Tunaanza na Tume Huru Kwanza

Yaani hata wewe unainhia kwenye mitego ya Hawa waramba viaty wa kiongozi mkuu wa chama,
Kati ya Mzazi na mtoto yupi alianza kuzaliwa?
Inatakiwa tushawishiwe kwa hoja Katiba ni ya wananchi sio ya wamiliki wa vyama vya siasa

Bila maridhiano hakuna Katiba mpya na wakushaiwishiwa ni CCM na si mwingine

Shida iliyopo ni Chama kimoja kuona kina haki ya kupata Katiba mpya kitu ambacho ni NDOTO , bila mtawala kuridhia ni ngumu na mtawala anatakiwa ashawishiwe kwa hoja vinginevyo utakuwa wimbo tu wa miaka na miaka
 
Mzee tuwe wakweli, hivi unafahamu makundi ya wajumbe wa Tume ya Katiba? Kwa taarifa yako hawa wabunge waliopo ndio wataokuwa kundi kubwa la wajumbe. Je kwa maoni yako thabiti unafikiri ni nini kitafanyika hasa ukizingatia uelewa wa hawa wabunge?
Tunaweza kutengeneza Katiba ya ajabu sana kama zilivyo hizi sheria zilizotungwa katika hili Bunge la safari hii. Kwa ushauri wangu Tume huru itaweza kutupatia walau wabunge kutoka vyama vingine vya kisiasa na baadae tukaingia katika Bunge la Katiba tukiwa na akina Lema, Mbowe, Zitto, Heche, Sugu na wengineo wenye uelewa mpana.
Vinginevyo kwa HARAKA tulionayo tunaweza kutunga katiba tutakayoikana baada ya muda mfupi na ikaweka rekodi ya kuwa Katiba iliyoishi muda mfupi zaidi duniani!
 
Kwani rasimu ya katiba Si ipo tayari ?
 
Kwani rasimu ya katiba Si ipo tayari ?
Kwa hawa wanasiasa tulio nao bado wanaipinga. Wanataka ile ya Warioba. Kwa hiyo tunayo makundi matatu
1. Kuna wale wanaoipendekeza Rasimu ya Kikwete
2. Kuna wale wanaitaka Rasimu ya Warioba
3. Kuna wale wanaotaka tuanze upyaaaaaa
 
Kiziwi hata ukipiga kelele vipi hatakusikia. Mbona Chadema kila siku wanaelezea umma umuhimu wa kuanza na Katiba mpya?

Amandla...
 
Kwa hawa wanasiasa tulio nao bado wanaipinga. Wanataka ile ya Warioba. Kwa hiyo tunayo makundi matatu
1. Kuna wale wanaoipendekeza Rasimu ya Kikwete
2. Kuna wale wanaitaka Rasimu ya Warioba
3. Kuna wale wanaotaka tuanze upyaaaaaa
Ya Kikwete inayo mambo yanayokwaza sasa hivi kama mamlaka ya Raisi kwenye teuzi, muundo wa tume ya uchaguzi bado yako vilevile.
 
Ya Kikwete inayo mambo yanayokwaza sasa hivi kama mamlaka ya Raisi kwenye teuzi, muundo wa tume ya uchaguzi bado yako vilevile.
Ndio maana tunataka watu wanaoweza kuzidadavua zile Katiba ya Kikwete na Warioba ili tupate suluhisho la kudumu. Ila kwa hawa Wabunge tulionao pale Mjengoni hatutoweza kupata Katiba Bora!
 
Inawezekana kutunga/kuandika katiba bila kutumia Bunge lililopo la akina Msukuma na akina Babu Tale.

Kumbuka kuwa mamlaka yote ya nchi hutoka kwa wananchi.Kwa hiyo wananchi wataamua ni akina nani waandike katiba.Hakuna alie juu ya wananchi.

Wananchi wana uwezo wa kusema kuwa akina Lema na kadhalika waandike katiba hata kama hawapo kwenye hili Bunge hewa.

Hili Bunge hewa lililotokana na kudra/mapenzi ya Magufuli badala ya kutokana na wananchi la akina Msukuma na Babu Tale halipo juu ya wananchi.
 
Ndio maana tunataka watu wanaoweza kuzidadavua zile Katiba ya Kikwete na Warioba ili tupate suluhisho la kudumu. Ila kwa hawa Wabunge tulionao pale Mjengoni hatutoweza kupata Katiba Bora!
Wabunge waliyopo hawapo kwa maslahi ya taifa bali ya waliyowaingiza mjengoni. Na hapo liitakapokuwa bunge la Tulia Ackson kwa uroho na ulafi aliyonao, ndio itakuwa mbaya zaidi.
Mhimili wa mahakama uliishakufa kwani waliishatamka wazi kuwa hawako tayari kuwa na mgongano na Bunge. Kwao Chief Hangaya walishaunda katiba yao IMARA kulinda nchi na taifa lao.
Hivyo basi wananchi twatakiwa kuacha ubinafsi na kuungana na kupambana ili kuweza kuunda Bunge huru la Katiba ili NASI kuilinda nchi yetu. Tuanzie pale alipoishia Warioba kwani yale ndio yalikuwa maoni yaliyotoka kwa wananchi.
Wenzetu Ghana walifanya hivyo 1990 ndio wakaweza kutoka kwenye mvurugiko kama huu waliokuwa wameingia
 
Wamejichanya kama NCCR nyakati za jiwe waliamini wangepewa majimbo leo wamekuwa wakali sana wa tawala za ccm...naona dhambarau nao wanapita humo kutaka kujaza matumbo kwa hisani ya Mtesi kitu hawajui tu wakati wa uchaguzi ccm wanakuwa hatari hawataelewa ujinga wakuwaachia majimbo ...baada ya 2025 watarudi humu kumwaga pove
 
Kuna tofauti kubwa kati ya Ghana na Tanzania hasa kwenye harakati za kisiasa. Sisa za mapambano kwa Watanzania ni ngumu sana kutekelezeka. Tunaweza kuitisha mapambano lakini watakaopambana ni kiduchu sana. Huo ubinafsi ulianza wakati uleee Zuberi Mtemvu alipojitenga na Kura tatu pale Tabora. Wenzake walimtenga akabakia peke yake na ANC yake.
 
Sasa unadhani katiba unaipataje bila kuwa na number bungeni?.
Hiyo sheria tu ya kuanza mchakato unadhani nani anaitunga?
 
Maridhiano yanapatikanaje kama sio kupiga kura na wengi ndio wanspitisha wanachotaka?
Democracy ndio inataka hivyo huwezi pata katiba mpya kwa kupush hashtag na kulalamika clubhouse,
Nchi nzima wanaoingia clubhouse hawazidi 1000,sasa hiyo ajenda itapitaje?
 
Hujaelewa Act wanataka tume huru ianze ili uchaguzi ujao uwe huru ILI UPINZANI UPATE VITI VINGI BUNGENI,
Maana si mnasemaga ccm huwa wanaiba, ila upinzani wanashindaga miaka yote
Huwezi kupitisha katiba unayoitaka kama huna watu
 
Uko sawa, hebu toa wazo, katiba mpya unaipataje?
 
Hujaelewa Act wanataka tume huru ianze ili uchaguzi ujao uwe huru ILI UPINZANI UPATE VITI VINGI BUNGENI,
Maana si mnasemaga ccm huwa wanaiba, ila upinzani wanashindaga miaka yote
Huwezi kupitisha katiba unayoitaka kama huna watu
Uwezekano wa tume huru haupo. Hao ACT ni mazwazwa. Tume huru misingi yake iko kwenye katiba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…