yutu
JF-Expert Member
- Nov 24, 2013
- 1,668
- 1,017
Habari wadau,
Mimi na mke wangu tuko kwenye ndoa mwaka wa 17 sasa na tumejaaliwa kupata watoto wanne wote wa kike.
Kutokana na uzazi wa mke wangu kujifungua kwa operesheni mara kwa mara madaktari hospitali ya mwananyamara walitushauri kuwa mke wangu afunge kizazi kwani mimba zaidi ya nne kwa operesheni itahatarisha uhai wake na mtoto pia endapo ataendelea kuzaa.
Kweli tulikaa na mke wangu japo tulitaka kuendelea kuzaa walau tupate mtoto wa kiume tukaona ni vizuri kufuata ushauri wa madaktari na kufanya kama walivyotushauri kwa kufunga kizazi.
Mwezi na siku na kadhaa zilizopita mke wangu alijisikia vibaya atukutilia maanani sana japo dalili zilikuwa ni za ujauzito kwani tuna miaka minne toka alipojifungua na kufunga kizazi.
Lakini hali hiyo iliendelea mpaka tulipoenda hospitali na kugundulika ana ujauzito wa miezi 3 na manesi walisema tayari hiyo mimba ni kubwa na kutokana na mishono aliyoshonwa tayari ni tatizo na kwa kifupi haitawezekana kujifungua salama eidha mtoto afe mama apone au mama afe mtoto apone
nilipopata hizi habari nilishtuka na kuhuzunika sana.
Nakuja mbele yenu wanajamvi mnipe ushauri mwenye uzoufu na masuala kama haya naamini kabisa inawezekana madaktari hawakufanya kazi yao ipasavyo katika kufunga kizazi lakini tayari tatizo limeshatokea, je tuuwe kiumbe au kilichopo tumboni au tufanyaje?"
Ushauri tafadhari.