Tunahitaji Kinu cha Nyuklia kwa ajili ya biashara, mambo ya kutegemea umeme wa mvua yanazidi kutoweka

Tunahitaji Kinu cha Nyuklia kwa ajili ya biashara, mambo ya kutegemea umeme wa mvua yanazidi kutoweka

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
Tunasubiri nini wamanga hao hapo wamekuja juzi tu leo hii wanafungua Nuclear plant na itawapatia umeme wa kuchezea nasikia wameanza kuwasha mataa mpaka kwenye mitende, sisi tutwasha mpaka kwenye minazi.

Serikali ya Samia livalie njuga hili ili tuondokane na mambo ya kusubiria mvua ili mabwawa yajae, yaani nilipoona kwenye CNN jamaa wakifungua mitambo na kuongeza megawati 1400 kwenye gridi ya Taifa, nikajiuliza mbona Tz Uranium tunaichezea gololi, inakuwaje hawa washiiri hawana hata machimbo leo hii wanafungua unit after unit.

Hapa utasikia umeme unakatika kwa sababu maji yamepungua, hivi umeme una kiuno? Tunabambikiwa misamiati ya ajabu ajabu tu.

Samia funga kazi ili kabla ya 2025 tuone kinu cha umeme kinachotumia Nuclear Power Plant, mambo ya kutegemea umeme wa mvua yanazidi kutoweka.
 
Punguza jazba mkuu tulia pangilia vema mada yako, inawezekana ukawa na jambo la msingi sana
 
Tunasubiri nini wamanga hao hapo wamekuja juzi tu leo hii wanafungua Nuclear plant na itawapatia umeme wa kuchezea nasikia wameanza kuwasha mataa mpaka kwenye mitende, sisi tutwasha mpaka kwenye minazi...
Nenda kagugo "Chernobyl Disaster 1986" youtube halafu ukimaliza kuangalia video kadhaa urudi hapa tuendelee kujadili.

Ila kwa kifupi tu Nyuklia haifai taifa la watu wenye akili mbovu kama hizi zetu.
 
Japo sijaelewa wamanga, washiiri....ni watu gani, ila ni kweli kuwa kama taifa imefika wakati tuwe na nyuklia kwa ajili ya nishati.
 
Dunia inaenda kwenye umeme wa jua, huo ndio wa uhakika na wa kudumu.
 
Dunia inaenda kwenye umeme wa jua, huo ndio wa uhakika na wa kudumu.
Hapa hamna jua ,maana siku za mawingu hazipishani kihivyo,hatuna jua la kutuwezesha kutoa nishati ya kutosha.tutumie uranium hakuna zaidi ya hilo,kama ni kutupa makapi basi tuna mashimo makubwa tu yakiwemo bonde la ufa.

Wasomi wa elimu ya nuclear naamini wapo na hawana la kufanya ,yule aliyewahi kuwa makamu wa raisi nasikia ni gwiji wa mambo ya nuclear.

Au tunasubiri Wazenji waanze kuitafuta na kutumia teknolojia hio ? ndio na sisi tuzinduke ?
 
Mataifa makubwa hawatakubali sisi tuweke kinu cha nuclear..

Nchi yetu.. Viongozi wengi akili zao wanazijua wenyewe..

Nuclear Power Plant inahitaji nchi viongozi wawe na utulivu wa moyo kwanza..

Njaa kwa viongozi wetu.. Vitatuletea balaa hasa kwenye material zinazotumika kutengenezea umeme.. Hapa nazungumzia Radio Active Element kama Uranium..

Uranium zitaishia mikononi mwa Magaidi.. Tutakuwa exposed na radiation.. Magonjwa ya ajabu balaa.. Nchi itaisha..

Kama tuu sakata la mto Mara tunaona danadana.. Usimamizi wa Kinu cha nuclear na mazingira yetu tutaweza?
 
