Tunaanza na Tume Huru Kwanza

Mimi hata siwaelewi wakina Zitto. Pamekuwa na chaguzi kiasi toka ile ya 2020 na ACT wameshiriki kikamilifu. Kama sikosei ACT wameshinda moja tu tena kwa mbinde. Kuna chaguzi nyingine huku bara wamelalamika kufanyiwa ubabe ule ule wa 2020. Ya mwisho ndio hawakupata hata kura 200. Sasa ikiwa wanachezewa rafu katika nchi ambayo wao ni washiriki kwenye utawala nini kinawaamisha kuwa 2025 hali itakuwa tofauti? Labda kama wanategemea hisani.

Fatma Karume alitoa pendekezo zuri sana kuhusiana na cheo cha Spika. Kwa vile inaelekea Spika anajiona kuwa ni Rais mtarajiwa basi anaona ni muhimu ajipendekeze kwa mamlaka yenye nguvu ya kuteua mgombea urais. Fatma alishauri kuwa ili kuepukana na tamaa hizo, Katiba imzuie Spika kugombea nafasi yeyote ya kisiasa muhula wake utakapoisha.

Hii itaondoa uwezekano wa kuwa corrupted kwa ahadi ya cheo cha kisiasa. Mimi nashauri iwe hivi kwa Jaji Mkuu, Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi na ile ya Vyama vya Siasa. Aidha, wasimamizi wote wa uchaguzi na wakuu wa vyombo vya usalama nao wasiruhusiwe kugombea kwenye chaguzi kuu mbili baada ya kutoka kwenye nafasi yao. Kwenye uspika, iwekwe wazi kuwa sio lazima kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa na mara ukichaguliwa hauruhusiwi kushiriki katika shughuli zozote za kisiasa za chama chako ( hamna mambo ya kuwa mjumbe wa NEC n.k.).

Mheshimiwa Rais anyang'anywe pia mamlaka ya kuwaondoa kwenye nafasi zao (kwa kuwapa kazi nyingine, kuwapandisha vyeo n.k) bila kutoa sababu inayoeleweka ambayo itakubaliwa na Tume itakayoundwa (kama Spika, tume iwe na maspika kutoka Jumuia ya Madola). Nadhani tukifanya hivi tutapata watumishi ambao wataweka taifa mbele na sio chama chao cha siasa.

Amandla...
 
Mimi hata siwaelewi wakina Zitto. Pamekuwa na chaguzi kiasi toka ile ya 2020 na ACT wameshiriki kikamilifu. Kama sikosei ACT wameshinda moja tu tena kwa mbinde.
Ile chaguzi wala hawakushinda kwa kampeni, lile ni jimbo lao na walitishia kujitoa. CCM waliona isiwe tabu ili kuendelea kuudanganya ulimwengu jimbo moja si deal , wakawapa
Huku bara si kwamba wameshindwa tu, bali pia walipigwa sana. Hawajaambulia chochote
Hapa ndipo tunawauliza haya yote yamefanywa si kwa idhini ya Tume bali vyombo vya dola, sasa wao wanadhani Tume ina nguvu gani kubwa kuliko vyombo vya dola?

Jecha si alichukuliwa na vyombo vya dola, Tume ilifanya nini!
Ndio msingi hasa wa sisi wengine kuhoji, huko ACT Wazalendo kuna watu wanafikiri ?
Ni moja ya msingi mkubwa wa kuwa na katiba. Tunakumbuka Mwenyekiti wa NEC aliwahi kuchukua fomu za kugombea Urais kupitia CCM.

