Tunahitaji kuwa na "one business centre"

eddy

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2007
Posts
16,054
Reaction score
11,568
Ufanyaji biashara Tanzania una changamoto nyingi sana, kuna utitiri wa mamlaka na vibali, sasa ipo haja ya kuwa na one business centre.

Sasa hivi unawekeza kwenye kiwanda, anakuja mipango miji mnamalizana, TRA mnamalizana, wanakuja TDFA munamalizana wanakuja EWURA mnamalizana, wanakuja NEMC mnamalizana, wanakuja OSHA mnamalizana hawa wote wanahitaji tozo na gharama mbalimbali za ukaguzi.

Fikiria unaishi nyakahanga karagwe unataka kuuza nyanya rusumo Rwanda, inabidi uende arusha kupata kibali cha kuuza mazao nje ya nchi na ukifika kule wanakwambia ufuate kibali TBS dar es salaam cha ubora.

Bora basi mtu angekuwa anaambiwa kabla ya kuanza biashara, wakati unapanga kuwekeza haya yote huambiwi unakuja kukutana nayo mbele ya safari tu.
 
Dira na dhamira zosizoeleweka kwa wasomi wetu ndo maana tunaangaika
 
Umeongea kitu cha msingi sana mkuu mm nilishangaa nilipotaka kutoka na bidhaa south Africa zilikua zinahitaji vibali katika wizara ya export and trade,nikaambiwa niende pretoria ipo sunyside.vibali vyote nilivyokua nahitaji kuwa navyo nilipata pale na niliingia katika ofisi moja wao ndio walibeba faili langu katika ofisi zingine kupata vibali wapo so friendly hakuna rushwa ukiambiwa uje saa tano kesho ni exactly unapata document zako zikiwa tayari..panaitwa Mandela square. Umeongea kitu cha msingi sana sidhani kama tutafika ile level niliyohudumiwa pale..na izo document ni bure kuzipata ila lazima uwe nazo ili upite na bidhaa zako au magari ambayo hayatarudi tena south unaenda kufuta usajili pale..
 
Marekani pia uwa hakuna longolongo,rushwa.wala kuzungushwa.

Tanzania msipotaka mabadiliko itakula mtalalamika maisha yenu yote

mtasema marekan imeendelea aya igeni mfano wa rwanda kusajili ata kampuni ni siku moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…