Tunaelekea wapi kama Taifa? Ni nini hatma ya Tanzania na raia wake katika Utawala wa Samia?

Ngengemkenilomolomo

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2015
Posts
316
Reaction score
549
Wakuu,

Inauma sana nimesikiliza jinsi viongozi wetu tuliowatuma (ingawa wengi hawakuchaguliwa kwa kura) kuwakilisha wananchi wanavyoongea kujibu hoja ya Gwajima.

Wamepotea watu wengi, wameuwawa watu wengi, wametekwa watu wengi hao wote wana wazazi, wana ndugu na wana familia pia lakini hakuna siku hata moja wabunge waliwahi kuhoji wala kusema chochote ila alipoguswa mtoto wa kiongozi tena kwa kutolewa mfano tuu wabunge wamecharuka mpaka wametoa laana
Inaumiza sana jinsi wanavyoongea yan unaona kabisa wanatetea matumbo na familia zao hawajali kuhusu wengine.

Inaumiza sana, ukitafakari kwa kina walichokiongea, hawaongelei kuhusu wananchi tena. Wanaridhika na wanafurahishwa na kinachoendelea maana wanajua hata tusipowachagua, watapita tuu as long as kuna mtu yupo na wanamuamini.

Mbunge Kasheku kaongea vitu vya ajabu sana ni moja ya viongozi niliokua nawakubali kwa misimamo na mawazo chanya lakin nimesikitika kwa kumshambulia mwenzie kwamba anatafuta huruma kwa sababu ameshindwa kutimiza ahadi zake. Je, yeye ahadi zote alizoahidi kwake jimboni amezitimiza?

Ukiwa mzalendo wa kweli na mwenye uchungu na nchi hii utaelewa namaanisha nini naposema inauma sana wawakilishi wetu kuona wanasimama na matumbo yao,wanasimama na familia zao na sio nchi wala wananchi.

Inauma sana!

Wengine wameenda mbali wanasema next time wakija watu kutoka nje warudishwe makwao wakiwa wanapumulia oxygen,imagine huyu mtu ni kiongozi anaewakilisha wananchi.

Ee Mungu simama nasi🙏
 
CCM kwa upana wake wote ni genge la majambazi hatari kwa taifa hili. Bila umma kulipuka na kusema no more lawlessness, tutaendelea kuendeshwa na shameless thugs!
 
It's a human nature pale maslahi yake yanapoguswa hugeuka mbogo na akili humtoka, wanatetea ugali wao, regardlessly!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…