Kinachotakiwa ni kuwa na sheria kwamba kuna nafasi hazitaruhusiwa kugombea nafasi za kisiasa au utumishi katika serikali

Nafasi hizo ni pamoja na za Spika na Naibu wake na kwamba takayechaguliwa kuwa Spika wa bunge atakuwa amepoteza uanachama wake wa chama cha siasa na hataruhusiwa kufanya siasa tena katika maisha yake. Hii inawezekana kwa kuzingatia kuwa masilahi yao ya leo hii yanawahakikishia maisha mazuri hadi kufa

Jaji mkuu na Majaji wa Mahakama kuu wasiruhusiwe kugombea nafasi yoyote au kuteuliwa nafasi yoyote ya kisiasa au utumishi katika serikali kwa muda wa maisha yao yote.

Kwamba mtumishi katika ngazi ya Jaji wakimaliza muda wao wa utumishi wasiteuliwe tena katika Taasisi za Umma au serikali katika maisha yao yote.

Mwenyekiti wa NEC asiruhusiwe kuwania nafasi ya Urais au uongozi katika serikali katika maisha yake. Wajumbe wa NEC nao wapewe muda wa miaka 20 kabla ya kujiunga na siasa tena

Rais asiwe na mamlaka ya kuteua Wajumbe wa NEC wala uwezo wa kutengua.
Kazi ya Rais iwe kusaini majina yanayofikishwa 'vetting' kwa namna yoyote

Polisi katika ngazi za Kamishna kwenda juu wasiruhusiwe kushiriki siasa baada ya utumishi wao

Hayo ni baadhiya mambo yatakayohakikisha kuwa wale wanaoteuliwa kwa majukumu kadhaa wapo committed na nchi na hawatakuwa compromised na mambo au mtu mwingine.
 
Ile chaguzi wala hawakushinda kwa kampeni, lile ni jimbo lao na walitishia kujitoa. CCM waliona isiwe tabu ili kuendelea kuudanganya ulimwengu jimbo moja si deal , wakawapa...
Mimi nawashangaa sana ACT. Wamepigwa, Ado Shaibu na wenzake wameswekwa ndani lakini kimya. Wanaugulia tuu maumivu yao wakitumaini ushindi Zanzibar utawapa uongozi wa upinzani Bungeni.

Nimeyapenda sana mapendekezo yako juu ya viongozi. Ni muhimu kukata huu mlango wa kuzunguka kati ya utendaji na siasa. Kwenye hili tuwaige waingereza sio wamarekani.

Amandla...
 
Mimi nawashangaa sana ACT. Wamepigwa, Ado Shaibu na wenzake wameswekwa ndani lakini kimya. Wanaugulia tuu maumivu yao wakitumaini ushindi Zanzibar utawapa uongozi wa upinzani Bungeni...
Kule Pemba kuna Polisi kawa demoted kwa kuruhusu mikutano ya ACT.
ACT wanaamini tatizo hilo litamalizwa kwa kuwa na Tume huru

Kinachonishangaza ni ufupi wa kumbu kumbu. Walishakuwa sehemu ya tume huru kupitia CUF. Walipokwa matokeo na Jecha na hawakumfanya lolote.

ACT wanasahau jinsi CUF ilivyouawa. Haikuwa Tume ya uchaguzi, ni ile taasisi nyingine ya vyama.
Wamepigwa sana kila uchaguzi mdogo. Hawakupigwa na Tume bali vile vyombo vyetu

ACT wanakaa na Msajili wa vyama wala hawamuulizi sheria ya kuzuia mikutano imeandikwa wapi!
Wanakaa na msajili hawaulizi kwanini kuna vyama vikitoa matamko ya mauaji havichukuliwi hatua!

ACT wanakaa na NEC hawawaulizi Wabunge 19 wapo Bungeni kwa sheria gani

Wanachoamini wao ni kuwa Tume huru itatoa haki, zile zile wanazonyimwa sasa!

ACT wajiulize hivi Othman Masoud si alikuwa mtu wa katiba ya serikali tatu, leo mbona kimya

Sidhani Zitto anayafanya haya kwa mapenzi, nadhani ACT kuwa na nguvu Zanzibar kunamweka Zitto katika wakati mgumu. Anajua wazi kinachofanyika si sahihi lakini kule si yupo Othman Masoud na ving'ora! Kelele za ving'ora zinamziba macho na masikio.

