Tunahitaji Diamond Platnumz watano ili...

Tunahitaji Diamond Platnumz watano ili...

kende

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2013
Posts
3,527
Reaction score
1,668
Watanzania tumeanza kutembea kifua mbele kwamba mziki wetu umekua hadi tunaanza kujiona tunaenda levo za wanigeria wakati si kweli.

Kwa mtazamo wangu naona bado sana, coz hadi sasa hivi msanii ambaye anatupa kiburi cha kubishana na nchi nyingine e.g majirani zetu Kenya ni Diamond tu, huyo ndio tunaweza kumuita msanii wa kimataifa, huku wengine wakibakia kuwa local tu ingawa tuna wasanii wengi wazuri, hivyo hatupaswi kujisifia kwamba mziki wetu umekua, ila tunapaswa kumsifia personally Diamond amekua.

Ukiangalia upande wa Nigeria, wakisema kwamba mziki wao umekua ni chizi tu ndie anaweza kubisha, hawategemei big name moja tu kuwatangaza, wana lundo la mastaa waliotoka kimataifa i.e P2, 2Face, Dbanj, Jmartin,Davido,Wizkid,Iyanya,Flavour,Tiwa Savage, Yemi Alade, etc.

So ili nasisi tujiite tumekua kimuziki inabid ifikie wakati tuwe na list ya big names atleast watano, ila kwa style hii ya kuanzishiana team sidhan kama tutafika.

Hizi team ndio huamsha ushindani..

Sema nyingi teammavi zinatukana balaa,

Mi sidhani km timu ni nzuri, kitu kizuri ni kumpa sapoti kila msanii anayefanya vizuri, inawezekana kabisa kuwapenda wote Diamond na Alikiba as long as wote wanafanya vizuri; Natamani sikumoja kuona tuna big names kama Rich Mavoco, Alikiba, Ommy Dimpoz, Diamond, Barnaba, Vannesa, etc. Yaani idadi kama hiyo ya majina inatambulika kimataifa, hapo ndipo tutasema mziki umekua
 
Kweli umeongea vanesaa mdee anaelekea level izo ila wengine bado sana juhudi zinahitajika sn
 
Mi sidhani km timu ni nzuri, kitu kizuri ni kumpa sapoti kila msanii anayefanya vizuri, inawezekana kabisa kuwapenda wote Diamond na Alikiba as long as wote wanafanya vizuri; Natamani sikumoja kuona tuna big names kama Rich Mavoco, Alikiba, Ommy Dimpoz, Diamond, Barnaba, Vannesa, etc. Yaani idadi kama hiyo ya majina inatambulika kimataifa, hapo ndipo tutasema mziki umekua

Kuna video aliweka Idris Insta ungeziona ungejua nazungumzia nini....

I love Diamond ila haimaanishi siwezi support kazi za wengine..
 
Ay and Chibu dangote

Next namuona V Money,

next nilikua namuona Rich mavoco sasa simuoni tena sijui tatizo nn,
Kiba ,Ommy,Jux nahisi bado vitu kidogo tu wataingia kundini MUNGU jalia muziki wa tanzania upige hatua.
 
Watanzania wote tunajivunia KingKiba pekee kama msanii wa kimataifa ila hao wengine labda tuwape muda kidogo baada ya miaka kama 4 mbeleni.
 
Ay and Chibu dangote

Next namuona V Money,

next nilikua namuona Rich mavoco sasa simuoni tena sijui tatizo nn,
Kiba ,Ommy,Jux nahisi bado vitu kidogo tu wataingia kundini MUNGU jalia muziki wa tanzania upige hatua.

AY alikuwa na trend nzuri sana kabla ya Diamond but sahivi amestack, kwa juhudi alizowahi kuzifanya alistahili kuwa mbele ya Diamond, ni vile tu hana nyota ya mchezo
 
+Kuna vitu fulani wasanii wetu km kina V money wakiwa navyo au wakivifanya kuna uwezekano wakatuwakilisha vizuri km Diamond!

+ management makini
Msanii unatakiwa awe na management makini ambayo itakua na uwezo wa kumtafutia msanii link na wasanii pamoja na project za kimataifa.

+ kujitangaza mwenyewe pamoja muziki wake
Msanii makini ni yule ambaye anajitangaza vizuri ili kulibrand jina lake na muziki wake. Hii naona inamsaidia sana Diamond, mfano hata akitoa single mpya lazima afanye kitu fulani huko kwenye mitandao kitakachofanya watu wawe aware na nyimbo zake. Hapa sasa hivi tu meneja wake mmoja yupo busy Uganda unafanya media tour kuitambulisha Nana.

+ uwezo binafsi, kujituma na nidhamu ya kazi
Kuthamini muziki wako na kufanya serious kama watu wengine.
Hayo ni baadhi tu yakifuatwa nadhani tutawapata kina Diamond wengine wengi tu
 
AY alikuwa na trend nzuri sana kabla ya Diamond but sahivi amestack, kwa juhudi alizowahi kuzifanya alistahili kuwa mbele ya Diamond, ni vile tu hana nyota ya mchezo

Kweli Ambwene amestack bana,lkn namuaminia sana huyu kijana hope siku moja atarudi vizuri,
 
+Kuna vitu fulani wasanii wetu km kina V money wakiwa navyo au wakivifanya kuna uwezekano wakatuwakilisha vizuri km Diamond!

+ management makini
Msanii unatakiwa awe na management makini ambayo itakua na uwezo wa kumtafutia msanii link na wasanii pamoja na project za kimataifa.

+ kujitangaza mwenyewe pamoja muziki wake
Msanii makini ni yule ambaye anajitangaza vizuri ili kulibrand jina lake na muziki wake. Hii naona inamsaidia sana Diamond, mfano hata akitoa single mpya lazima afanye kitu fulani huko kwenye mitandao kitakachofanya watu wawe aware na nyimbo zake. Hapa sasa hivi tu meneja wake mmoja yupo busy Uganda unafanya media tour kuitambulisha Nana.

+ uwezo binafsi, kujituma na nidhamu ya kazi
Kuthamini muziki wako na kufanya serious kama watu wengine.
Hayo ni baadhi tu yakifuatwa nadhani tutawapata kina Diamond wengine wengi tu

Vee Money nae anazidi Ku shine for sure...
 
kende

Kimsingi naungana naww ila nadhani tatizo kubwa nililoliona na ni muda mrefu ni management. Talent tunazo, muziki mzuri upo mpaka saa nyingine hua natamani Africa ingeuskia huu mziki ila tatizo kubwa ni MANAGEMENT NZURI kama aliyonayo bwana diamond, tungepata wakina Babutale na Said Fella wengine watano wawasimamie wakina omy, kiba, v money, rich mavoko n.k. Nakwambia tungefika mbaaali sana
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom