Kwa kifupi hapa nitaelezea namna unavyoweza kurekebisha tatizo lako au hata wengine wenye simu za samsung ( android version ) maana ni tatizo la hizi simu kwa wengi sana.
Tatizo ni pale unapotaka kupiga simu na unapata ujumbe huu : “
NOT REGISTERED ON NETWORK.” hapa siongelei ujumbe wa :"
Mobile network not available" kwa maana Ujumbe wa
Not registered on network unamaanisha kwamba simu yako ina service na unaweza kupiga simu
Emergency calls only kama police, fire, ila huwezi piga simu tofauti na
Emergency calls.
NOT REGISTERED ON NETWORK:
Sababu kubwa ya kupata neno
NOT REGISTERED ON NETWORK ni pale mtandao wako au mtoa huduma wako anashindwa kuitambua au kuiruhusu IMEI namba za simu yako, mfano
0000000000000, au inayoanza na
0049XXXXXXXX,
3500000000000006 au
NULL
Kwahiyo check IMEI kwa kubofya
*#06# na uangalie kama imei zako ni fake kama zilizopo hapo juu, na kama ni hizo hapo juu basi mpelekee fundi ataweza kurapir IMEI na zitarudi zile za mwanzo ( original IMEI )
Sababu nyingine ya kupata neno
NOT REGISTERED ON NETWORK, ni
IMEI namba zako kuwa
blacklisted na
TCRA. Ku-blacklist kwa maana nyingine TCRA wameifungia IMEI namba zako kwasababu ambazo pengine wewe huzijui
Kwa suala kama hili hutokuwa na chaguo lolote zaidi ya kufuata yafuatayo
- Nenda Polisi na ukaripoti aliekuuzia hiyo simu( maana inaweza ikawa ya wizi au au imehusishwa na tukio )
- Wasiliana na aliekuuzia ili akurudishie hela zako
- Badilisha IMEI namba za hiyo simu ( kwa hapa kwetu hairuhusiwi )
- Kaiuze nje ya nchi.
Sababu nyingine ya kupata neno
NOT REGISTERED ON NETWORK inaweza ikatatuliwa kirahisi kama sio matatizo ya hapo
juu, Nitaelezea machache ila wengine wanaweza changia ya ziada kulingana na wao walivyotatua za kwao
.
1. kwanza nenda kwenye :
Settings.
2. Halafu nenda kwenye :
Wireless and Networks or Network connections.
3. Halafu bofya:
More networks →
Mobile Networks (Ukiona hujapata Mobile Netrwoks basi utabofya tena More Settings halafu uta search na uweze kupata "Mobile networks").
View attachment 509013
4. Sasa bofya
Networks operators.
View attachment 509016
5. Ikisha search itakuletea mitandao ya simu iliyopo TZ, Basi unachagua kulingana na line unayotumia ( kama ni Vodacom, TiGo, AirTel,Halotel, etc.)
Mpaka hapa nafkiri tatizo litakuwa limekisha,
Ukiona bado tatizo lipo basi rekebisha kidogo hapa:
Kwenye Mobile Networks, chagua
Network mode as
WCDMA only halafu zima na kuwasha simu yako na urudie maelekezo ya hapo juu.