Tunahitaji Katiba yenye kutuwajibisha sote kwa Umma

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Tumeyasikia Ugiriki:

Waziri mhusika wa usafirishaji wa serikali ya huko amejiuzulu. Ma stesheni master wamekamatwa.

Nini kiwafanye wenye dhamana kwetu kuwajibika?

Ndiyo maana watu watatekwa, pesa zitaibiwa, ajali zitatokea, nk, yaani mambo shaghala bagala. Uwajibikaji au matumaini ya baadaye yakiendelea kuwa zero.

Bila katiba mpya:

"Bado tupo tupo sana." -- Mwana FA.
 
Kama uwajibikaji haupo kwenye DNA zetu, basi ni lazima tulazimishwe hilo na Katiba Mpya, hakuna namna nyingine.
 
Ajali kila siku utafikiri wehu, mwisho wa siku anakuja mtu na nyota zake anasema ooh gari ilikuwa haina breaks

Wao ndio wanaruhusu hizo ajali kwa rushwa
Inatakiwa wainamishe vichwa kwa aibu ila kwa sababu mshipa wa aibu hakuna wainamishe hata mifuko
 
Kama uwajibikaji haupo kwenye DNA zetu, basi ni lazima tulazimishwe hilo na Katiba Mpya, hakuna namna nyingine.

Uzoefu umeonyesha bila ya kuwa na mustabala ambapo uwajibikaji ni kwa watu haya ndiyo matokeo:

Mbatia: Ajali ya MV NYERERE ni ya kujitakia tu

Kwa nini watu watekwe nyara, pesa za umma zitapanywe, uzembe wa wazi utokee, nk na hakuna mwenye kuwajibika?
 
Ajali kila siku utafikiri wehu, mwisho wa siku anakuja mtu na nyota zake anasema ooh gari ilikuwa haina breaks

Wao ndio wanaruhusu hizo ajali kwa rushwa
Inatakiwa wainamishe vichwa kwa aibu ila kwa sababu mshipa wa aibu hakuna wainamishe hata mifuko

Tusimame imara kudai katiba yenye kutaka uwajibikaji kwa watu:

Kwani nini kilifanyika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…