Hakuna msimu jua halionekani Tanzania, hata vipindi vya mvua na baridi jua bado huchomoza Tanzania.

Nchi zinazoongoza kutumia umeme wa jua ni pamoja na China, Japan na nchi za Ulaya ambako kuna vipindi virefu vya baridi.
[emoji57][emoji57][emoji57][emoji57][emoji57]Jua kuna msimu halionekani
 
Nchi pekee yenye uwezo wa matumizi sahihi ya nyuklia Africa ni Africa ya kusini.

Wengine hawana uwezo wa kusimamia miradi ya aina hiyo, wataishia kupewa "mabeberu" tu waimiliki na kuindesha kama kwenye gesi.
hapa hamna jua ,maana siku za mawingu hazipishani kihivyo,hatuna jua la kutuwezesha kutoa nishati ya kutosha.tutumie uranium hakuna zaidi ya hilo,kama ni kutupa makapi basi tuna mashimo makubwa tu yakiwemo bonde la ufa.
wasomi wa elimu ya nuclear naamini wapo na hawana la kufanya ,yule aliyewahi kuwa makamu wa raisi nasikia ni gwiji wa mambo ya nuclear. Au tunasubiri Wazenji waanze kuitafuta na kutumia teknolojia hio ? ndio na sisi tuzinduke ?
 
Tunasubiri nini wamanga hao hapo wamekuja juzi tu leo hii wanafungua Nuclear plant na itawapatia umeme wa kuchezea nasikia wameanza kuwasha mataa mpaka kwenye mitende, sisi tutwasha mpaka kwenye minazi.

Serikali ya Samia livalie njuga hili ili tuondokane na mambo ya kusubiria mvua ili mabwawa yajae, yaani nilipoona kwenye CNN jamaa wakifungua mitambo na kuongeza megawati 1400 kwenye gridi ya Taifa, nikajiuliza mbona Tz Uranium tunaichezea gololi, inakuwaje hawa washiiri hawana hata machimbo leo hii wanafungua unit after unit.

Hapa utasikia umeme unakatika kwa sababu maji yamepungua, hivi umeme una kiuno? Tunabambikiwa misamiati ya ajabu ajabu tu.

Samia funga kazi ili kabla ya 2025 tuone kinu cha umeme kinachotumia Nuclear Power Plant, mambo ya kutegemea umeme wa mvua yanazidi kutoweka.

Shocker sina uhakika juu ya kina cha uelewa wako kuhusu Nuclear Power! Labda nikutaarifu tu kuwa mataifa yote yenye uwezo wa kuzalisha nishanti ya nyuklia wana mipango ya kuondokana na nishati hiyo kwa kuwa nishati hiyo ni CHAFU!! It is unclean power and extremly risky!

Dunia ina mifano miwili ya hatari sana: Mfano wa kwanza ni kupasuka kwa kinu cha nyuklia huko ilikokuwa USSR na leo ni UKRAINE. mfano wa pili ni kupasuka kwa kina cha nyuklia huko Japan kutokana na tetemeko la tsunami. Hayo ni majanga makubwa sana na yalileta madhara makubwa kwa mataifa hayo

UJerumani ina ratiba kabisa ya kuachana na nishati hiyo. kadhalika Japan na mataifa mengine!! Ajali ya nyuklia usipime!! Siyo kitu cha kutamani! Ikiwa mataifa makubwa yanaachana na nishati hiyo ni kioja kwa nchi yenye uchumi wa chini kuwa na mawazo hayo.

Matumizi makubwa ya nyuklia kwa sasa si matumizi ya amani kama kuendesha meli kubwa za vita kwa kutumia nishati ya nyuklia.
 
U M A S I K I N I na N U C L E A R ni vitu viwili haviwezi kukaa pamoja...

Yaani unawaza kuzalisha Nuclear ilihali nchi yako unaiendesha kwa Mikopo,,, Vyoo vya shule bado unajenga kwa mkopo.
 
Back
Top Bottom