Katika sheria mbovu zilizopo na mfumo mbovu uliopo hata Tume ya uchaguzi ikiundwa na ACT/CDM/NCCR bado CCM watashinda kwa kishindo. Ndivyo walivyoshinda kule Zbar halafu wakamwambia Mbunge ajiuzulu na kuwapa kiti ACT. Yaani CCM wanaamua nani ashinde na inakuwa

Tunaposikia ACT wamekaa meza moja tena kujadili Katiba pendekezwa na Tume huru inasikitisha sana. Tunaweza kuwalaumu lakini huenda ni uwezo wa kufikiri na kupambanua! inasikitisha sana
 
 

Mtawala ndio Nani? Nchi Ni Mali ya wananchi na sio mtawala ambaye anakula na kuvaa kwa Kodi ya wananchi. Na baa ya miaka mitano anakuja kuomba aongoze Tena.
 
Hujaelewa Act wanataka tume huru ianze ili uchaguzi ujao uwe huru ILI UPINZANI UPATE VITI VINGI BUNGENI,
Maana si mnasemaga ccm huwa wanaiba, ila upinzani wanashindaga miaka yote
Huwezi kupitisha katiba unayoitaka kama huna watu

Tume Huru nje ya Katiba mpya Ni kujilisha upepo. Utakuwaje na Tume huru wakati structures zipo vile vile Kama zamani?. Tusiingie kwenye mtego wa ACT na Zitto Kabwe, hatujui wamehaidiwa nini. Kama walipewa Jimbo Pemba kwa makubaliano ya kutokuongelea katiba mpya nani ajuaye.
 
Sasa unadhani katiba unaipataje bila kuwa na number bungeni?.
Hiyo sheria tu ya kuanza mchakato unadhani nani anaitunga?

Kisheria Bunge la kawaida halipitishi katiba mpya Bali, bali Bunge Maalum la Katiba ndilo linalojadili rasimu na kuipitisha. Bunge la kawaida Lina badilisha tu vipengere vya katiba.
 
Chama Cha TISS hamuwezi enda tofauti na wanaowaseti nini Cha kufanya, Tunawajua.
 
Kwa mujibu wa Katiba Tume Tuliyo nayo ni Huru[emoji123][emoji106]
 
Ile chaguzi wala hawakushinda kwa kampeni, lile ni jimbo lao na walitishia kujitoa. CCM waliona isiwe tabu ili kuendelea kuudanganya ulimwengu jimbo moja si deal ...
Act kwa Sasa wameshakaribishwa mezani (serikali ya nusu mkate huko Zenji) na wamejihakikishia ruzuku ya kudumu.

Kwa Sasa Zitto ameshapata ajira ya miaka 9 ndani ya kikosi kazi hivyo kelele zake zitapungua.

Kiufundi Act na Zitto wameshapata wanachokitaka
 
Nyie ACT Mama naye kawauliza Nini maana ya Tume Huru mmeshindwa kujibu mkabaki mnacheka.
 
Nakubaliana nawe . Tatizo ni kwamba wanatumika kukwaza au wanatumika kama mpini

VP Othman Masoud alikuwa AG wakati wa Bunge la katiba. Maoud alijiuzulu nafasi yake kwasababu takwa la rasimu ya Warioba la katiba mpya halikutimizwa.

Othman alikuwa miongoni mwa viongozi wa UKAWA waliojiondoa Bunge la katiba

Leo kapewa ving'ora(Shaka anasema) hawezi tena kusimamia alichokiani

Majuzi waliadhimisha mwaka mmoja wa kifo cha maalimu.

Maalim aliamini katika katiba mpya na muundo wa serikali za muungano

Maalim alifarikia akipigani haki hiyo. Leo akina Othman na Zitto wameusaliti umaalim wanautukuza katika mikutano tu. Matendo yao ni kinyume kabisa

Lakini si Masoud na Zitto, unafiki upo kwa Wazanzibar.

