Ufanyaji biashara Tanzania una changamoto nyingi sana, kuna utitiri wa mamlaka na vibali, sasa ipo haja ya kuwa na one business centre.
Sasa hivi unawekeza kwenye kiwanda, anakuja mipango miji mnamalizana, TRA mnamalizana, wanakuja TDFA munamalizana wanakuja EWURA mnamalizana, wanakuja NEMC mnamalizana, wanakuja OSHA mnamalizana hawa wote wanahitaji tozo na gharama mbalimbali za ukaguzi.
Fikiria unaishi nyakahanga karagwe unataka kuuza nyanya rusumo Rwanda, inabidi uende arusha kupata kibali cha kuuza mazao nje ya nchi na ukifika kule wanakwambia ufuate kibali TBS dar es salaam cha ubora.
Bora basi mtu angekuwa anaambiwa kabla ya kuanza biashara, wakati unapanga kuwekeza haya yote huambiwi unakuja kukutana nayo mbele ya safari tu.