Kama uko serious sio lazima sana ulitumie shamba lote kwa mara moja. Tenga ten acres halafu fanya yafuatayo
1) . Nunua Ng'ombe Jike kama Kumi mpaka Ishirini
- Mitamba kams 10. Walozaa Kama 5 na Ndama 5
- Chagua Fresians, Asians na Mpwapwa (Hawa wanahimili Joto)
2) . Wazalishe kwa artifiacial Insermination (Uzalishaji wa chupa) faida yake ni kuwa unaweza chagua mbegu ya ndama uitakayo
3). Tenga tena Ekari tano lima mazao haya yafuatayo
A. Green Beans, zinauza sana, na majani yake utalishia ngo'ombe zako
B. Baby Corn (Mahindi Machanga) yanauza sana, na majani yake yana maziwa kwa ng'ombe
C. Alizeti utapata mashudu
D. Desimodiamu(kiingeereza ila sikumbuki spelling) ni majani yenye maziwa sana.
Kwa kufanya hivyo ng'ombe mmoja ataweza kukupa lita za maziwa 20 mpaka 40 kwa mkamuo mmoja. Jumla lita 40 mpaka 80 kwa siku kwa ng'ombe mmoja.
Kwa ushauri zaidi na jinsi pia ya kuwapata nitakupa mawasiliano, na ukitaka hao ng'ombe ntakuuzia na ushauri wa kitaalamu ntakupa. Pia mifano hai nitakuonesha na ntakupeleka kwa mashamba mengi.
Baada ya muda hizo ekari ulizotenga zitakuwezesha kuendesha shamba lote in five years to come.