Tuna vyuo vikuu bora, Kwanini tunashindwa kulimudu soko la Ajira?

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,252
Reaction score
8,003
Kuna usemi umeshakua maarufu 'Tatizo la ajira ni bomu linalosubiri kulipuka', lakini tatizo ni nini hapa? Nini mzizi wa tatizo hili? Leo hii wanagraduate watu zaidi ya laki 1.5 kwa mwaka!

Unaambiwa Mtanzania akisimama na Mkenya kwenye usaili, Mkenya anakupita mbali sana. Tatizo nini hapa? Watanzania tuko inferior kiasi kwamba uoga ndio chanzo? Pamoja na kuwa na vyuo vikuu bora Afrika lakini tunabaki kuwa wasindikizaji tu.

Naikumbuka sana lile shindano la Zain African Challenge Interuniversities Championship miaka ya nyuma lililoshindanisha wanafunzi wa vyuo vikuu Afrika. Tuliona wenzetu walivyotushinda mfano Nigeria, Kenya, Ghana na hata Malawi. Nini tatizo juu ya hili?
 
Tatizo ni products/graduates wetu hawana quality inayofaa, tumekuwa ni watu wa kukalili tu na kutema materials kwa Mitihani na mwisho wa siku tunajisifia kwa kupata GPA's kubwa...implementation yake inakuwa ni zero.
 
lawama zote nazitupa kwa wanafunzi kwani wanashindwa kujiongeza katika masomo yao wanaendekeza zaidi starehe wanasoma mradi liende tu kukariri mwanzo mwisho kufanya kwa vitendo kile kilichofundishwa ni ishu
 
lawama zote nazitupa kwa wanafunzi kwani wanashindwa kujiongeza katika masomo yao wanaendekeza zaidi starehe wanasoma mradi liende tu kukariri mwanzo mwisho kufanya kwa vitendo kile kilichofundishwa ni ishu

Uko sawa kabisa
 
Tatizo kubwa ninaloliona ni Lugha ya English ni sheedaa ila elimu iko sawa kama sehemu nyingine.

Hapo kwenye lugha ndio waganda na wakenya wametukamatia
 
Yeah tatizo ni hii lugha ya Kingereza.Lakin elimu yetu ni safi sana.Ninajua kuna vijana wa kitanzania wameanza mwaka1 ughaibuni na hapo kuna nchi nyingi sana za kiafrika.Wanaburuza wote bila kujali ni Mkenya au Mganda.

Ni kwamba hawatumii lugha ya kiingereza pale.Ndio kusema material tunayi kichwani ila tukifikai kujieleza kimombo tunaanguka.
 
Wabongo tunaakili sana...imagine tunasoma tu siku za mitihani zikikaribia na tunafaulu.,hapo tu mimi ndo napo waheshimu
 
Wabongo tunaakili sana...imagine tunasoma tu siku za mitihani zikikaribia na tunafaulu.,hapo tu mimi ndo napo waheshimu

Unaona ni akili ila kiukweli ni ujinga, swala la kusomea mitihani ndo sababu moja wapo bongo graduates hakuna wataalam kabisa wa kitu chochote kile, wote wanabahatisha mambo, mtu successful ni yule anasoma kupata knowledge,

anayejisukuma anasoma kila siku na anaenjoy anachokifanya, hawa wanaosomea mitihani sio akili bali ujinga... Hatuna wataalam tanzania kabisa, kila sector inamatatizo,

na siwezi kulaumu sana chuo maana siku zote juhudi zinaanzia kwa mtu binafsi kitu ambacho ni 1% ya wanafunzi ndo wanayo na ambao hua wanatoka vizuri wengine waliobaki hata barua ya kuomba kazi hawajui kuandika wanabaki mtaani afu wanalaumu serikali na vyuo huku walikua wanawaza ngono tu shuleni
 

Ngeli ni tatizo kubwa lakini tatizo kubwa zaidi ni msingi kuanzia chini.. Tanzania watu hawajitumi kabisa, mfano lile tangazo la hakielimu mwanafunzi anatangaza leo mwalimu wa history haji wanafunzi wanashangilia,

hili swala lipo kwenye shule zote Tanzania, hadi mtu anakuja kufika highschool ana msingi mbaya sana, huko chini kapita kwa kuungaunga tu, ukifika chuo ambapo panahitaji application ya knowledge yote ambayo mtu kakusanya toka chini inakua mziki mwingine.

Kuna nchi za wenzetu mfano South Korea mwalimu akikosa darasani wanafunzi wanachukia wanaweza enda kushtaki nyumbani, wanafunzi wanajituma kulala masaa manne kila siku, akitoka shule ni tuition hadi usiku, akirudi home ni lecture online na homeworks,

bado wanasaidiana na wazazi pia, mtu akifika chuo anahistory nzuri sana huko nyuma, huwezi mkimbiza mtu kama huyo, hiyo ndo 90% ya wanafunzi wao, ila kwa tanzania wanaofanya hivo ni chini ya 1%... In reality tuko kwenye condition mbaya zaidi ya tunavofikiria.
 
Tatizo si kutojua mambo, tatizo liko kwenye kujieleza tu. mwanafunzi wa darasa la saba wa kenya anaweza kujieleza vizuri kwa kiiengereza kuliko mwanafunzi wa chuo kikuu hapa TZ.

Dudu linaloitwa serikali ndio kiini cha tatizo hili. english kule primary ni almost haifundishwi kabisa. alafu mwanafunzi akianza fomu wani anakumbana na english, kwaiyo ile miaka minne ya sekondari mwanafunzi anapambana kujifunza english na kuitumia kwenye masomo yake, jambo ambalo ni gumu.

Ushauri. elimu ya darasa la kwanza hadi la tano ijikite kufundisha lugha ya Kiswahili, english na hesabu tu. darasa la sita na saba masomo mengine yaqfundishwe kwa kiingereza. kiswahili libaki kuwa somo tu.
 
Siwezi kujilaumu au kuwalaumu wanafunzi wa Tanzania,

Ila nailaumu serikali kwa kukumbatia mfumo huu wa elimu usioweza kumuandaa mtu kujiajiri na kujiamini..tatizo siyo lugha kuna watu wanajua kuongea kiingereza vizuri lakini ni waoga na bado wana fikra za kuajiriwaa.

Pia unaposema tuna vyuo vikuu bora inabidi tujue ni bora katika nyanja gani? vinaweza kuwa bora katika mambo mengine lakini siyo katika elimu vinayotoa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…