Tuna Rais asiyepuuza ripoti ya CAG. Hongera Rais Samia

Tuna Rais asiyepuuza ripoti ya CAG. Hongera Rais Samia

Joined
Sep 17, 2021
Posts
39
Reaction score
84
Nimemkumbuka Mzee wetu Prof Assad. Nimekumbuka alivyoondolewa madarakani kwa mabavu, nimekumbuka ile IST yake siku anaondoka ofisini.

Nimekumbuka pia kwamba RIPOTI YA CAG ilikuwa inaogopwa na Serikali na kupingwa vikali. Nimekumbuka wapinzani kuishi kama digidigi pale wanapojaribu kujadili yale yanayoibuliwa na CAG.

Sijasahau kuhusu taarifa za kupikwa, siajasahau kiini macho cha ATCL kupata faida na Mashirika kusema wanapelka gawio ilihali wao wanagugumia ndanindani.

Leo nimemuona Rais asiyepuuza RIPOTI YA CAG. Nimemsikia akikubali madudu, nimemsikia akikiri Bima ya afya kuwa na matatizo lakini amesema atayapatia mwarobaini.

Nimemskia Rais akisema Wabunge wkajadili hii Ripoti na kuchukua hatua, nimesikia akisema hoja zinazofaa kujibiwa zijibiwe hadharani.

Ni Rais Samia Suluhu. Huyu Mama jamani Mungu amjaalie sana.
 
Mama anaupiga mwingi. Awamu ya 5 ilikuwa ya kifedhuli. Watanzania hatutakubali kamwe kutawaliwa na watu jamii ya Sukuma Gang wasio na ubinadamu wala utu.

Kama kuna Sukuma Gang anataka uongozi aende akagombee kwa tiketi ya CHADEMA kwasababu huko ndo kuna upungufu.
 
Mi naliona tatizo ni la kimfumo zaidi

Serikali utendaji kazi wake ni kama Mpira wa miguu wenye kocha na formula mbalimbali na kucheza juu

Ukweli ni kuwa kocha ndio anachezesha kwa kufuata mfumo waliofundishwa wachezaji na kocha

Sasa sio kocha wala mfumo wala wachezaji waaopaswa kulaumiwa uwajibikaji wa pamoja ndio suluhu

Sasa hata ukiwa na kocha mzuri mfumo utakuziba TU na atamukiwa na mfumo mzuri wachezaji watakuziba TU na hata ukiwa na wachezaji wazuri kocha inawezekana akazingua TU

Hawa watatu ni wamoja
 
Nchi hii ina fedha nyingi sana.

Muhimu ni Kila mwanchi aamke na tulazimishe kuitoa ccm madarakani.

Mpaka sasa imeshindwa kuendesha serikali!

It is about time mifumo ifanyiwe massive overhaul!
 
Nchi hii ina fedha nyingi sana...
Muhimu ni Kila mwanchi aamke na tulazimishe kuitoa ccm madarakani...
Upinzani wenyewe umeisha ingia kwenye mfumo wa CCM,Lema juzi alisema ilibidi waungane na Chadema na ccm ilikumwondoa Magufuli iliwaweze kulamba asali.

Nchi hii ni ngumu sana, Nyerere mwasisi wa taifa hili alitufanya vibaya kwenye mambo ya siasa,Zidumu fikra za mwenyekiti hii kauli ilikuwa haifai kutamkwa kwa watanganyika.
 
Upinzani wenyewe umeisha ingia kwenye mfumo wa CCM,Lema juzi alisema ilibidi waungane na Chadema na ccm ilikumwondoa Magufuli iliwaweze kulamba asali...
Mabadiliko makini na endelevu ya mifumo yataletwa na wananchi wenyewe. Si vyama vya siasa!!
Wake up my people!!
 
Mabadiliko makini na endelevu ya mifumo yataletwa na wananchi wenyewe. Si vyama vya siasa!!
Wake up my people!!
Wananchi wanapitia wapi wakati kuondoa mfumo huu wa kisisimu lazima upitie chama cha siasa,navyama vyote vimeisha ingizwa kwenye mfumo huu wa kisisimu wanaramba asali.
 
Wananchi wanapitia wapi wakati kuondoa mfumo huu wa kisisimu lazima upitie chama cha siasa,navyama vyote vimeisha ingizwa kwenye mfumo huu wa kisisimu wanaramba asali.
Mkuu Tatizo la nchi hii ni namna tulivopata uhuru... Watu hawakuwahi kuingia mtaani kudai haki zao!
Wananchi ndo wenye hatma ya nchi yao.

Vyama vya siasa ni njia mojawapo tu! Sasa huwezi kuniambia kuwa hutaki kuondoa mfumo mbovu uliopo kisa hakuna vyama!

So Kwa utashi wako tuendelee tu kuibiwa tukisubiria vyama stahiki si ndiyo??
 
Mkuu Tatizo la nchi hii ni namna tulivopata uhuru... Watu hawakuwahi kuingia mtaani kudai haki zao!
Wananchi ndo wenye hatma ya nchi yao. Vyama vya siasa ni njia mojawapo tu! Sasa huwezi kuniambia kuwa hutaki kuondoa mfumo mbovu uliopo kisa hakuna vyama!

So Kwa utashi wako tuendelee tu kuibiwa tukisubiria vyama stahiki si ndiyo??
Vyama vya Siasa na wanaharakati ndio vilikuwa macho na mdomo wa kuwambia wananchi matatizo ya Serikali yao kabla ya kuingizwa kwenye mfumo.

Maana matatizo ya nchi hii Mengi tuliyajua kupitia kwa wanasiasa na wanaharakati, Sasahivi tafuta habari hizo kama zipo, Maana Sasahivi wamekabidhiwa kila mtu buyu lake.

Sasa hivi jaribu kusema Serikali ya Samia vibaya uone mashambulizi utakayopata kutoka kwa wanasiasa na wanaharakati,kwanza utaoneka kichaa furani hivi kwa kupinga Serikali ya Samia.
 
Mama anaupiga mwingi. Awamu ya 5 ilikuwa ya kifedhuli. Watanzania hatutakubali kamwe kutawaliwa na watu jamii ya Sukuma Gang wasio na ubinadamu wala utu. Kama kuna Sukuma Gang anataka uongozi aende akagombee kwa tiketi ya CHADEMA kwasababu huko ndo kuna upungufu.
Ile jamii ya akina Vitara hautaki tena kamwe abadani,asilani🏃
 
Vyama vya Siasa na wanaharakati ndio vilikuwa macho na mdomo wa kuwambia wananchi matatizo ya Serikali yao kabla ya kuingizwa kwenye mfumo...
Kuna nchi zipo wananchi wake wako very active. Kitu kidogo tu tayari wanahoji kiasi kwamba vyama vya siasa na wanaharakati wanafanya kuwatuliza.

On the contrary; waTanzania wanakasimu majukumu yao ya kuifuatilia, kuihoji na kuiwajibisha serikali kwa vyama na wanaharati.

Tuendako si Salama zaidi. Ipo siku watalambishwa asali wote hao na ndipo mtakosa msemaji na mtetezi!
So, amkeni mapema!
 
Back
Top Bottom