Tunahitaji kuteua PhD kusimamia sanaa na filamu Tanzania?

Tunahitaji kuteua PhD kusimamia sanaa na filamu Tanzania?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Let us be serious kwenye teuzi zetu, hivi Dr. Ishengoma ni wapi amewahi kushiriki sanaa au kuigiza au kusimamia filim production? Nimetoa mfano huu baada yakuangalia viongozi wanaosimamia sanaa na filamu nchini nikaona most of them are civil servant and academician.

Tunapotaka kukuza hizi sekta tujaribu kurejesha madaraka kwa wamiliki wa sekta husika. Kuteua watu kutoa kwenye sekta nyingine nakuwaleta kwenye maeneo ya ubunifu matokeo yake ndiyo haya ya mtu kutumia mamilioni ya fedha kuzalisha filim au mziki ukitoka hewani ukapigiwa kelele kirogo tu unafungiwa.

Sanaa inakufa kwakuwa wenye sanaaa hawaongozi sanaa. Tuwape wenye vipaji kazi watengeneze ajira tupunguze tatizo la ajira nchini.
 
haya mambo unatakiwa unatoa na reference kwamba sehemu flani alipewa bob male au lili waini kuongoza sanaa na ndio maana ikafika pale ilipo. Ukisema tu bila mifano zinakua hisia, kuna watu wamefanikiwa kwenye sanaa je, uongozi wao ukoje?
 
Kwani kipindi kile cha kampeni waliwaambia nini mpaka mnajaa kwenye mikutano?
 
Wivu tu huu, kwani wenye Ph.D hawana haki ya kuongoza sekta za sanaa na ubunifu? Waliowahi kushiriki sanaa au kuigiza au kusimamia filamu wamefanya nini so far?
 
wizara ya kilimo ateuliwe mkulima kule Kilosa.

Wi ya elimu ateuliwe mwalimu wa shule ya msingi Simiyu.

Wi.madini ateuliwe Apollo mmoja kule Arusha.

Wizara ya ajira achaguliwe job less mmoja huko mazenseWizara ya maji achaguliwe muuza maji kwenye madumu huko Gongo la Mboto.

Hiyo haitakuwa nchi ni takataka.

Lini Bob Marley alikuwa waziri wa sanaa.
 
Haha! 🤣🤣 nadhani ndo anachotaka mleta hoja. Yaani akina Kingwendu wateuliwe kuongoza Idara ya Sanaa na Bodi ya Filamu.
 
Hakuna kundi ambalo sitokuja kulihurumia kwa namna yoyote ile kama hili kundi la wasanii (wa Bongo Muvi na Bongo Fleva)

Hawa wapambane wenyewe na Serikali yao inayo wajali.
 
Hao unao watetea most of them hawajielewi, na 90% ni makada, acha yaongozwe na yapigwe ban to nyimbo na movie zao.
 
Back
Top Bottom