Tunahitaji Katiba yenye kutuwajibisha sote kwa Umma

Tunahitaji Katiba yenye kutuwajibisha sote kwa Umma

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Tumeyasikia Ugiriki:

Screenshot_20230302-100759~3.jpg


Waziri mhusika wa usafirishaji wa serikali ya huko amejiuzulu. Ma stesheni master wamekamatwa.

Nini kiwafanye wenye dhamana kwetu kuwajibika?

Ndiyo maana watu watatekwa, pesa zitaibiwa, ajali zitatokea, nk, yaani mambo shaghala bagala. Uwajibikaji au matumaini ya baadaye yakiendelea kuwa zero.

Bila katiba mpya:

"Bado tupo tupo sana." -- Mwana FA.
 
Kama uwajibikaji haupo kwenye DNA zetu, basi ni lazima tulazimishwe hilo na Katiba Mpya, hakuna namna nyingine.
 
Ajali kila siku utafikiri wehu, mwisho wa siku anakuja mtu na nyota zake anasema ooh gari ilikuwa haina breaks

Wao ndio wanaruhusu hizo ajali kwa rushwa
Inatakiwa wainamishe vichwa kwa aibu ila kwa sababu mshipa wa aibu hakuna wainamishe hata mifuko
 
Kama uwajibikaji haupo kwenye DNA zetu, basi ni lazima tulazimishwe hilo na Katiba Mpya, hakuna namna nyingine.

Uzoefu umeonyesha bila ya kuwa na mustabala ambapo uwajibikaji ni kwa watu haya ndiyo matokeo:

Mbatia: Ajali ya MV NYERERE ni ya kujitakia tu

Kwa nini watu watekwe nyara, pesa za umma zitapanywe, uzembe wa wazi utokee, nk na hakuna mwenye kuwajibika?
 
Ajali kila siku utafikiri wehu, mwisho wa siku anakuja mtu na nyota zake anasema ooh gari ilikuwa haina breaks

Wao ndio wanaruhusu hizo ajali kwa rushwa
Inatakiwa wainamishe vichwa kwa aibu ila kwa sababu mshipa wa aibu hakuna wainamishe hata mifuko

Tusimame imara kudai katiba yenye kutaka uwajibikaji kwa watu:

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amepokea ripoti ya uchunguzi wa ajali ya kivuko cha MV Nyerere kutoka kwa kamati iliyoundwa na Serikali kwa ajili ya kuchunguza ajali hiyo. Amepokea ripoti hiyo Alhamisi, Oktoba 25, 2018 kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstafu, Jenerali George Waitara,kwenye makazi ya Waziri Mkuu, jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuishikuru kamati hiyo kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli kwa kazi kubwa waliyoifanya ambayo imethibitisha umakini wao.

Pia ameipongeza kamati hiyo kwa namna walivyotumia muda wao vizuri kwa kufanya kazi hiyo na kutoa mapendekezo kwa Serikali juu ya mambo waliyoyabaini. “Nimepokea taarifa kwa niaba ya Serikali, Serikali itafanya mapitio ya taarifa yote na viambatisho vyake na itapitia kwa kina mapendekezo mliyoyatoa ambayo yote yatafanyiwa kazi.” Waziri Mkuu ameongeza kuwa Serikali inaamini mambo yote yaliyosheheni katika taarifa hiyo ni yale ambayo Watanzania wanasubiri kuona yakifanyiwa kazi. MV Nyerere ilipindika na kuzama Septemba 20, mwaka huu katika ziwa Victoria ambapo Watanzania zaidi 200 walipoteza maisha na wengine Zaidi ya 40 waliokolewa.

Septemba 24 mwaka huu Waziri Mkuu alitangaza kamati ya kuchunguza ajali ya kivuko cha MV Nyerere yenye wajumbe saba ambayo iliyoongozwa na Jenerali mstaafu, Waitara. Akitangaza majina hayo kwenye kijiji cha Bwisya katika kisiwa cha Ukara, wilayani Ukerewe, mkoani Mwanza, Waziri Mkuu alisema wajumbe hao wanapaswa kuikamilisha kazi hiyo ndani ya mwezi mmoja. Aliwataja wajumbe wengine ni aliyekuwa Mbunge wa Ukerewe, Bw. Joseph Mkundi, Mhandisi Marcelina Magesa, Wakili Julius Kalolo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Bi. Queen Mlozi. Wengine ni SACP Camillus Wambura na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uratibu Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Bashiru Taratibu Hussein.

Itakumbukwa kwamba, kunako tarehe 21 Mei 1996 MV Bukoba ilizama katika Ziwa Victoria na kusababisha watu Zaidi ya 800 kupoteza maisha. Tarehe 10 Septemba 2011 Meli ya MV Spice ilipata ajali Bahari ya Hindi na kusababisha vifo vya watu 200 na tarehe 18 Julai 2012 Meli ya MV. Skagit ilizama katika Bahati ya Hindi na kusababisha vifo vya watu 150. Ni matumaini ya watanzania kwamba, ripoti ya Tume ya Waitara, itatoa ushauri ambao utaisaidia Tanzania kuweza kuboresha usafiri wa majini kwa kuimarisha usalama pamoja na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazopaswa kufuatwa na wadau mbali mbali, ili kuokoa maisha ya watu na mali zao!

Kwani nini kilifanyika?
 
Back
Top Bottom