Tunaanza na Tume Huru Kwanza

Je, mtoto anaweza mzaa mama?!
Ndicho act wanachotaka?!
 
Act ndio chama gani hiki,mbona cha hovyo kiasi hicho!chama akijui hata nguvu ya rais aliyonayo kwenye tume ya uchaguz bila katiba mpya usitegemee ccm kutoka madarakani.
 
Tatizo wapinzani ni ndumila kuwili ni ACT haohao walikuwa pamoja na wenzao kutokuutambua uchaguzi uliopita waliporushiwa mfupa wa serekali ya mseto Zanzibar tayari uchaguzi ukawahalali kwao utafikri siyo wale waliokuwa wanapinga uchaguzi.

Na hata hili la Rais la kukutana na wapinzani nalo linawatia doa wapinzani kuwa hawako kitu kimoja, baadhi ya wapinzani wanakubali vipi kwenda wakati wapinzani wenzao wako jela kwa makosa ya kubambikizwa wakati ilitakiwa wakomae wote kwa pamoja wasiende mpaka wapanzani wenzao watakapoachiwa huru.
 
Hawala" kingereza mnaitwa concubine wa ccm au siyo mwami?

Kumbe mnapewa mil,370 kila mwezi KWA siri Ili kuiua CDM
 
ACT ni zao la CUF chini ya hayati Maalim Seif.
Mwaka 2010 CUF na CCM walikubaliana uwepo wa serikali ya umoja wa kitaifa (GNU)

Walikubaliana uwepo wa TUME HURU ya Uchaguzi, iliyoundwa na Wajumbe kutoka CCM na CUF

Mwaka 2015 Tume ikiwa karibu kutangaza matokeo ambayo CUF Walishinda, Mwenyekiti Bw Jecha akabanwa na '' kuhara na kubebwa na watu maalumu kisha kupata matibabu'' TV Zanzibar akibatilisha matokeo

Serikali ya CCM na vyombo vyake vikakubali uhuni uliofanyika.
Mahakama haikuwa na nguvu, maamuzi ya Tume huru iliyokuwa na CUF hayahojiwi mahakamani.

CUF ambayo ni ACT ya leo wakapoteza uchaguzi na Maalim Seif akabaki kuwa mhanga hadi kifo

Tume huru haihakikishi uchaguzi huru. ACT wameshiriki chaguzi nyingi hawakuhujumiwa na Tum
Kazi ilifanywa na vyombo vya dola kwa baraka.ACT hawajashinda hata mtaa mmoja

Serikali za mitaa hazisimamiwi na tume! ACT hawakumbuki uhuni uliofanywa

Kama kuna kundi linalohujumu katiba mpya, ACT ni sehemu kubwa sana na muhimu ya kundi hilo

Kuna jambo la kujiuliza ikiwa ACT wanakumbukumbu, wanafikiri sawasawa au Wanatumika

JokaKuu Mag3 Pascal Mayalla Matola
 
Tume huru utaipataje chini ya Raisi mfalme, kwanza Raisi apunguzwe nguvu, ndo tume itakuwa huru
 
ACT wanafanya siasa za kuifurahisha CCM, ACT inataka ifanye siasa za kuonekana wastaarabu mbele ya CCM. Ukitazama vizuri kwa sasa, ACT inafanya siasa za Zito alizokuwa anazifanya miaka yote alipokuwa CDM. Ni vyema wapinzani wa kweli wakawa makini sana na siasa za ACT/Zito, ambazo ni za ghiliba. Wapinzani wa kweli wabaki na hoja kuu ambayo ni katiba mpya na sio kutekeleza matakwa ya CCM ya tume huru ya uchaguzi, ambayo lengo ni kuipa ACT viti kadhaa lakini CCM ikijihakikishia inabaki madarakani kwa shuruti.
 
Hapo kwenye baada ya usaili majina yapelekwe kwa rais kwa ajili ya uteuzi ndipo mm binafsi nina mashaka napo uwezekano wa mteuliwa kutii maagizo ya mteuaji Ni mkubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..tatizo haliko ktk tume ya uchaguzi peke yake.

..tatizo liko ktk MNYORORO mzima wa uchaguzi hapa nchini.

..mfumo mzima unatakiwa ufumuliwe kuanzia ktk uandikishaji wapiga kura, kuteua wagombea, kampeni, ...mpaka hatua ya mwisho.

..kwa maoni yangu, michakato yote miwili ianze kwa pamoja, lakini ni lazima MFUMO WA UCHAGUZI uwe umebadilishwa kwa kuboreshwa kabla ya 2024.

Cc Nguruvi3
 
..tatizo haliko ktk tume ya uchaguzi peke yake.
..tatizo liko ktk MNYORORO mzima wa uchaguzi hapa nchini.

..mfumo mzima unatakiwa ufumuliwe kuanzia ktk uandikishaji wapiga kura, kuteua wagombea, kampeni, ...mpaka hatua ya mwisho.
Ndio maana nasema ACT wazalendo sijui kama wanajua tatizo ni nini!

Laiti wangalikuwa na kumbukumbu japo 25% yaliyotokea Zanzibar wasingejiunga na hatua ya Msajili hata kwa bahati mbaya. Sielewi kuna pipi gani wamepewa

Kinachoharibu uchaguzi si Tume ya uchaguzi. Mfumo mzima ni mbovu.

Dola inatumika kikamilifu. Zitto ana imani Msajili wa vyama aliyekaa kimya Kenan Kihongosi wa UVCCM akitoa matamshi ya mauaji, atakaa kimya kwa mwanachama wa ACT! Chama kitafutwa siku hiyo hiyo

Msajili aliyeshiriki ''kuua CUF'' ndiye huyo huyo leo wana 'dance' na ACT wazalendo.
ACT wanaamini ana nia njema na mchakato

Polisi walimkamata Zitto akifanya mkutano halali Lindi , ACT wanaamini tume huru Polisi hawataMkamata tena!

Wagombea wananyang'anywa form mbele ya Polisi ACT wanadhani hayatatokea kukiwa na tume huru. ACT wamegombea kila kiti hakuna walichoambulia zaidi ya vipigo, leo wapo meza moja na waporaji wakipanga mipango ya tume huru ya uchaguzi!! kama si kioja sijui

Orodha ni ndefu inatosha kuwaambi hujuma za uchaguzi ni za kimfumo si tume peke yake.

Zanzibar ilikuwa na Tume huru wakiwemo CUF wakaporwa uchaguzi na Jecha na vyombo vya dola. ACT ambao ni CUF wanadhani tume huru ina matokeo tofauti ni ile iliyowapora uchaguzi

Kufanya jambo lile lile kwa namna ile ile ukitegemea matokeo tofauti ni definition ya Insanity

Kwahili siamini kama ACT hawafahamu! nadhani kuna pipi wanapewa , let's hope that I'm wrong

Msoud Othman wa ACT aliacha kuwa AG akitetea Katiba mpya na Zanzibar yenye mamlaka! Kapewa ving'ora hakumbuki yaliyompa Maalim, kama si usaliti sijui ni nini

ACT mna feli na mnafelisha Taifa, hamna hoja. Ushirika wenu na CCM una madhara makubwa sana kwa Taifa hili. ACT si chama kikubwa bara lakini visiwani ni kikubwa

ACT acheni huu uzumbukuku, kumbukeni ya nyuma! msitumike kirahisi haina tija kwa Taifa
..kwa maoni yangu, michakato yote miwili ianze kwa pamoja, lakini ni lazima MFUMO WA UCHAGUZI uwe umebadilishwa kwa kuboreshwa kabla ya 2024.
True!
 

ACT ni CUF ya zamani, hakuna kilichobadilika. Hoja ya CUF ya Maalim ni Zanzibar yenye mamlaka kamili. Hoja hiyo ya CUF na shinikizo la CDM ndivyo vilimshinikiza JK kuanzisha mchakato wa Katiba

Mchakato wa katiba ulilenga kurekebisha mifumo ya nchi ikiwemo wa kupata Tume huru ya uchaguzi. Tume ni zao la Katiba kwani uwepo wake umeanzishwa na Katiba.

CUF ya Maalim walienda Bunge la Katiba chini ya Ukawa. Mwanasheria mkuu wa SMZ alikuwa Maosud Othman. Mwanasheria (AG) alijiuzulu kufuatia kutokubaliana na mambo ambayo serikali ya CCM iliyafanya ikiwemo kuhujumu mchakato wa katiba mpya

Masoud Othman sasa ni VP akitembea na ving'ora , ulinzi na kila faraja za uongozi, kasahau alisimamia nini na kwanini alijiuzulu kuwa AG.

Mh Masoud ambaye ni kiongozi wa ACT yeye na wenzake hawakumbuki madhila yaliyomkuta maalim Seif chaguzi nyingi ikiwemo ya CUF kuwa sehemu ya tume ya uchaguzi , Jecha akatenda

Masoud Othman kuongoza CUF kuingia makubaliano na CCM inachekesha wala haifikirishi
Kwamba lini CCM wamekuwa wema sana kwa wapinzani katika Taifa hili ?

Wale wanaohisi tu kuwa kuna kutumika na ''quid pro quo' ni ngumu sana kuwashawishi hakuna

ACT hawajiulizi ni kwa mapenzi yapi CCM wanataka Tume huru ya uchaguzi ikiwa hata mikutano hawaruhusiwi? Juzi kule Pemba Polisi wameshushwa vyeo kwa kuruhusu mikutano ya ACT, bado ACT wanadhani ipo namna tofauti na zile zilizofeli huko nyuma

Kwahili, ACT wanaharibu mchakato wa katiba, na kuna kila sababu ya kuamini lipo jambo!
 
Kujadili sinema za Zitto Kabwe ni kupoteza muda wenu bure.

Aliombewa kazi ikulu kaunda suti zimemkataa, msitumie muda wenu kuwajadili wahuni kama Zitto Kabwe.

Wazanzibar wanajipanga kukichukuwa hicho chama jumla na Ayatollah hatoamini macho yake.
 

Hao Wapemba walioko ACT wameingizwa mkenge na siasa za Zito, watatumika hadi wakija kustuka muda utakuwa umekwisha.
 
Hao Wapemba walioko ACT wameingizwa mkenge na siasa za Zito, watatumika hadi wakija kustuka muda utakuwa umekwisha.
Kwa mtu makini ''hesabu' za ACT Wazalendo hazieleweki kwa namna yoyote

Miaka 30 ya vyama vingi CCM hawakuwahi kujadili Tume huru ya uchaguzi.

Pressure ya Katiba mpya inawafanya watafute uhalali 'legitimacy' ya kuhujumu uchaguzi wakitumia vyombo vya dola na kujisafisha na tume huru.

Kwamba, Wapinzani wametaka Tume huru wamepewa na wameshindwa vibaya.
Mbele ya uso wa dunia itaonekana kweli na CCM watafanikiwa na kuduwaza watu.

Baada ya kupata uhalali wa uchaguzi kwa Tume huru inayoshirikisha ACT, CCM wataandika katiba wanayotaka wao. Bungeni watakuwa kama walivyo sasa .

Watu wajiulize, ACT kweli walikaa chini na kufikiri sawa sawa au walikaa chini na kutafakari kingine tusichojua na kuamua kuingia chaka hili. Kuna motive ya hili jambo! si bure
 
Umesema yote mkuu,tukisema Zitto hamna kitu kichwani na yuko upande CCM,mtu wa siasa maslahi,mnakasirika.

Anapoipeleka ACT ndiko Lipumba alikoizika CUF. Zanzibar wanashabikia ACT kwa sababu za kidini tu.
 
ACT nyinyi ni hopeless kabisa. Utapataje tume huru ya uchaguzi bila kufumua katiba ya nchi ???

Mmepewa tenda ya kuneutralize agenda kuu ya katiba mpya kwa kuchukua kiagenda kidogo ndani ili mpunguze nguvu ya uhitaji wa katiba mpya.
 
Yan Zitto ni Yuda Iskariote

Mpe tu vipande 30 vya fedha and you own him, he is the cheapest political commodity in the land, so very sad😔
 
Wafuasi wa kilichokuwa chama kikuu cha upinzani wanavyoushambulia uzi wa ACT wazalendo ni dhahiri wanatambua 2025 hali ni mbaya kwao.
Mtake msitake 2025 ACT wazalendo wanakwenda kupata wabunge wengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…