RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
📖Mhadhara (73)✍️
Miongoni mwa mambo ambayo yanasababisha kutokuwepo kwa nidhamu, uadilifu, weledi, na ufanisi kwa wafanyakazi wa makampuni na idara mbalimbali ni kuajiri watu ambao hawakukidhi vigezo vya ajira (nafasi) husika. Sikuhizi undugu ndio umeshika nafasi kubwa sana kwenye suala la ajira.
Kwa mfano kukiwa na uhitaji wa nguvukazi, ndugu anampigia simu nduguye anamuuliza; "Hivi ulisomea Diploma ya nini?" - Nduguye anajibu; "Nimesomea Diploma ya maendeleo ya jamii" - Ndugu anamwambia nduguye; "Kuna nafasi ya uhasibu hapa kazini kwetu inahitaji mtu mwenye shahada ya uhasibu, lakini njoo nikupachike wewe, majukumu ya uhasibu utajifunzia hapa hapa".
Utakuta mlinzi anayelinda na kufungua geti la Kampuni ana shahada nzuri ya Chuo Kikuu, lakini hao waliopo ndani ya kampuni wana diploma za ubabaishaji. Nikisema ubabaishaji namaanisha ni ubabaishaji kweli kweli, yaani mtu alisoma kwa ubabaishaji lakini Mungu si athumani alimaliza chuo, hata yeye mwenyewe hakuamini kama angemaliza chuo.
Kwa maana hiyo mlinzi alikosa "connection" ya kuajiriwa kwenye nafasi aliyosomea mwishowe na shahada yake ya uhasibu ameangukia kwenye ulinzi wa getini pasipo kupitia mafunzo yoyote ya mgambo, waliopitia mafunzo ya mgambo ndio wapo ndani ya vitengo. Ole wako wewe uende kuomba kazi na vyeti vyako vya Masters watakutoa mbio.
Wafanyakazi wengi wamekengeuka (hawana uadilifu) kwasababu wanadhani kwamba wanafanya kazi ya ukoo. Meneja ni baba mkubwa, HR ni shangazi, mhasibu ni baba mdogo, afisa manunuzi ni mjomba, wakili wa kampuni ni mtoto wa shangazi, afisa mahusiano wa kampuni ni mtoto wa dada.
RIGHT MARKER
DAR ES SALAAM.