. Awamu hii kila kiongozi kazi yake ni kufikisha maagizo toka juu!
 
Wewe jiandae kumsindikiza babako kwa pirato wa dunia..!!
 
Hili la uteuzi kwamba sijui mtoto wa dada au laa, nadhani na lenyewe nalo ni jambo tunalo kariri tu; mifano niliotoa hapo juu, regardless ni mtoto wa nani but wanazo elimu, wengine ni Phd holders kabisa, kwani GM wa NSSFna PPF wana vyeti gani? Achilia mbali uhusiano wao na aliyewateua, ma DED na ma RAS wa wilaya na mikoa wengi wao si ndio wana vyeti hivyo hivyo vikubwa vikubwa? NI kweli tunalo tatizo la kimfumo but hatuwezi kukwepa kwamba tunalo tatizo kubwa sana la kusbiri maelekezo kwa kila kitu; hivi NSSF na PPF kua na account kwenye bank ambayo wao wenyewe wanazo share na lenyewe linatakiwa somebody from above aseme? Tanesco kununua transofromer kwenye kiwanda ambacho wao wenyewe wana miliki hadi mkubwa aseme? Tusihamishe goli, elimu kwa watendaji wengi haijawasaidia sana kufanya maamuzi, inasaidia tu kuadhibu na kukosoa wengine, period.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…