SoC03 Tunachukua hatua sasa?

SoC03 Tunachukua hatua sasa?

Stories of Change - 2023 Competition
Joined
May 24, 2016
Posts
15
Reaction score
10
Nimeanza na swali hili ambalo lilikua ni wito kwa serikali zote Duniani kuhusu kusambaa kwa taka za plastiki katika mazingira yetu. Kiukweli taka za plastiki ni hatari Duniani kote si kwa binadamu pekee bali hata kwa viumbe wengine.

Katika maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani hapo Mei 5 mwaka huu kuna wito umetoka wa kuchukua hatua thabiti za kujinasua na tatizo la taka za plastiki maana imekuwa tishio wa usalama ya viumbe wote.

Hivyo kiongozi wa shirika la Umoja wa mataifa la mpango wa mazingira. Alitumia jukwaa hilo la maadhimisho kuleta wito kwa watu wote Dunia kuchukua hatua madhubuti sasa za kutokomeza taka za plastiki.

Amezitaka serikali na watu wote kwa pamoja na hata wafanya biashara na kampuni za biashara hakuziacha kuziagiza kupitia wito huo. Alienda mbali Zaidi na kuona kuwa uwezo upo wa kuweza kushinda na kuwa na jamii bora na safi kiafya, kiuchumi na maendeleo.

Hebu sasa tuone hiyo kauli aliyoitoa mbele ya viongozi wengine wa kimataifa na wakitaifa.

Dhamira kuu Katika Makala hii nataka tuangalie kama kweli hizo hatua katika nchi yetu zimeanza kuchukuliwa? Au la na kama bado nini kifanyike, tunahitaji maoni Zaidi ikiwa ni bado mapema hata mwezi mmoja haujaisha.

Kiongozi huyo kwa upande wake amesema, ikiwa tunaadhimisha siku ya mazingira Duniani kuna hatua zinatakiwa zichukuliwe sasa kutokomeza taka hizo. Na inawezekana kama tutashikana pamoja kama watu wamoja.

Amesema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya mazingira mwaka huu ambapo yalikuwa na kauli mbiu ya inayosema "tokomeza taka za plastiki". Kiongozi huyo ni Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo, UNEP - UN Environment Programme, Inger Anderson alisema "kwasababu taka za plastiki zinaisonga mifumo ya ikolojia, zinapasha joto hali ya hewa yetu na kuna uwezekano mkubwa wa kuharibu afya zetu.

Urudishaji tena viwandani siyo mazingaombwe. Mifumo yetu haiwezi kuhimili. Mabadiliko lazima yafanyike katika mzunguko wa maisha ya kuzitumia plastiki tena.

Alisema ni lazima kukataa vitu visivyo vya lazima vya matumizi ya mara moja. Tupange upya bidhaa na vifungashio ili kutumia plasitki kidogo tuzirudishe tena katika matumizi, tuzirudishe katika mzunguko tena, tuelekeze upya watu wetu na tubadilishe mifumo yetu."

Amesema kwa kufanya hivyo ndiyo Dunia itaweza kuengua plastiki katika mifumo ya ikolojia na uchumi, na kusisitiza kuwa hilo ni jukumu la kila mtu "Kila mtu lazima atimize wajibu wake.

Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali vinaweza kutoa mwongozo madhubuti katika kuweka sawa mpango huo wa kukomesha na kutokomeza uchafuzi wa mazingira kwa usambaaji wa plastiki kwa kuweka mijadala mbali mbali.

Wafanya biashara na biashara zao wanaweza kuchukua mtazamo mpya wa jinsi ya kukabiliana na janga hilo, sekta ya fedha inaweza pia kuwekeza mtaji wake katika kuchochea mabadiliko, na nchi zinaweza kutumia sauti zao, kura na hata fedha zao kuleta mabadiliko.

Kwa upande wake katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Geterres amesema katika kuunga mkono wito huo, "Kila mwaka, zaidi ya Malori 2,000 ya takataka zilizojaa plastiki hutupwa katika maeneo mbalimbali ya bahari, mito na hata maziwa yetu.

Matokea ya vitendo hivyo ni kusababisha janga. Hii husababisha chembechembe za plasitiki kuishia kwenye vyakula tunavyokula, maji tunayokunywa na hewa tunayoivuta."

Amesema kuwa plasitiki zimetengenezwa kutokana na nishati ya sumaku na kadiri tunavyozalisha plastiki zaidi ndivyo mafuta hayo ya kisumaku tunavyoyachoma na ndivyo tunavyofanya mgogoro wa tabianchi kuwa na taswira mbaya zaidi.

Hata hivyo amesema tunayo njia ya kupata suluhisho njia hiyo ni "Mwaka jana, jumuiya ya kimataifa ilianza kujadili makubaliano ya kisheria ya kukomesha uchafuzi wa taka za plastiki.

Hii ni hatua ya kwanza na ya kuonyesha matumaini, lakini tunahitaji kila hatua zilizo jadiliwa kutekelezwa."

Amesema na kuongeza kuwa ripoti mpya ya UNEP inaonyesha kuwa, "Tunaweza kupunguza uchafuzi huo wa taka za plastiki kwa asilimia 80 ifikapo mwaka 2040 kama ikiwa tutachukua hatua kuzirudisha tena katika viwanda, kuzichakata tena, kuelekeza upya njia bora ya matumizi, na kutenganisha plastiki na taka nyingine."

Hata hivyo aliweka msisitizo kwa kusema "Ni lazima tufanye kazi kwa pamoja yaani tuwe kitu kimoja, Serikali, kampuni za biashara na watumiaji kwa pamoja ili tuweze kuondokana na dhahama hii ya matumizi ya plastiki, kuweka msisitizo wa kutokuwa na taka za plastiki ili kujenga uchumi imara na wa kweli.

Amesema, kwa pamoja, tutengeneze maisha safi, yenye afya bora na endelevu zaidi kwa watu wote na viumbe vyote."

Alimaliza kwa kusema hayo, sasa swali langu hapa ni kwamba hizo hatua tumeshazianza au ziliishia siku ya tarehe Mei 5, 2023, katika midomo ya hao viongozi wa kimataifa wa Umoja wa mataifa?

Mnasemaje wenzangu una mchango zaidi wa nini kifanyike kuchagiza na kuhimiza viongozi wetu wa kitaifa kuchukua hizo hatua?

Na kama mwanachi mpenda maendeleo una njia nyingine bora ya kushauri viongozi wetu ili kuleta hamasa ya ukusanyaji na urudishaji bidhaa ya plastiki viwandani?

pexels-inchs-6702766 2.jpg
 

Attachments

Upvote 2
Back
Top Bottom