Tumuombee sana Musiba asidhurike kwa namna yoyote ile

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Kama ulikuwa humjui msiba ni nani utamjua sasa
Kama ulikuwa humfahamu tafadhali mfahamu sasa
Kama ulikuwa unambeza na kumdharau badili mtazamo wako huo sasa... Kwakuwa moja lililo dhahiri ni hili.... Musiba ana nguvu, ana kinga na ana backup.... Cheza naye mbali...
Kwa mara ya kwanza na kwa kasi ya supersonic jeshi letu la polisi limefanyia kazi taarifa za mitandaoni/ vyombo vya habari
Vyombo fulani ya habari, vinavyomilikiwa na bwana huyo... Vimeandika habari kwenye kurasa za mbele kwa maandishi makubwa meusi vikiwatuhumu watu kadhaa kutaka kumdhuru Musiba... Wahuhumiwa wote na sehemu wanatoka wametajwa moja kwa moja na wanajulikana kabisa
Chini ya masaa sita tangu magazeti hayo kuandika habari husika... Jeshi la polisi limeshachukua hatua ya kuanza kuwahoji watuhumiwa... Hii haijawahi kutokea...
La kushangaza ulimwengu ni hili.... JESHI LA POLISI LIMEANZA UCHUNGUZI KWA KUHOJI WATUMWA BILA YA MTUHUMU KUFUNGUA KESI

Tumuombee huyu bwana afya njema maana siku akijikwaa hata kidole tutapata tabu sana... Nasema tutapata tabu sana na si ajabu tukapewa kipigo cha mbwamwizi
Kukichwa kutapambazuka... Lakini kabla ya jua kuchomoza kiza huwa totoro...

Good morning Afrika...!!!
 
 
Amerithi/amerithishwa mikoba ya mkuu wa mkuoa mmoja na mkuu wa wilaya waliokua wanachafua hali ya hawa kwa sababu za ama kusahaulisha watanzania tukio Fulani au kuhamisha makini za watanzania kutoka kujadili suala Fulani na kujadili jingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…