Kama ulikuwa humjui msiba ni nani utamjua sasa
Kama ulikuwa humfahamu tafadhali mfahamu sasa
Kama ulikuwa unambeza na kumdharau badili mtazamo wako huo sasa... Kwakuwa moja lililo dhahiri ni hili.... Musiba ana nguvu, ana kinga na ana backup.... Cheza naye mbali...
Kwa mara ya kwanza na kwa kasi ya supersonic jeshi letu la polisi limefanyia kazi taarifa za mitandaoni/ vyombo vya habari
Vyombo fulani ya habari, vinavyomilikiwa na bwana huyo... Vimeandika habari kwenye kurasa za mbele kwa maandishi makubwa meusi vikiwatuhumu watu kadhaa kutaka kumdhuru Musiba... Wahuhumiwa wote na sehemu wanatoka wametajwa moja kwa moja na wanajulikana kabisa
Chini ya masaa sita tangu magazeti hayo kuandika habari husika... Jeshi la polisi limeshachukua hatua ya kuanza kuwahoji watuhumiwa... Hii haijawahi kutokea...
La kushangaza ulimwengu ni hili.... JESHI LA POLISI LIMEANZA UCHUNGUZI KWA KUHOJI WATUMWA BILA YA MTUHUMU KUFUNGUA KESI
Tumuombee huyu bwana afya njema maana siku akijikwaa hata kidole tutapata tabu sana... Nasema tutapata tabu sana na si ajabu tukapewa kipigo cha mbwamwizi
Kukichwa kutapambazuka... Lakini kabla ya jua kuchomoza kiza huwa totoro...
Good morning Afrika...!!!