Tunahitaji kubadilisha mindset za Watanzania ili kuifikia nchi ya ahadi.

Joined
Sep 22, 2020
Posts
7
Reaction score
1
Watanzania wengi (Waafrika) mindset zetu kuna namna bado haziko huru yaani bado zinatawaliwa na watu wachache hasa mataifa yaliyoendelea. Inawezekana nitakuwa natumia lugha ngumu kama nikisema tuna colonised mind. Ndio ni maneno makali lakini huo ndio ukweli. Kuna mambo tunashindwa kuyafanya na kuna maamuzi tunashindwa kuyafanya pia kwasababu ya mindset zetu haziko huru. Kuna muda mtu anashindwa kufikia pontential yake kwasasabu ya kutojiamini na kuamini kwamba hicho kitu anachokifikilia kinawezekana kwa baadhi ya watu na sio yeye.

Hoja yangu kubwa ni utumwa wa fikira miongoni mwa Watanzania au Waafrika kwa ujumla. Ukitaka kudhibitisha hili angalia baadhi ya misemo inayosemwa na baadhi ya vijana; 'Ni bora kuzaliwa mbwa Ulaya kuliko kuzaliwa Afrika.' 'Bongo bahati mbaya.' Hii misemo tunaweza kuwa tunaichukulia kawaida au kiutani utani lakini inadhibitisha namna gani bado akili yetu ina shida, bado akili yetu haidhamini utu wetu.

Kwenye taasisi mbalimbali za umma na binafsi kuna muda watu weusi wanaweza kuwa kwenye foleni (queue) wanasubiri kuhudumiwa ila akija mzungu haijalishi yupo tabaka gani atapita moja kwa moja na hata akisimama watoa huduma wanaweza kuja kumchukua kumhudumia yeye kwanza. Wengi huwa wanatetea hili suala wakisema ni ukarimu wa wabongo lakini sio kweli, hapo kuna namna tunawapa heshima kubwa kuliko tunavyojipa wenyewe. Kudhibitisha hii hoja, nenda hotelini au hata baadhi ya maeneo hapa nchini, mtu mweusi harusiwi kuingia amevaa bukta lakini mtu mweupe anaingia. Huu ni utumwa wa fikira kwani tumejengewa kuwa-value hawa watu na sisi tumeamini.

Huwa kuna muda naamini labda ndio maana hata rasilimali tulizo nazo kwenye bara letu tunashindwa kuzitumia zitufikishe kwenye nchi ya ahadi kwasababu tunaamini hatuwezi kuzitumia mpaka tupate msaada kutoka kwa mataifa yaliyoendelea. Tunapoanza kutafuta msaada hapo ndo huwa tunaibukia kwenye mikataba mibovu isiyofaa na isiyo na manufaa kwa nchi zetu.

Aidha, ukiangali kwa wenzetu mambo mengi ya kimaendeleo katika nyanja tofauti tofauti yamenzishwa na mtu mmoja mmoja japo inawezekana baadae serikali zilitia mkono. Lakini hii kwetu ni tofauti kwani tuanakosa hadi udhubutu maana tunaogopa kufeli. Mfano, angalia waanzilishi wa mitandao ya kijamii, vifaa vya electronics, n.k. Waanzilishi ni watu binafsi. Tutasema wana uwezo kiuchumi ni kweli sikatai lakini ukiangalia kwetu huku hata serikali haziweki mipango ya kuwezesha hivi vipaji au watu wenye mawazo mazuri kufikia hatua fulani.

Naamini kuna haja ya kutengeneza kizazi kipya ambacho kina jiamini na kina uwezo wa kuleta ushindani na watu kutoka mataifa yaliyoendelea. Wanasema samaki mkunje angali mbichi, tutafute namna ya kuwafanya watoto wadogo wakue wakiwa na fikira huru na sio fikira iliofungwa. Kwa watu wazima ni ngumu kwani huwezi kumfundisha mbwa mzee mbinu mpya za uwindaji. Tutengeneze kizazi ambacho hata akiwa mtoto mdogo akisimama na mtoto mwenzie ambaye ni mweupe asijione kuwa yeye ni mweusi na anapaswa kunyenyekea bali ajione yeye ni mtoto na ana uhuru wa kufanya jambo kama ilivyo kwa mwenzake.

Bora kuchelewa kufika kuliko kukosa kabisa, ni lazima tufanye jambo bila hivyo tutaendelea kuonekana wanyonge milele. Chini ya jua hakuna linaloshindikana kama tukiamua kama nchi tunaweza japo najua ni ngumu sana kubadili mindset za watu.

Kama ningekuwa na uwezo 🙂 ningeeneza hata propanganda ambayo itawafanya watoto wakue wakijiamini mbele ya watu weupe. Ningeeneza propaganda shuleni ambayo ingekuwa ni sehemu ya mtaala ili kuwajengea mindset watoto tokea wakiwa shule za vidudu mpaka vyuo vikuu. Ningewatumia wazazi katika huu mchakato. Ningetumia media katika hii propaganda.

Kama tukipata kizazi kilicho na mindset huru kitaweza kusimamia vizuri rasilimali tulizonazo na kitaweza kuifikisha nchi yetu mbali zaidi kimaendeleo. Pia, kizazi hiki kitaweza kutumia potential au vipawa vyao kuleta mabadiriko chanya kwenye jamii.

Haya mabadiliko hayawezi kutokea overnight yanahitaji muda labda hata miaka mia moja ijayo. Tuandae kizazi bora kwaajili ya wajukuu zetu.

Nipo tayari kujibu hoja zenu wazalendo.
Asante!
 
Jamii zetu za kiafrika ni za kanyaga twende, (bora liende), yaani hupokea fikra chanya na hasi bila uwezo wa kuzichakata, (kuzipambanua)
 
Back
Top Bottom