Tuna imani na Mkwasa, apewe mkataba wa kueleweka

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Watanzania walio wengi wamejionea jinsi Timu ya Taifa ya soka (Taifa Stars) ilivyoimarika. Inatofautiana kiuchezaji na hata ari ya wachezaji na zile za makocha wa kigeni zilizotangulia. Taifa Stars ya sasa inasakata kandanda la uhakika. Haya ni matunda yaliyoanza kuonekana ya Kocha Mkuu mzawa wa Taifa Stars, Charles B. Mkwasa aka Master. Ni Mkwasa na benchi lake la ufundi ndilo lililoifikisha hapo ilipo Taifa Stars.

Imeripotiwa kuwa Kocha Mkwasa ana kibarua tu katika timu ya Taifa. Mkwasa anamaliza kibarua chake mwezi huu na anapaswa kuachia ngazi. Watanzania walio wengi wana imanina Mkwasa. Wanatamani Mkwasa apewe mkataba wa kueleweka wa kukinoa kikosi cha Taifa Stars ili kuonyesha uwezo wa wazawa katika kufundisha soka. Mkwasa aweza kuwa Joel Bendera wa 1980 aliyesaidia Stars kucheza Michuano ya Afrika.

Inasikitisha kuona kuwa makocha wa kigeni husainishwa mikataba minono na kwa haraka halafu Mkwasa anapewa kibarua tu cha kukinoa kikosi cha Stars. Ifike mahali, Serikali na TFF watambue na kuthamini uwezo na mchango wa makocha wazawa. Umefika wakati wa kuwapa akina Mkwasa mikataba ya kueleweka ili kukinoa kikosi cha Stars kwa utulivu na maarifa yao yote. Pia wanahitaji muda wa kukiandaa kikosi na hawafai wajaribiwe kwa mechi chache.

Watanzania wameweka silaha zao chini, wako na Taifa Stars. Wakati huu ambapo watanzania wanarudisha imani na mapenzi yao kwa Stars si wakati wa kuuchezea. Watanzania wana imani na Mkwasa na benchi lake zima la ufundi. Wapewe stahiki zao za mikataba ili kulitumikia Taifa kwa njia ya kufundisha soka la nchi hii. Makocha wa kigeni hawana lolote jipya. Hata wetu wanaweza, Mkwasa na wenzake!
 
Mbona kama hii Topic imepotea jukwaa?kumbukeni ili nijukwaa la siasa mkuu
 
Akipewa mkataba mrefu atabweteka
ivo ivo kidogo kidogo yatosha, akivurunda anasepeshwa fasta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…