KERO Tunahangaika sana kupata Pasipoti kutoka Uhamiaji huku vigezo vyote tukiwa navyo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

phano

New Member
Joined
Oct 31, 2024
Posts
1
Reaction score
1
Uhamiaji kumekuwa na malalamiko ya rushwa na usumbufu katika mchakato wa kupata pasipoti. Baadhi ya waombaji wanadai kuwa baada ya kujaza taarifa Mbagala na kwenda Posta kuchukua pasipoti, hupewa vikwazo mbalimbali au kuambiwa warudi kujaza taarifa upya.

Wengine wanasema wamezunguka kwa muda mrefu bila kupata pasipoti licha ya kuwa na vigezo vyote, hali inayodaiwa kuchochea mazingira ya rushwa na kufanya upatikanaji wa pasipoti kuwa changamoto kubwa.
 
Duhh, kwanini wanafanya hivyo?
 
Hii nch ngumu sana ..
Mifumo yake mpak ufanikiwe kujinasua umekauka..
Passport n haki ya mTz lkn inakua km unaomba bunduki ..
Vikwazo kibao
Kwa pesa wanazolipwa bado wananyemelea na za masikini! Inaumiza sana..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…