Kesho akija Rais mwingine utasikia kelele zinaanza tena,kwasasa wametulia kwasababu wanachotewa tu kutoka Hazina Dar es Salaam, hawahitaji kwenda kazini au kuvua, hakuna shida tena ya katiba mpya wala muungano! ni starehe kwenda mbele

Zitto ametumika kupitia TCD na tulimuonya kuwa hataweza mbinu za dola.
Mkutano wake wa TCD ndio umezaa tume za akina Sheikh Alhad na Mkandala na yeye akiwemo

Zitto anafahamu 'usaliti' alioufanya kwa Upinzani, tazama kila mahali Task force ya Mkandala inapojitokeza Zitto ananekana kuwa na shaka na asiye ana furaha.

Nafsi inamsuta sana akijua amesaidia sana ''kuuza ghala la silaha''

ACT Wazalendo watakuwa washirika wa CCM huko Zanzibar hawatashika dola hata siku moja, kwa mtu wa bara anayetafakari sawa sawa ACT Wazalendo inatia shaka sana na haina lengo jema na Taifa hili.

Hatuwezi kumsema Mrema wa TLP au Cheyo wa UDP tukameza maneno kwa Zitto wa ACT. Hawa wanasafiri katika chombo kimoja , ni maswahiba wa Lumumba

JokaKuu
 
Kesho akija Rais mwingine utasikia kelele zinaanza tena,kwasasa wametulia kwasababu wanachotewa tu kutoka Hazina Dar es Salaam, hawahitaji kwenda kazini au kuvua, hakuna shida tena ya katiba mpya wala muungano! ni starehe kwenda mbele
Inawezekana Wazenji wametulia kwa sababu kero za muungano zimepatiwa ufumbuzi.
 
Inawezekana Wazenji wametulia kwa sababu kero za muungano zimepatiwa ufumbuzi.
Swali ni kuwa kero hizo zimepatiwa ufumbuzi kwanini imekuwa siri?

Yapi yamejadiliwa na Rais wa Zanzibar na Rais wa JMT Mzanzibar kuhusu Tanganyika?

Je, makubaliano yapo kisheria? Kama hayapo kisheria mbele ya safari akija mwingine na kugundua kuna madudu ''tunayodhani'' yapo ya kuwaumiza Watanganyika na Rais huyo akayaondoa Wazanzibar watalalamika?

Watanganyika wajiulize, ni kipi kimewatuliza Wazanzibar kwa miezi 12 iliyopita kiasi hata cha 'kumsaliti'' Maalim Seif? Kuna kitu gani?

Watanganyika hawahoji kwanini makubaliano ni siri ya Wazanzibar tu! Kuna nini

Ukiangalia kwa ujumla kuna unafiki mkubwa sana!
 
Ukweli tuanze na tume huru. Sababu

1. Ndio itasimamia kura ya maoni ya wananchi kuridhia rasimu ya warioba.
Tukienda na tume tuliyonayo tutatumia fedha zetu na matokeo tutaambiwa wana 70% wameikataa.

Tutaanza upya.
2. Tume hii itasimamia zoezi la uchaguzi iwapo kutakuwa na ucheleweshaji wa katiba mpya.

Ni mawazo tu mimi si mtaalamu wa sheria.

Matusi hapana
 
Ukweli tuanze na tume huru. Sababu

1. Ndio itasimamia kura ya maoni ya wananchi kuridhia rasimu ya warioba.
Tukienda na tume tuliyonayo tutatumia fedha zetu na matokeo tutaambiwa wana 70% wameikataa.

Tutaanza upya.
2. Tume hii itasimamia zoezi la uchaguzi iwapo kutakuwa na ucheleweshaji wa katiba mpya.

Ni mawazo tu mimi si mtaalamu wa sheria.

Matusi hapana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…